Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Nimepata taarifa kwamba waliokunywa dawa ya abu wa liliondo sasa wanaanza kuumwa na matumbo. waanza kuvimba. TAYARI Jjamaa, ndugu na marafiki wa karibu wanafanya harakati za kumkimbiza muhimbi ili aangalie nini kimezidi. lkn anavyosmea yeye mwenyewe kwamba maumivu hayo yamekuja baaa ya kunywa dawa hiyo.haya nimeyapata kutoka kwa mmoja wa mtumiaji AMBAE AKIIMWA NA UKIMWI.

Yaani hata baada ya ku-edit bado spelling mistakes zipo kibao, halafu unajiita muhadhiri.......mmmh! kweli wadogo zetu huko vyuoni wana shida.......naona na wewe pia unahitaji kikombe cha babu vilevile!
 
1. Kodo lyako huelewi chochote, yaani uko km wepa za gari tena jeifong.

2. Kwa vyovyote wewe utakuwa unapumuliwa kisononi.

3. Km sivyo, baisi umekalia kitu kigumu ktkt ya makalio yako kinakufanya uwe kihereherehre

du we mjinga nimekubali we ni mpasua jibu , na hapa umepasua MJIPU na sio jipu
 
huyo ni mkirsto, tena KKT haamini kagera. amekimbili kwa babu. lkn thari yake sasa hiyo. anavimba tumbo. amezidisha marazi
Asee!!!kumbe wakristo hawaamini Magomeni kagera eeeh!!!wanaoamini ni akina nai hao?????
Utawajua tu!
 
Wakati watanzania wakimiminika kwenda wilayani Loliondo,kwa Babu kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hajapona hata mmoja.

... “Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?”
 
Kwa vyovyote vile hizi ni habari nzuri.

pia

ni wakati wa watafiti makini kujichukulia fursa....kujaribu kuja na kitu more objective!!!

Midaktari ya Tanzania inasubiri serikali itoe hela, watakuja wazungu wafanye mambo tutaanza kulalamika tena oooohhh, kitu kitarushwa hewani na wazungu na kujipatia Ujiko...
 
imani ndugu... Na dhambi kama uazo nyingi huponi
' but we jamaa tupe source or link
 

Tuesday, 15 March 2011
Shija Felician, Igunga


WAKATI Watanzania wengi wakimiminika kwenda wilayani Loliondo, mkoani Arusha kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hawajapona.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapigakura uliofanyika kwenye Viwanja vya CCM wilayani Igunga, Tabora mbunge huyo alisema haiamini dawa hiyo kwa kuwa ana ushahidi kwa ndugu zake hao ambao anadai kwamba wanaendelea kuugua kisukari licha ya kutumia dawa hiyo siku saba zilizopita.


Aliwataka wale watakaokwenda Loliondo ambao wanatumia dawa za hospitalini kuendelea kuzitumia badala ya kuzipuuza na kuzitupa... "Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?"


Hata hivyo, aliwataka wananchi wote wenye imani juu ya dawa hiyo waende huku akiwasisitizia kutopuuza ushauri wa madaktari kwani.


Wakati Rostam akipinga dawa hiyo, wilayani Kahama, mamia ya wafanyabiashara wamefunga shughuli zao na kukimbilia Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile kunywa dawa hiyo huku baadhi ya waliorejea baada ya kuinywa wakidai kuwa hali zao sasa ni nzuri.


Wafanyabiashara hao wengi wao wanaondoka kwa siri wakidai wanakwenda Dar es Salaam katika shughuli zao, lakini siri imefichuka baada ya baadhi yao kuoneka katika runinga wakiwa katika foleni wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.


Mbali ya kuzungumzia suala hilo la tiba ambalo limegusa hisia za wananchi wengi wa Afrika Mashariki, mbunge huyo aliwapa pole wananchi wa Igunga ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha wiki iliyopita ambazo ziliathiri kaya 19. Aitoa msaada wa Sh500,000 kwa kila kaya iliyokumbwa na maafa hayo.


