Mjadala kuhusu Mke asiye wa Ndoa na Mtoto wa nje ya Ndoa kwenye urithi

Mjadala kuhusu Mke asiye wa Ndoa na Mtoto wa nje ya Ndoa kwenye urithi

Watu wanadharau sana kuhusu swala la kuandika Wosia kiufupi kama umeshaona una watoto wako nje ya ndoa na uliogopa kuwaleta kwa mke wako kuwatambulisha basi andika wosia kwa mwanasheria ugawe mali kwa haki na uhifadhi hizo document au, kama ushamzalisha huko na uwezo unao nunue eneo mjengee kabsaa eneo kwa jina lake na unaandika na wosia kabsaaa, pindi ukifa huyu wa nje hasumbui wa ndani wala wa ndani hawamsumbi wa nje mana wosia umeeleza kila kitu ila jitahidi sana utende haki juu ya wosia huo au jinsi utakavyogawa hizo mali.

Kama muulizaji swali ni Muislam na mali zikigawiwa kiislam hutakiwi kurithi hata kijiko cha chai, urithi wako ni kwa mama yako tu, labda huyo baba tangu akiwa hai akupe baadhi ya mali zake akiwa yuko hai, hiyo inahesabika amekugaia lakin akifa tu, sahau kurithi kitu, labda ndugu zako wa ndani ya ndoa warithi kwanza wao halafu wakugaie kidogo ila usiite ni kama umegaiwa yani sadaka.
this is too bad..............
well may be ni njia ya kuwafanya watu wasizae nje kwan watoto watabaguliwa sana.
niliwah kusoma kwenye novel moja eti mtoto wa nje anaitwa bastard i was like what????????
 
Ninaongea kwa msimamo wa dini ya Kiislamu, kwa upande huu mtoto wa nje ya ndoa hawezi kurithi. Na hakubaliki kwa familia hata kama atatambulishwa.
Hizo dini zilizokuja na majahazi tabu tupu,unazaa alafu unasema haramu,hata aliyekuumba akikusikia atakutia laana
 
Kaka ulifanya mistake ukawa na mtoto wa nje ya ndoa , basi ujue katika sheria ya kiislam sio mrithi , nadhani mpaka pale utakapoacha wosia, wosia wa marehemu kwenye dini umepewa kipaumbele zaidi...

Anyways i have to confirm this kwa mwalimu wangu ila nadhani anarithi kama kutakuwa na wosia tu!
 
this is too bad..............
well may be ni njia ya kuwafanya watu wasizae nje kwan watoto watabaguliwa sana.
niliwah kusoma kwenye novel moja eti mtoto wa nje anaitwa bastard i was like what????????

ndo hivo tena...

bas·tard
ˈbastərd/
noun
noun: bastard; plural noun: bastards
  1. 1.
    a person born of parents not married to each other.
    synonyms: illegitimate child, child born out of wedlock;
    datedlove child, by-blow;
    natural child/son/daughter
    "he had fathered a bastard"
  2. 2.
    an unpleasant or despicable person.
    "he lied to me, the bastard!"
    synonyms: scoundrel, villain, rogue, rascal, weasel, snake, snake in the grass, miscreant, good-for-nothing, reprobate;
    informallowlife, creep, nogoodnik, scamp, scalawag, jerk, beast, rat, ratfink, louse, swine, dog, skunk, heel;
    slimeball, son of a bitch, SOB, scumbag, scumbucket, scuzzball, scuzzbag, dirtbag, sleazeball, sleazebag;
    datedhound, cad;
    archaicblackguard, knave, varlet, whoreson
    "he's a real bastard"
    • a person of a specified kind.
      "the poor bastard"
    • a difficult or awkward thing, undertaking, or situation.
      "it's been an absolute bastard of a week"
 
Du sijakuelewa,wewe ni mwanasheria au hayo ni mawazo yako!kama ni mwanasheria taja vifungu ,nashindwa kuelewa mbona wengine wanataja sheria ya mtoto,
Embe bolibo hujanielewa wapi???
Nilichokiandika mimi ni kwamba, sheria haitambui mtoto wa nje. Lakini kuna ukoo wa makabila fulani wanaamua kuwaingiza watoto wa nje wa ndoa kwenye mirathi ya marehemu mzazi wao kwa sababu tu kwa mila na taratibu za kiukoo watoto wa nje wanatambulika kifamilia. sasa hapo ndipo mkanganyiko unapotokea na ndio maana nikaandika ushauri kwa wakinababa ambao wameshachepuka na kuzaa nje wajiandae kuwaandikia watoto wao wosia. hio itasaidia sana kuondoa majanga kwenye mali.
 
Kwa wakristo na sheria za kimila wanaruhusiwa kurithi kama wosia ukiachwa ila kwa waislamu sahau!!
 
