Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Kwa kuanzia hili la mdhara ndio la muhimu zaidi na kwa kweli wamechelewa kuifanyia kazi na kutoa matokeo. I just cant imagine kama wangesema ina madhara....ukizingatia maelfu waliokwisha kunywa pamoja na viongozi kadhaa! Ni kweli kila dawa ina side effects lakini ni kwa kiwango gani cha madhara ukilinganisha na faida yake kwa mtumiaji.

kama kweli walikuwa wanaangalia madhara kwa nini waliacha watu waendelee kunywa?huoni results zinaweza kuwa biased?
Sijawahi kuona dawa isiyo na madhara regardless umuhimu wake kama dawa.kwa hiyo watoto,wazee,vijana,wajawazito,wenye magonjwa ya figo na ini wote hawatapata madhara!poor tanzania ujinga unatuangamiza!
Wanachotakiwa kufanya ni kusitisha matumizi ya hicho kikombe mpaka pale itakapogundulika ni dawa.
 
Hivi kweli serikali haioni madhara ya kumuendekeza huyu babu wa KKKT(Kunywa Kikombe Kimoja Tu). Tunaambiwa wanakufa watu sio chini ya watano kwa siku.

Mbona malaria ina dawa na watu wanakufa????
wengi wanafia njiani kabla hawajapewa dawa na wapo wanokufa vilevile baada ya kunywa dawa tusubiri kupata taarifa kamili kutoka kwa wataalam
 
WC yaelekea una chuki binafsi na Mchungaji, vifo ya watu huko Loliondo hayatokani na madhara ya kikombe anachotoa Babu huyo bali ni kukosa huduma hiyo ya matibabu kwa muda muafak kutokana na wagonjwa hao kuzidiwa

Chuki binafsi itoke wapi ndugu yangu. Viongozi wa serikali waache kumnadi mzee huyu. Waende kimyakimya kama wanavyokwenda kwenye matibabu mengine na wanapokwenda "gesti".
 
Hivi kweli serikali haioni madhara ya kumuendekeza huyu babu wa KKKT(Kunywa Kikombe Kimoja Tu). Tunaambiwa wanakufa watu sio chini ya watano kwa siku.

Mkuu una dispensary maeneo ya loliondo? naona unaongea as if wateja kwako wamepungua
 
kama kweli walikuwa wanaangalia madhara kwa nini waliacha watu waendelee kunywa?huoni results zinaweza kuwa biased?
Sijawahi kuona dawa isiyo na madhara regardless umuhimu wake kama dawa.kwa hiyo watoto,wazee,vijana,wajawazito,wenye magonjwa ya figo na ini wote hawatapata madhara!poor tanzania ujinga unatuangamiza!
Wanachotakiwa kufanya ni kusitisha matumizi ya hicho kikombe mpaka pale itakapogundulika ni dawa.

Ndio maana nimesema wamechelewa kufanya hilo.

Ni kweli kila dawa ina madhara lakini ni lazima madhara hayo yapimwe kwa kulinganisha na manufaa yake.

Let say kuna dawa inatibu HIV lakini pia dawa hiyo inafanya mtu ana paralyse mwili mzima for good......na kuna 'dawa' nyingine haitibu HIV lakini inamwongezea mgonjwa maisha (ARVs) lakini inasababisha watumiajji wanakuwa ni 'vitambi' vya wastani hivi. Katika situation hii kwa maoni yangu dawa/tiba ya pili ni bora zaidi kuliko ya kwanza.
 
Vifo vya wagonjwa wa kisukari mwezi 2/3 lazima vizidi vifo vitokanavyo na malaria!
 
sasa dawa ya babu iko kundi lipi hapo?kwa mujibu wa watafiti wetu dawa ya babu haiko kundi lolote hapo!(haina madhara) sasa huu si uhuni?
 
Hivi kweli serikali haioni madhara ya kumuendekeza huyu babu wa KKKT(Kunywa Kikombe Kimoja Tu). Tunaambiwa wanakufa watu sio chini ya watano kwa siku.

Mbona Makka wanakufa sana watu? lakini hijja ile haijazuiwa unanini wewe?
 
Hivi kweli serikali haioni madhara ya kumuendekeza huyu babu wa KKKT(Kunywa Kikombe Kimoja Tu). Tunaambiwa wanakufa watu sio chini ya watano kwa siku.
wild card ushindwe na ulegee wacha kumkashifu babu tena inaonekana wewe ni mgonjwa inabidi ukanywe kikombe wacha longolongo nyie wote ni watu ambao hamlitakii mema taifa la tanzania mnaleta ubaguzi wa dini na ukabila,
 
Mhh hii kali, wanawezaje kuyapima madhara yanayosababishwa na kunywa dawa kwa muda mfupi namna hiyo??? Je wametumia vigezo gani kufikia jibu walilolitoa??? Je ikitokea baada ya miezi sita au miaka 2 watu wote waliokunywa dawa ya Babu wanaugua magonjwa yanayofanana, wizara itatuambiaje???? Jamani wizara ingejitoa kabisa katika hesabu ya hii dawa. Kama ambavyo haithibitishi dawa nyingine za tiba asili, basi na hii waichukulie kama moja ya tiba ya asili, ambapo mgonjwa hutumia dawa for his or her own risks. Kujiingiza kwa serikali kichwa kichwa katika hili, mambo yakija geuka itashindwa pa kutokea.
 