Chanzo: Mwananchi - 16/3/2011
 
Akawaulize wenzake walioenda watamwambia; wanaona wivu hospitali zao za kifisadi hazijai?? Na bado, sisi tutaenda kwa babu bwana, 500 tu
 
Tihi tihi tihiii, tutasikia mengi na hata bubu watanena mwaka huu. Vipi kale kacheki ka malipo amekwisha kapokea nini! Huyu Babu amepunguza makali ya hoja hivi sasa watu wanapumua na kuweza kuto maoni yao mpaka magazetini
 
Akawaulize wenzake walioenda watamwambia ;wanaona wivu hospitali zao za kifisadi hazijai?? Na bado, sisi tutaenda kwa babu bwana, 500 tu

Low thinkers utawafahau tu. Chuki zao zipo kila mahali, Hayo ni mawazo yake Rostam, si kila kitu mnakipeleka katika siasa. Mnona tunaambiwa Lowassa nae kapata kikombe na ametoa magari na nauli za kuwapeleka wapiga kura wake kwa babu?

Zaidi ya yote, mbona Kadinari PENGO wa RC, MWINGIRA wa EPHATA, KAKOBE wa FGBF, Askofu MUSHI wa KANISA HALISI LA AFRIKA na Gazeti la ANNUR wote wamemponda Babu? Kakobeamemuita Babu kuwa ni wakala wa Shetani na Mwingira amemlaani Babu!

Si kila kitu ni siasa. Kama hamuwezi kufikiri deeply, hameni JF
 
Litakuwa limechakachua foleni kama kawaida yalo! Yani ufisadi kila mahali....
 
Low thinkers utawafahau tu. Chuki zao zipo kila mahali, Hayo ni mawazo yake Rostam, si kila kitu mnakipeleka katika siasa. Mnona tunaambiwa Lowassa nae kapata kikombe na ametoa magari na nauli za kuwapeleka wapiga kura wake kwa babu?

Zaidi ya yote, mbona Kadinari PENGO wa RC, MWINGIRA wa EPHATA, KAKOBE wa FGBF, Askofu MUSHI wa KANISA HALISI LA AFRIKA na Gazeti la ANNUR wote wamemponda Babu? Kakobeamemuita Babu kuwa ni wakala wa Shetani na Mwingira amemlaani Babu!

Si kila kitu ni siasa. Kama hamuwezi kufikiri deeply, hameni JF

Utahama wewe humu JF, usiejua mwelekeo wa dunia unaenda wapi? Very low thinker..

Kwa sisi tulioona ndugu zetu wamepona,siwezi kuona watanzania wakipotoshwa na vidampa kama wewe na bosi wako ra. Kama hamna la kuongea ni vema mngekaa kimya,kuliko kutoa ushuzi wenu haf hadharani sasa

Jambo usilolijua n kama usiku wa giza,kaeni kimya punguzeni viherehere! Zaidi ya hapo ndio tunapokuja kuona ni mambo ya maslahi zaidi, kama vile kakobe amekosa waumini! Sasa ra hospitali zake zimekosa wagonjwa,nk nk. Na wewe kidampa Kauza umetumwa kwa njaa zako, nk
 
Midaktari ya Tanzania inasubiri serikali itoe hela, watakuja wazungu wafanye mambo tutaanza kulalamika tena oooohhh, kitu kitarushwa hewani na wazungu na kujipatia Ujiko...


.. Kujiamini, kujisimamia na kujituma ... mambo haya hatuna... sio tamaduni zetu..

kutathmni mambo kama haya ...rahisi tu ...kujituma na kujiamni ...atakuja kijana mdogo wala hana uzoefu kama mababu ma dokta wa hapo Muhimbili ...atajichukulia sifa kirahisi...!!
 
Wakati watanzania wakimiminika kwenda wilayani Loliondo,kwa Babu kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hajapona hata mmoja.

... Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?
Hao wamepungukiwa na imani bila shaka kwn Mi nimeshuhudia jamaa ndg waliokuwa hoi bin taaban wakipona.
 
Jamani JF ina nafasi kwetu wote - tujitahidi kutawala hamasa zetu katika maandishi.
 
Mbunge wa igunga,rostam aziz amesema dawa ya mchungaj mwasapile haitibu
source-jamboleo

mwambie amtafute mheshimiwa Mrema ampe full hbr kuhusu hiyo dawa ndo atajua km inatibu au la!!!!!!mrema anakwambia c unaona ht nimeanza kutakata...........
 
Back
Top Bottom