Watu wanadharau sana kuhusu swala la kuandika Wosia kiufupi kama umeshaona una watoto wako nje ya ndoa na uliogopa kuwaleta kwa mke wako kuwatambulisha basi andika wosia kwa mwanasheria ugawe mali kwa haki na uhifadhi hizo document au, kama ushamzalisha huko na uwezo unao nunue eneo mjengee kabsaa eneo kwa jina lake na unaandika na wosia kabsaaa, pindi ukifa huyu wa nje hasumbui wa ndani wala wa ndani hawamsumbi wa nje mana wosia umeeleza kila kitu ila jitahidi sana utende haki juu ya wosia huo au jinsi utakavyogawa hizo mali.

Kama muulizaji swali ni Muislam na mali zikigawiwa kiislam hutakiwi kurithi hata kijiko cha chai, urithi wako ni kwa mama yako tu, labda huyo baba tangu akiwa hai akupe baadhi ya mali zake akiwa yuko hai, hiyo inahesabika amekugaia lakin akifa tu, sahau kurithi kitu, labda ndugu zako wa ndani ya ndoa warithi kwanza wao halafu wakugaie kidogo ila usiite ni kama umegaiwa yani sadaka.
Katika uislam mtoto wa nje ya ndoa hawezi kurithi... kwahyo ukimuandika kwenye wosia kama unavyosema kweli atapata ila kama mtu mwingine kwenye ile 1/3....

Asa hapo usipoacha wosia ndo nitolee
 
W
Mtoto wa nje ya ndoa sheria inamtambua kama mrithi wa mali ya baba yake endapo baba atamtambulisha kwa mke mkubwa na atatoa faini ya mtoto huyo na kukabidhiwa mtoto huyo na kuishi nae nyumbani.

Hivyo katika mgawo wa mali lazima atapewa sehemu ya mali ya baba yake kama mtoto halali.
Wewe mlaumu Baba yako kwa kutoacha wosia
 
Kuna mengi ya kujifunza kuhusu hili na JF ina member wenye ujuzi mbali mbali sasa kama member ana point za kisheria muacheni atoe somo kwa wote na si kukashifiana, muda mwingine kupitia JF tunajifunza mambo mengi especially linapokuja swala la specialist.
 
Mtoto wa nje ana haki ya kurithi kabisa..... kifungu cha 10 cha sheria ya mtoto ya mwaka 2009 kinaelezea vizuri kabisa. .
Kuna watu wamekuwa wakichanganya kifungu hicho cha 10 kwa kuhisi ni mtu chini ya miaka 18 tu ... lakini haki ya mtu ya kurithi uliyokuwa nayo kama mtoto haiwezi ikapotea kwa vile umekuwa mtu mzima...

Hivyo basi kutokana na sheria ya mtoto na katiba yetu ambayo inapinga kabisa mtu kuwa discriminated mtoto wa nje ana haki ya kurithi...
 
Ahsante Ndugu
 
Watoto nje ya ndoa wamekuwa ni doa ktk jamii na hata upande wa dini zote. Lakini ni kati ya watu wenye bahati kubwa. Japo wenyewe wengi wanajiona hawana bahati hiyo. Wakumbuke kuzaliwa ni bahati, hata kama mama alibakwa, kumbe ndio njia iliowafikisha hapa duniani. Washukuru, wengi hawakuipata.
 
Mtoto wa nje ana haki ya kurithi kabisa..... kifungu cha 10 cha sheria ya mtoto ya mwaka 2009 kinaelezea vizuri kabisa. .
Kuna watu wamekuwa wakichanganya kifungu hicho cha 10 kwa kuhisi ni mtu chini ya miaka 18 tu ... lakini haki ya mtu ya kurithi uliyokuwa nayo kama mtoto haiwezi ikapotea kwa vile umekuwa mtu mzima...

Hivyo basi kutokana na sheria ya mtoto na katiba yetu ambayo inapinga kabisa mtu kuwa discriminated mtoto wa nje ana haki ya kurithi...
Hicho kifungu,ndio nilikuwa nataka kiwekwe hapa,niliwahi kuskia,kwa mali ya baba tutapewa tu,baba alikuwa na baadhi ya mali,kabla hata hajamuoa huyo mama yetu mdogo,wala hawajazaa hao watoto wao wawili,du huyu mama hajuwi mali sikitu,katutenganisha na wadogo zetu,hatufiki kwetu hatujuani la heri wala shari,kwa uroho wake wa mali,ndg zangu wa JF wasio jua mzazi wako akifariki usimtenge ndg yako wa damu,unamuumiza sana,kuliko unavyofikiri,mwenye mali aliyepata tabu kutafuta amekufa ameacha,je anarizka huko alipo kwa tamaa yenu ya kuwanyima watoto wake jasho lake?hawezi kuunga mkono,marehemu baba yetu alisema kabla hajakata kauli,kuna shamba gawaneni kila,mmoja heka tatu,ndio sababu tumekimbilia mahakamani,tena mahaka kuu,du wasio juwa hawatofika mahakamani,watapigwa changa la,macho,tunamshukuru magufuli amesisitiza kesi ziende haraka,tunasubiri,mungu yupo baba alisema tupewe bahati mbaya,hakuacha wosia,baba pumzika kwa amani tutapewa haki yetu,kwa kuwa uligawa kabla hujafariki
 
mtoto wa nje ya ndoa, si mtoto halali kisheria, ila anaweza kuwa mtoto halali hadi pale atakapokuwa amehalalishwa. kuhalalishwa kwa mtoto wa kambo kuna njia nyingi, kila kabila lina desturi zake, cha muhimu ahalalishwe kwa minajiri ya kabila na desturi zinazokubalika na watu wa aina yake na anakuwa mtoto halali kabisa kuweza kurithi mali ya baba yake hata kama hakai na baba yake. sio lazima akae na baba yake, cha msingi ni kuhalalishwa.

