Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Ndugu Zangu,


ABRAKADABRA ni neno lisilo na maana yoyote yenye kueleweka na kuleta mantiki. Mwenye kuongea na kujifanya anafanya vitu vya miujiza na vya kimazingaombwe kimsingi anachofanya ni abrakadabra, hata kama halitamki neno hilo. Ni mambo yasiyo na uthibitisho wa kisayansi na mara nyingi wenye kutenda hudai kuwa ’ wameoteshwa’ na kumhusisha Mungu, hivyo basi, huwezi kuthibitisha kisayansi.

Na Watanzania tunaumwa kweli. Tumekuwa wagonjwa wenye kutafuta chochote kile ili tupate nafuu ya maradhi yetu. Na ’ watalaamu’ wa tiba ya maradhi yetu wanatugombania. Ndio, ni wagonjwa tunaogombaniwa. Si tumemsikia Askofu fulani wa Kanisa la kule Mwenge, tayari amemshambulia ’ Babu’ hadharani. Anatishia kumchukulia ’ wagonjwa’ wake! Askofu nae ni ’ mgonjwa’- maradhi yake ni pesa, hatosheki.

Na si tumemsikia ’ Babu’ wa Loliondo anavyojisifu na kujitangazia unabii? Anasema; “Na kama nilivyokueleza, mimi ni Mchungaji mstaafu lakini pia ni “Nabii” ambaye naweza kuona maono au ndoto na kuzungumza na Mungu mara kwa mara . Na yote ninayoyatekeleza kama unavyoona ni maagizo ya Mwenyezi Mungu.”
“Nimefanya kazi za uchungaji tangu mwaka 1967 katika sehemu kadhaa nchini hadi mwaka 1989 nilipohamishiwa katika eneo hilo. Na nimefanya kazi za uchungaji hapa hadi nilipostaafu mwaka 2002”

‘Nilianza kuota maono na kusikia sauti ya Mungu tangu mwaka 1991 ikinieleza kuwa nibaki kuishi eneo hili; kwani Mungu alikuwa anataka kunipa kazi maalumu ambayo kwa wakati huo sikuifahamu” ( RAIA MWEMA NA: 176)

Sitatafuna maneno bali kuweka bayana, kuwa hayo ya ’ Babu’ wa Loliondo ni abrakadabra. Kwa wajanja neno hili Abrakadabra ni neno la ajabu, neno la miujiza. Kwa kawaida neno hulala, lakini abrakadabra laweza kusimama katika pembe tatu.

Zama hizi, ambapo watu wengi wamekumbwa na hali ya umasikini mkubwa, ujinga na maradhi, kumeibuka manabii wa siku za mwisho. Wenye kunufaika na hofu za wajinga, masikini na wenye maradhi kwa kutumia abrakadabra. Lakini abrakadabra inatumika pia kututoa kwenye kujadili mambo yetu ya msingi.


Manabii hawa wa kujitangaza hufika mahala wakawa na nguvu kiasi cha kuwa na ushawishi mkubwa. Mwandishi Danny Sofe katika kitabu chake; "His Exellency Head Of State" (Mheshimiwa Mkuu wa Nchi) anabainisha hili kwa kumchambua mmoja wa wahusika wakuu katika kitabu hicho. Moses Akaba,


Bwana huyu, Moses Akaba alikuwa Mwalimu na msomi wa uchumi na maarifa ya Biblia. Mwanafunzi mmoja wa shule yake alianguka ghafla na kuzimia. Alipelekwa hospitalini na kudhaniwa kuwa amekufa, mara alizinduka ghafla. Akaelezea kisa chake, kwamba alijikuta akiwa kwenye handaki jembamba na lenye giza. Mwisho wa handaki hilo kulikuwa na mwanga.



Alipoukaribia mwanga alimwona mtu aliyevalia joho jeupe. Mtu huyu alimwambia kuwa Mungu alimtaka arudi tena duniani kwa vile kazi aliyotakiwa kuifanya duniani alikuwa hajaimaliza. Kwamba wazazi wake masikini walimwihitaji.