Vifo vya wagonjwa wa kisukari mwezi 2/3 lazima vizidi vifo vitokanavyo na malaria!

Malaria kwa siku inauwa watu takribani 160 nchini Tanzania. Ni wagonjwa wangapi wa kisukari wamekufa kwa kisukari baada ya tiba ya babu au wakati wakisubiri tiba ya babu?
 
sasa dawa ya babu iko kundi lipi hapo?kwa mujibu wa watafiti wetu dawa ya babu haiko kundi lolote hapo!(haina madhara) sasa huu si uhuni?

Kwenye mfano wangu, labda kundi la pili:A S-coffee:! Hata hivyo sijasema kuna makundi hayo mawili tu...nimetoa mfano kujaribu kukuonesha considerations ya benefts na side effects za dawa!
 
Mhh hii kali, wanawezaje kuyapima madhara yanayosababishwa na kunywa dawa kwa muda mfupi namna hiyo??? Je wametumia vigezo gani kufikia jibu walilolitoa??? Je ikitokea baada ya miezi sita au miaka 2 watu wote waliokunywa dawa ya Babu wanaugua magonjwa yanayofanana, wizara itatuambiaje???? Jamani wizara ingejitoa kabisa katika hesabu ya hii dawa. Kama ambavyo haithibitishi dawa nyingine za tiba asili, basi na hii waichukulie kama moja ya tiba ya asili, ambapo mgonjwa hutumia dawa for his or her own risks. Kujiingiza kwa serikali kichwa kichwa katika hili, mambo yakija geuka itashindwa pa kutokea.

Kwa kuzingatia idadi ya watu wanaoweza kushawishika kutumia dawa hiyo...serikali haiwezi kujitoa, ni lazima ifanye wajibu wake. Kumbuka pia magonjwa yanayozungumziwa ni yale ambayo wanasayansi bado wanakuna vichwa kupata tiba zake. So nadhani approach ya serikali imekuwa ni kuipa dawa ya babu 'the benefit of the doubt'. kama itatokea kwamba dawa hiyo inatibu kweli...serikali si bado italazimika kuingilia kati?
 
Serikali yetu inapenda kufanya kila kitu kiwe kigumu.

Hivi serikali imeshindwa kuchukua wagonjwa 10 ambao wamekubali binafsi kutumiwa kufanyiwa research ya hio dawa? Serikali kwa kuwalipa fidia hao wagonjwa wangeshapata jibu kamili zamani sema kama kawaida yao wataanza na mambo ya tume mwisho hakuna jibu kamili.

Tafuta wagonjwa kumi wapimwe kabla na baada ya kunywa dawa kwa mda uliotajwa na babu wangetoa majibu kamili. Na kama jibu lingekuwa lina utata wangefanya tena.

Ni ajabu sana kuona hili swala bado halina jibu kamili mpaka leo.

Na hatuwezi kuwalaumu watu wanaoenda kunywa dawa hata kama hawana huakika wa kupona kwani inawezekana washa jaribu njia zote na hawaoni hatari kujaribu hii.

Kila la kheri wagonjwa wote walioenda kwa babu na ambao hawajaenda, Mungu hawape nafuu na mueze kupona kwa njia yoyote hile.
 
Kila mtu na imani yake,kama huoni ina umuhimu kwako ipotezee,kama ni muhimu basi kubaliana na yote.
 
Attachments

Malaria kwa siku inauwa watu takribani 160 nchini Tanzania. Ni wagonjwa wangapi wa kisukari wamekufa kwa kisukari baada ya tiba ya babu au wakati wakisubiri tiba ya babu?

sijui!lakini baada ya kukusanya data za mwezi wa 2 na 3 utayakubali maneno yangu.
 
Kwenye mfano wangu, labda kundi la pili:A S-coffee:! Hata hivyo sijasema kuna makundi hayo mawili tu...nimetoa mfano kujaribu kukuonesha considerations ya benefts na side effects za dawa!

ukweli ni kwamba 'dawa' ili iitwe dawa lazima itibu huku ikileta madhara kidogo kwa mtumiaji au kwa kundi kubwa la watu.hakuna kisicho na madhara duniani hata chakula tunachokula.
Nazidi kuona maajabu ya dawa hii ya babu,haina madhara!
 
hii dawa nami naiamini kwa kiasi fulani lakini hili suala la ushahidi linaleta utata. Ofisini kwetu kuna mtu ana sukari/hiv lakini tangia arejee kutoka Loliondo ni zaidi ya majuma mawili lakini hatwambii lolote!

hilo ndo tatizo. Tunahitaji ushahidi pleeees!
 
mzee wa upako nae nimemsoma kwenye gazeti la jioni hii Dar Leo nae kaanzisha yake,anasema ni kiboko kuliko ya babu.
Swali: walikuwa wapi siku zote?
 
Back
Top Bottom