Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

"Serekali ingekuwa na msimamo" .... What are you talking about??

Msimamo kama waliokwisha kuwa nao wapi? Na Lini..??

Serekali ni legelege... Ni laini ... Inasujudia ... kila kitu.... imiishiwa ..ona wanavyokimbizana na chadema mambo yasiyo na msingi...Ndio wawe na msimamo??

..Serekeali ikaonyeshe msimamo wake kwanza kwa Kile anachofanya magufuli...Ikisimamie kwa dahati maana ilikianzisha...

Serekali ikawawajibishe..Mafisadi waliokomaa..nichini

Ndio iweze kuwa na msimamo kwa Babu..

Vinginevyo serekali ndio ya kwanza kupiga foleni Lololiondo..na karibu Babu atakamata IKULU...Wait and See!!

Unataka kuona nini ili kujua kuwa hatuna nchi tena...Unataka kuona nini kujua ile Tanzania yetu haipo??

Kama tuna tiba mbadala ..tutafute Serekali mbadala...Iturejeshee nchi yetu

YES THAT IS THE BIG PICTURE OF WHAT IS HAPPENING IN LOLIONDO!!!
 
hahahahaa Mjengwa inawezekana maneno yako yakawa na ukweli kuhusu babu kule Loliondo! Lakini unategemea nini hasa katika nchi ambayo haina serikali?? unaongea serikali ipi?? Hii ambayo hata haijui mahitaji ya watu wake na wala haina uwezo wa kutoa kauli mno! Serikali ambayo watu wamepoteza imani na matumaini juu yake, Serikali ambayo haina uwezo wa kujenga mazignira shindani kwa huduma za kibinadamu! Nachelea kusema kuwa wacha watanzania wahangaike jangwani Maggid mpaka mlango wa ukombozi utakapofunka
 
Jesus walked on water. That was another abrakadabra, whatever you may call it.
 
Fikiria, maelfu haya ya watu waliopata ' Kikombe Cha Babu', kama kungekuwa na watu mia tano tu waliopona, basi, tunashindwaje kuwapata watu ishirini miongoni mwao wa kututhibitishia kisayansi, kuwa walikuwa na maradhi hayo sugu kabla na sasa wamepimwa na hawana tena
Hiyo ndo point muhimu convincing wise.
 
Halafu sasa sijui kama kuna kifungu cha sheria cha kuweza kumfanya babu kuwajibika kwa "kutoa Dawa Yake "pindi ikithibita kwamba ni feki.

Masiha Alisema kwamba Watakuja manabii wengi wa uwongo lakini mtawajua kwa matendo yao.
 
Mi nawaambia mkatae msikatae mkubali msikubali kwa macho yangu nimeona waliooenda kwa babu wamepona hao ni watu kadhaa na walikuwa na magonjwa unayoyaona kwa macho.
 
Tatizo la wabongo tumekuwa na imani haba,.
Huyo anayebisha aende ajionee jinsi kulivyokuwa na umati mkubwa wa watu kutoka mataifa mbalimbali,.je hao wote ni wajinga?
Acheni hizo waache watu wapate tiba wapone, wewe usiyeamini baki na ugonjwa wako, maana hata yesu kuna baadhi ya watu hawakumwamini japo waliona miujiza mingi,bado waliendelea kuwa na mioyo migumu,.iweje leo kizazi cha digital!
 
Bw. Maggid,

Mtu yeyote anayeumwa anachokitafuta ni tiba, basi. Wananchi wengi wameshuhudia jinsi wanavyoendelea vizuri baada ya kunywa dawa ya babu. Wengine wamepima kwenye maabara na kubainika kuwa wamepona maradhi yaliyowasumbua miaka mingi. Kuna rafiki yangu aliyenisimulia jinsi alivyoanza kujisikia vizuri usiku wa kwanza tangu anywe hiyo dawa. Leo hii, ikiwa ni wiki mbili tangu anywe hiyo dawa amepima kwa mara ya nne kwenye hospitali ya Tumbi na kupata majibu yaleyale kwamba hana HIV. Yupo rafiki yangu mwingine ambaye baba yake mzazi alikuwa anasumbuliwa na kisukari miaka mingi ilifika hatua alikuwa kama mtoto anayeugua utapiamlo. Leo hii baada ya kunywa dawa ya babu anakula kila kilicho mbele yake na afya yake ipo safi na ame-gain sana.