Kijana huyu aliamini kuwa mtu yule mtakatifu aliyekutana naye kwenye mpaka wa mauti na uhai alikuwa Moses Akaba, mchumi na msomi wa maarifa ya Biblia na ambaye alikuwa mwalimu katika shule ya kijana yule. Baada ya kusikia kauli ya kijana yule, Moses Akaba akajitangaza kuwa nabii, akaanzisha kanisa la Life-After -Life (Maisha Baada ya Maisha.)


Nabii Akaba alikuwa hodari sana wa kulitawala jukwaa na kuzungumza katika hadhara. Akaba alikuwa na mbinu na uwezo mkubwa wa kushawishi. Watu wengi na hasa masikini walijiunga na kanisa lake. Walichanga pesa na vito vyao vya thamani.



Na Watanzania tunazidiwa na WaNigeria tu katika dunia hii katika mambo ya abrakadabra. Na foleni za kwa ' Babu' Loliondo zitapungua mara ile Watanzania watakapoamka kuwa abrakadabra ya ' Babu' ni miyeyusho. Lakini kwa vile bado tunaumwa, basi, tunabadilisha ' hospitali'.



Naam. Hakuna lililo bora kwa mwanadamu kama kuwa na hekima. Kwa mwanadamu, kuelewa jambo hutanguliwa na kutanabahi. Ina maana ya kufikiri kwa umakini na kugundua undani wa mambo. Ni bahati mbaya, kuwa wengi wetu tu wavivu sana wa kutanabahi.


Ndio, tumekuwa ni watu wa kufuata mkumbo wa fikra, hatujipi tabu ya kutanabahi. Jambo hili laweza kuwa na madhara makubwa. Zamani sana alipata kutokea mtabiri wa nyota katika mji mmoja mdogo kule Ulaya.



Huyu alitawatabiria watu wa mji huo , kuwa katika tarehe fulani kungetokea kimbunga kikubwa. Kimbunga hicho kingeangamiza majengo na kuna watu wangepoteza uhai. Salama yao? Ndio, pindi dalili za kuanza kwa kimbunga hicho zingeonekana, basi, wakazi wa mji huo waharakishe kuelekea Kaskazini ya mji huo kuliko na milima.


Jioni moja giza lilianza kuingia katika siku iliyotabiriwa. Ikafika saa tatu za usiku bila kuonekana kwa dalili za kimbunga. Ghafla, bwana mmoja kupitia dirisha lake aliona gari likitoka kwa kasi ya kutimua vumbi kutoka nyumba ya jirani. Bwana yule aliamini kuwa kimbunga hicho sasa kimeingia kwenye mji wao na kwamba jirani yake alikuwa akikimbia na familia yake kuokoa maisha yao.


Bwana yule naye akaamrisha familia yake kuingia ndani ya gari. Naye akaondosha gari lake kwa kasi ya kutimua vumbi kuelekea Kaskazini ya mji. Mwenye nyumba nyingine baada ya kuona gari mbili zikipita kwa kasi nje ya nyumba yake, naye akaamini kimbunga kilichotabiriwa kimewadia. Akabeba familia yake na kutimua vumbi na gari lake. Kuona hivyo, wakazi wa mji huo, mmoja baada ya mwingine, wakaanza kukimbia mji wao kuelekea Kaskazini wakihofia kimbunga. Kijiji kizima kikahama!


Huko walikokimbilia wakaanza kuulizana; Ilikuwaje? Ikabainika, kuwa yule bwana wa kwanza aliyevurumisha gari lake alikuwa amegombana na mkewe, na aliamua kuondoka nyumbani kwake akiendesha gari kwa kasi akiwa na hasira, basi. Na hasira zilipomwisha akajirudia nyumbani kwa mkewe!

Tuna cha kujifunza katika kisa hicho. Si tunaona, kuwa sasa kila mmoja anamzungumzia ’ Babu’ wa Loliondo. Wengi wanafunga safari kwenda Loliondo. Hatutumii muda mwingi kujiuliza; Ya kwa ’ Babu’ Loliondo yalianzaje? Na je, kama ’ Babu’ wa Loliondo ana dawa ya kutibu kansa, kisukari na hata UKIMWI kuna uthibitisho wa Kisayansi?