kuna desturi zingine, kama ya kabila langu, kuhalalisha mtoto ni kwenda kwa wazazi wa mama wa mtoto, kulipa fungu utakalotajiwa na hao wazee na unakuwa umemkomboa mtoto huyo. pia kama umeoa mambo haya yatatakiwa kuwa wazi na mkeo na ndugu zako wajue ili kumkaribisha ndugu mpya kwenye ukoo halali. hata hivyo, kuhalalishwa huku ni kwa wakristo na wapagani tu, katika uislam mtoto wa kambo si mtoto halali, hata ukimkomboa hataweza kurithi mali ya baba yake (ila anaweza kurithi mali ya mama kwani anatambulika kama mtoto wa mama yake tu na si mtoto wa baba), hata hivyo hata kama si mtoto halali (ni mtoto haram) anaweza kurithi mali ya baba yake muislam kama mtu baki tu akiwa amewekwa kwenye wosia wa ile 1/3, na atawekwa kwenye wosia kama mtu baki na si mtoto halali. ile 2/3 inayobaki itagawanywa kwa minajiri ya quran na yeye hatapata kitu kule kabisa kwasababu hatambuliki.

hii ni kwasababu, sharia ya kiislam inaruhusu mtu baki asiye mrithi kupewa mali kwenye wosia na mwosia hatakiwi kuzidi 1/3. zaidi ya hapo, kwa waislam, mtoto huyo au mtu yeyote ambaye si muislam hawezi kurithi mali ya muislam, hata kama una mtoto wa kambo unataka kumpa mali kwenye wosia (kama mtu baki tu kwani hatambuliki kama ni mtoto halali), utampa tu yule aliye muislam, mtu asiye muislam hawezi kurithi mali ya muislam. bofya hapa www.sheriakwakiswahili.blogspot.com
Mkuu vp kwa watoto ambao mkeo amekukuta unao na unaishi nao,ama wale ambao mkeo alikuta umezaa na mkakubaliana kuwachukua na mkawachukua hata kabla hamjachuma chochote na Mali zenu mmechuma mkiwa nao pamoja
 
Jibu rahisi ni Hivi, Mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kurithi kwenye mirathi ya babake au mamake. huo ndio ukweli wenyewe. vitabu vya sheria vipo na vinasema hivyo hivyo.
Lakini pamoja na hayo kuna Familia ambazo zinajumuisha watoto wa nje ya ndoa kwenye Mirathi ya marehemu kwa kigezo cha kwamba ni watoto wanao tambulika kifamilia na ukoo, Matokeo yake inapofika kwenye mgao wa mali nao wanapewa chao.
Ushauri wangu kwa wakina baba ambao wamshachepuka na kuzaa nje, ni heri wakae na hao watoto na kufanya tathmini ya maisha yao, kisha waandike wosia kwa ajili yao. Hii itasaidia sana kuondoa migongano, usumbufu, lawama kwa marehemu, matukio ya kudhulumiwa na ndugu au watoto wa kambo, au mama wa kambo nk. bila ya kufanya hivyo itakuwa shida kwasababu sheria tayari haitambui watoto wa nje ya ndoa.
Mi nna watoto ambao make wng alinikuta nao ma sasa tunaishi wote hapa pamekaaje
 
Mi nna watoto ambao make wng alinikuta nao ma sasa tunaishi wote hapa pamekaaje
hao watoto uliowazaa na kuishi nao, mama yao ulifunga naye ndoa au mlikuwa kwenye uhusiano wa kawaida halafu mkaachana? kama jibu ni kwamba hao watoto, mama yao mlikuwa kwenye ndoa halafu mkatengana basi sheria inawatambua hao watoto ni halali na kwenye mirathi watapewa chao.
lakini kama hao watoto uliwazaa na mama yao bila ya ndoa basi ujue kwenye kesi ya mirathi hawana chao, kwasababu sheria haitawatambua kama watoto halali.
cha msingi hapo ni kukaa na kuandika wosia kwa hao watoto ili sheria iweze kuwatambua hao watoto kwenye mgao wa mali. ukiweza kufanya hivyo utakuwa umelinda heshima ya familia yako
 
Asante mkuu maana sijafa tayari kimeanza kunuka wanaambiwa nyumba nlojenga haiwahusu na inatakiwa iuzwe ili wife atambae na chake ama nitoke na wanangu nimuachie nyumba na mtoto nlozaa nae
 
Back
Top Bottom