Sasa unachotaka kutueleza hapa ni nini Bw. Maggid?? Ukweli ni kwamba bado hujaugua kwa kiwango wanachougua wenzio na ndiyo maana unaweza hata kubeza na kuwashangaa watu wanaosafiri umbali mrefu kumtafuta huyo babu.

Kwa ujumla, huduma za afya hapa nchini ni hovyo. Watanzania wengi wanapoteza maisha yao kwa uhovyo wa huduma za afya. Inapotokea mtu anatibu maradhi yanayowasumbua muda mrefu na wagonjwa waliopona wanashuhudia hivyo, unatarajia nini? Kimsingi, sikubaliani na article yako na nasikitika misimamo yako mingi nimekuwa sikubaliani nayo tangu mwanzoni mwa mchakato wa uchaguzi mkuu uliopita. Nadhani sasa ninaweza kuhitimisha kwamba mawazo yangu mimi na wewe kamwe hayawezi kukaa mstari mmoja. Na kwa hiyo nitaacha kusoma articles zako. Aksante!
 
Maggid,

Wewe kula kwako kunategemea "porojo" unazoziandika katika magazeti - right?
 
Maggid, abracadabra kali zaidi ni jinsi Watanzania walivyoweza kudanganyika kiasi cha kumpa mtu kama Kikwete madaraka. Angalau kwa 'Babu' wa Loliondo kuna hiari, tumaini na unafuu hata kama ni wa muda but for now who really really knows !
 
Majidi na wengine watu wanapona, sisi tulio karibu na watu tunaona waliopona , tatizo la watu kutojitokeza hadharani hilo nitatizo la vyombo vya habari ya tz,kutowatafuta hao watu waliopona na wakadhibitisha au majid mpaka ndugu yako apone ndo uamini.Watu wengi wamepona we kama uhamini endelea kutoamini.Na kwaarifa yako watu kibao ambao wanakisukari wamepona kibao, ni wengi amabo nawaona huku niliko.
 
Maggid, abracadabra kali zaidi ni jinsi Watanzania walivyoweza kudanganyika kiasi cha kumpa mtu kama Kikwete madaraka. Angalau kwa 'Babu' wa Loliondo kuna hiari, tumaini na unafuu hata kama ni wa muda but for now who really really knows !

Ubarikiwe kwa mtazamo huo. Hakuna upuuzi mkubwa na wa kihistoria tuliofanya watanzania kama kumrejesha kwenye madaraka makubwa ya nchi yetu mtu anayesema hajui kwa nini watu wake ni maskini na wakati huo huo anawaahidi maisha bora kwa kila mtu!!!!!
 
Pole mjengwa, hata mimi nilipata shida ktk hili, ila ile tume ilipojiridhisha tena kwa kuipima ile na kusema eti ni sumu kali sana, ambayo eti mtu hwezi hata kuonja, hawa ma dr eti wana shangaa, sasa nikajua kuwa kumbe ile ni dawa a ukweli, sumu ile kazi ndiiyo inayoponesha
 
Mbunge Shelukindo ametoa ushuhuda kuwa amepona, mrema liyatonga amekunywa naye atakupa ushuhuda, makongoro mahanga anshashuhudia na wewe unataka nini tena.Abrakadabra ni yule shekhe SHARIFU aliyetokea kipindi cha miaka ya 99 hadi 2000.
 
Watashuhudia lakini bado hawatasadiki!Huu uponyaji ni wa kiimani zaidi,it cant be proved scientifically!Maono ya kibinadamu hayawezi kufikia maono ya muumba wao.Sumu kwa maono ya binadamu,mungu kasema iwe dawa na imekuwa!Kwa wasioamini ni kweli ile ni abrakadra kwao lakini wanaoamini ile ni tiba na wengi wamepona!Sio kazi ya kila aliyepona kumtafuta mtu kama Magid na kumshuhudia.Unaweza ukalaumu watanzania wanafata sana mkumbo,lakini vipi kuhusu watu wa mataifa mbalimbali wanavyomiminika kupata tiba Loliondo?Unaweza ukaita unabii wa uongo,lakini manabii wa uongo hutumia jina la mungu kupata mali(rejea yule wa mwenge).Huyu babu wala hanufaiki na hii tiba.Anauza 500,kati ya hizo sh.200 inaenda kanisani, sh.200 inaenda kwenye mfuko wa maendeleo ya kijiji na yeye mwenyewe anabaki na sh.100!Kweli huyu nae mwizi?Msioamini bakini na msimamo wenu.Msiwashawishi wengine hata kwa kutumia peni zenu.Acheni wanaoamini wapone!
 
Back
Top Bottom