Na mengine ni rahisi kuyapima hata kwa masikio kujua kama kuna ukweli. Fikiria, maelfu haya ya watu waliopata ’ Kikombe Cha Babu’, kama kungekuwa na watu mia tano tu waliopona, basi, tunashindwaje kuwapata watu ishirini miongoni mwao wa kututhibitishia kisayansi, kuwa walikuwa na maradhi hayo sugu kabla na sasa wamepimwa na hawana tena.


Ni mtazamo wangu, kuwa hii ya kwa ’ Babu’ Loliondo ni Abrakadabra nyingine. Serikali ilikuwa haina sababu ya kubabaika katika kulitolea msimamo hili la Loliondo. Msimamo wa awali ulikuwa sahihi kabisa; kusimamisha zoezi la utoaji wa tiba hiyo mpaka Serikali itakapojiridhisha juu ya dawa hiyo kupitia uchunguzi wa kisayansi.


Ndio, Serikali ilipaswa kuueleza umma, kuwa kwa sasa dawa hiyo haitambuliki kisayansi, haijafanyiwa uchunguzi, inahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kuhakikisha, sio tu kama inatibu, bali kama ina madhara kwa mwanadamu. Hilo ni jukumu la Serikali katika kulinda usalama wa watu wake. Na huko hakutakuwa kuingilia masuala ya imani za watu.
Maggid
Dar es Salaam.
Jumatatu, Machi 14, 2011
http://mjengwa.blogspot.com

Acha uzushi, huna hata aibu kupotosha umma, yaani umepinda mgongo kuandika upupu, shwain
 
Nashangaa kuona wapo wa2 wanageuza eneo hli kuwa uwanja wa ma2c, ugomvi na fkra mgando. Coni sababu ya wao kutukanana... Mazee ths is the GREAT THINKERS FIELD. Mmeshndwa kufkr kwamba swala la kwa babu lpo kiiman zaid.. Hebu fkr kwann kama hao wanasayans waliotumwa walsema ni "sumu" iweje serkal iruhusu watu kuendelea?

Mjengwa! Hoja ya kwamba hakuna mtu aliepona na kujtokeza kukr hlo sion msing wake kwan kama umeweza kunukuu vtabu mbalmbal bas hata magazet unasoma ambayo meng yameandka ushuhuda wa weng wao, mi mwenyewe shangaz yangu alkuwa na presha na ksukar na sasa ni zaid ya mzma, kunamama (jiran yetu) alkuwa na cancer ya kzaz kwa kias kwamba hadi tumain la maisha llshapotea, sahv ni mzma na anafanya mambo yake peke yake.
Ni kwel kwamba hata biblia imeandka kuhusu siku za mwsho na mambo yatakayotokea, manabii wa uongo ni sehem mojawapo lakn biblia hyo hyo imeandka kuhusu kla m2 na kpawa alchopewa na mungu istoshe kla mtu yupo dunian kwa kusudi maalum la mungu. Na hvo Mungu pekee anajua namna ya kuwasliana na watu wake kuwatuma kutimiza kusudio lake.
Sikunym wala kukulazmisha kuwaza niwazavyo mimi
 
Tatizo la wabongo tumekuwa na imani haba,.
Huyo anayebisha aende ajionee jinsi kulivyokuwa na umati mkubwa wa watu kutoka mataifa mbalimbali,.je hao wote ni wajinga?
Acheni hizo waache watu wapate tiba wapone, wewe usiyeamini baki na ugonjwa wako, maana hata yesu kuna baadhi ya watu hawakumwamini japo waliona miujiza mingi,bado waliendelea kuwa na mioyo migumu,.iweje leo kizazi cha digital!

So wewe unaamini kwa sababu ya umati wa watu wengi unaoenda huko?
 
Maggid, abracadabra kali zaidi ni jinsi Watanzania walivyoweza kudanganyika kiasi cha kumpa mtu kama Kikwete madaraka. Angalau kwa 'Babu' wa Loliondo kuna hiari, tumaini na unafuu hata kama ni wa muda but for now who really really knows !
Well said.
 
Hivi ni lini atatokea "babu" mwingine atakaetuletea tiba ya matatizo ya kijamii? naombea atokee "babu" aje na dawa ya mgao wa umeme, foleni zisizoisha, dawa ya maji ya uhakika, utawala bora na kuutokomeza ufisadi.

Nadhani atakuwa kesha oteshwa ila time will tell.

