kinachogawanywa kwenye mirathi sio mali ya pamoja, ni mali ya mtu binafsi tu, only that potion you own. kama mama na baba walichuma mali, mali tunayoongelea watoto kurithi hapa ni kile kipande pekee anachomiliki mama huyo kwenye ile kuu wanayomiliki na baba. maadam mali hiyo imethibitishwa kisheria kwamba mama ni mmiliki (ni mali ya mama), mtoto anaweza kumiliki. hata kama mama alikuwa anamtegemea mume wake, mume akafariki katika mirathi mama akapata potion kama urithi toka kwa marehemu mume wake, fungu lile ndilo watoto wake wa kambo wataweza kurithi siku akifariki. ukizunguluka wee utakuja jibu linakuja moja tu kwamba, mali ambayo kisheria mama anamiliki ndiyo mtoto wake anaweza kurithi siku akifa.
labda utuambie hapa sisi ambao sio wataalam wa sheria za kiislam. baba na mama wamechuma mali pamoja, wamezaa watoto lakini kwenye familia kuna mtoto wa kambo wa mama na wote ni waislam. siku moja mama na baba wanaendesha kwenda moshi, wakapata ajali wakafariki wote wawili. wamebaki watoto tu, watoto wa kiislam wa kwenye ndoa na mtoto muislam ambaye mama alimzaa nje ya ndoa. ....hapo itakuwaje?
au mama na baba hao waliopata ajali na kufariki kuacha watoto wa aina hizo mbili nyumbani, mama alikuwa mke wa nyumbani tu (mama wa nyumbani) mume wake ndiye alikuwa mtafutaji. je? kuna asilimia fulani walau hata kama sio 50% kwa 50% ambayo mama yule wa nyumbani atakuwa alikuwa anastahili? na je, mirathi ile itafunguliwa mmoja mmoja au utawaunganisha pamoja na kufanya mirathi ya watu wa wili pamoja....na je, mama hapo atakuwa alikuwa na haki yeyote ya kumiliki mali alizokuwa anachuma mume wake? kama ndio ni kwanini na kama sio ni kwanini?
na je, mtoto yule wa kambo, atakuwa na haki ya kumiliki mali za mamake tu (kama zipo), katika mazingira kama haya, mama mali zake zitatoka wapi ili mtoto apewe haki ya kurithi kwa mamake?
hiyo ni homework, ukijibu maswali haya utafungua wengi humu. thanks.