My take.

Ya babu wa loliondo inathibitisha kuwa matatizo yetu hayataweza kuja kutatulika kisayansi ila kwa "ABRAKADABRA"
 
Magid, unapotumia kalamu yako kupotosha watu si vyema na hauwatendi haki, watu wanaoishi kiimani, wewe ni mwislamu, hata siku moja hauwezi kuishi kwenye imani ya kikristo, katika ukristo kuna maono na kuna kutokewa na roho mtakatifu, sasa ni vyema jambo usilolijuwa ukakaa kimya kuliko kudandia treni kwa mbele, hivi wewe ukiwa kama muislamu utajisikiaje mtu akisema marehemu mtume Muhamad SAW, ingawa ni kweli hayuko duniani? acha kukebehi imani za watu. sheikh Yahya miaka nenda rudi anafundisha watu hadharani jinsi ya kutengeneza majini na hatujawahi kuwasikia mkisema akadagabra, leo mchungaji anatoa dawa bure kwa sababu ya udini uliokujaa imekuwa nongwa, nakupa changamoto nenda kwa JK KWA SABABU HUWA ANAKUTUMIA SANA PALE ANAPOKUHITAJI, na umuulize ile dozi aliyokunywa kwa babu imemsaidia au hamna kitu?
 
Inashangaza sana kwa makala hii kuwa kali kiivyo. Kwani huyu mleta mada kaingiliwa kiasi gani na mwinjilist hadi kumdamkia? Kuna msemo wa wahenga husema, waache wafu wawazike wafu wao. Tena kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji.
 
Hod hodi Jf mimi ni mgeni humu nawasalimia.

Nimevutiwa na hii topic ya Babu wa Loliondo. Baba yangu mzazi ameenda huko siku tatu iliyopita. Anaugua cancer ya mifupa na kisukari. Mimi nimeokoka na baba yangu ni mkatoliki. Baba yangu aliombewa na kupona maumivu yaliisha na afya yake ikawa inaendelea kutengamaa. Sasa kwakua giza na mwanga haviwezi kukaa pamoja nilimshauri baba asiende kwani mm nilikuwa naona anahisi tu kwamba hajapona kutokana na ukubwa wa magonjwa aliyokuwa nayo kwahiyo hisia zake ndo tatizo. Ilikuwa aende wiki moja iliyopita. Nikaomba Mungu, anipe ishara kama hayo si mapenzi yake na tukatukabaliana na Mungu itokee pingamizi, kesho yake serikali ikatangaza imesitisha huduma ya babu. Hiyo ikawa kwangu uhakika kuwa hapo kuna walakini. Nikamshukuru Mungu kwa hilo. Baada ya siku mbili hilo tangazo sijui ikawaje nikaona baba na kaka yangu wanapanga safari. Nikamsihi sana baba asijepoteza utukufu wa Mungu kwa kuabudu miungu mingine asiyoijua, baba akakubali kaka yangu akakataa. Sasa nimewaambia kati ya Mungu wa Loliondo na wakwangu kama hawatendi kazi na roho mmoja mmoja lazima awe mwongo na kama ni roho ile ile basi baba afya yake itatengamaa. Kama sivyo lazima ugonjwa uzidi kuliko ulivyo mwanzo nahapo Mungu wangu mimi nitamwita kushuhudia kuwa ndiye Abba na Yehova Yire (Mungu mponyaji).

Nitaleta huu ushuhuda. Iwapo baba atapona basi huyo Mungu atakuwa ndiye Mungu wangu pia hivyo nitarudi kumshuhudia hapa na nitampa sifa na utukufu na aibu yangu nitaitangaza ili yeye abakiye mwenye kuabudiwa na kutukuzwa. Kama siye basi hali ya baba nitaithibisha kwenu na baada ya hapo nitamwombea na kuondoa huyo pepo wa maradhi. Na shukuru Mungu haya kutokea maana baada ya hapa injili itajithibitisha nyumbani kwetu na nguvu ya udini itaondoka.

Mbarikiwe na bwana.
 
Hana anayempotosha, ukisoma jina lake tu hapo chini unaelewa ndo wale waleeee, wanaokwendaga kwenye mihadhara kutukana dini za wenzao. Hana ajualo wala analoelewa. Baba mwenye nyumba mwenyewe kakimbilia huko na keshapata dozi, kamuulize. Looh! Watu wengine wadhani kuandika saaaaanaaaa kurasa kitabu ndo tutakubali hadithi yako iliyojaa udini na kutoelewa usemacho??? Toka lini Muislamu ukayajua ya Ukristo kama sio kutaka kuleta upupu tu hapa ukumbini??? Acha niishie hapa nisiendelee maana.... :smash:

Kama limetoka kwa Bwana hata uje na nguvu gani hutaweza kulizuia na waliokusudiwa watapata baraka zao. Kalagabaho!
 
Huyu majid ni vuvuzela la mambo ya udini na si lolote wala chochote kama imani yako haihusiki kinakuuma nini?shut up!!!!
 
Magid, unapotumia kalamu yako kupotosha watu si vyema na hauwatendi haki, watu wanaoishi kiimani, wewe ni mwislamu, hata siku moja hauwezi kuishi kwenye imani ya kikristo, katika ukristo kuna maono na kuna kutokewa na roho mtakatifu, sasa ni vyema jambo usilolijuwa ukakaa kimya kuliko kudandia treni kwa mbele

...one time i agree with Matola!!
 
Hod hodi Jf mimi ni mgeni humu nawasalimia.

Nimevutiwa na hii topic ya Babu wa Loliondo. Baba yangu mzazi ameenda huko siku tatu iliyopita. Anaugua cancer ya mifupa na kisukari. Mimi nimeokoka na baba yangu ni mkatoliki. Baba yangu aliombewa na kupona maumivu yaliisha na afya yake ikawa inaendelea kutengamaa. Sasa kwakua giza na mwanga haviwezi kukaa pamoja nilimshauri baba asiende kwani mm nilikuwa naona anahisi tu kwamba hajapona kutokana na ukubwa wa magonjwa aliyokuwa nayo kwahiyo hisia zake ndo tatizo. Ilikuwa aende wiki moja iliyopita. Nikaomba Mungu, anipe ishara kama hayo si mapenzi yake na tukatukabaliana na Mungu itokee pingamizi, kesho yake serikali ikatangaza imesitisha huduma ya babu. Hiyo ikawa kwangu uhakika kuwa hapo kuna walakini. Nikamshukuru Mungu kwa hilo. Baada ya siku mbili hilo tangazo sijui ikawaje nikaona baba na kaka yangu wanapanga safari. Nikamsihi sana baba asijepoteza utukufu wa Mungu kwa kuabudu miungu mingine asiyoijua, baba akakubali kaka yangu akakataa. Sasa nimewaambia kati ya Mungu wa Loliondo na wakwangu kama hawatendi kazi na roho mmoja mmoja lazima awe mwongo na kama ni roho ile ile basi baba afya yake itatengamaa. Kama sivyo lazima ugonjwa uzidi kuliko ulivyo mwanzo nahapo Mungu wangu mimi nitamwita kushuhudia kuwa ndiye Abba na Yehova Yire (Mungu mponyaji).

Nitaleta huu ushuhuda. Iwapo baba atapona basi huyo Mungu atakuwa ndiye Mungu wangu pia hivyo nitarudi kumshuhudia hapa na nitampa sifa na utukufu na aibu yangu nitaitangaza ili yeye abakiye mwenye kuabudiwa na kutukuzwa. Kama siye basi hali ya baba nitaithibisha kwenu na baada ya hapo nitamwombea na kuondoa huyo pepo wa maradhi. Na shukuru Mungu haya kutokea maana baada ya hapa injili itajithibitisha nyumbani kwetu na nguvu ya udini itaondoka.

Mbarikiwe na bwana.


Haueleweki hata unachotaka kutuambia, mara unataka kumuombea baba yako mara aende akirudi ndio utoe ushuhuda, hivi ni lini babu wa Loliondo aliwahi kujitangaza kwamba yeye ni mungu? wewe huna cha ulokole wowote, ni mtu tu ambaye umeshakuwa brain washed na wajanja wachache wanaoishi kwa kutegemea fungu la kumi kwa gia ya ulokole, in short wewe ni mjinga tu kama wajinga wengine.
 
Back
Top Bottom