Mjadala kuhusu Mke asiye wa Ndoa na Mtoto wa nje ya Ndoa kwenye urithi

Mjadala kuhusu Mke asiye wa Ndoa na Mtoto wa nje ya Ndoa kwenye urithi

mtoto wa nje ya ndoa, si mtoto halali kisheria, ila anaweza kuwa mtoto halali hadi pale atakapokuwa amehalalishwa. kuhalalishwa kwa mtoto wa kambo kuna njia nyingi, kila kabila lina desturi zake, cha muhimu ahalalishwe kwa minajiri ya kabila na desturi zinazokubalika na watu wa aina yake na anakuwa mtoto halali kabisa kuweza kurithi mali ya baba yake hata kama hakai na baba yake. sio lazima akae na baba yake, cha msingi ni kuhalalishwa.

kuna desturi zingine, kama ya kabila langu, kuhalalisha mtoto ni kwenda kwa wazazi wa mama wa mtoto, kulipa fungu utakalotajiwa na hao wazee na unakuwa umemkomboa mtoto huyo. pia kama umeoa mambo haya yatatakiwa kuwa wazi na mkeo na ndugu zako wajue ili kumkaribisha ndugu mpya kwenye ukoo halali. hata hivyo, kuhalalishwa huku ni kwa wakristo na wapagani tu, katika uislam mtoto wa kambo si mtoto halali, hata ukimkomboa hataweza kurithi mali ya baba yake (ila anaweza kurithi mali ya mama kwani anatambulika kama mtoto wa mama yake tu na si mtoto wa baba), hata hivyo hata kama si mtoto halali (ni mtoto haram) anaweza kurithi mali ya baba yake muislam kama mtu baki tu akiwa amewekwa kwenye wosia wa ile 1/3, na atawekwa kwenye wosia kama mtu baki na si mtoto halali. ile 2/3 inayobaki itagawanywa kwa minajiri ya quran na yeye hatapata kitu kule kabisa kwasababu hatambuliki.

hii ni kwasababu, sharia ya kiislam inaruhusu mtu baki asiye mrithi kupewa mali kwenye wosia na mwosia hatakiwi kuzidi 1/3. zaidi ya hapo, kwa waislam, mtoto huyo au mtu yeyote ambaye si muislam hawezi kurithi mali ya muislam, hata kama una mtoto wa kambo unataka kumpa mali kwenye wosia (kama mtu baki tu kwani hatambuliki kama ni mtoto halali), utampa tu yule aliye muislam, mtu asiye muislam hawezi kurithi mali ya muislam. bofya hapa www.sheriakwakiswahili.blogspot.com
Inakuaje na kwa mtoto wa nje ya ndoa ambaye alibadili dini na kuwa muislamu akaolewa afu baada ya baba yake kufa akaja kudai mirathi kwa baba mkristo. Hii imekaaje kisheria.
 
Kuwa mtoto wa nje ya ndoa,ni jambo baya sana,nilikuwa sijuwi,baba alipofariki,ndio nilijuwa,ningekuwa na uwezo ningemuomba mwenyezi mungu,anipe japo dakika kumi,niongee na baba,baba alipofariki mimi na mwenzangu tulinyanyaswa sana,wakati baba anaumwa alijitahidi akatoa wosia,alisema kuna shamba gawaneni heka 3,kila mmoja,tupo4pamoja na wadogo zetu2wenzetu wamezaliwa ndani ya ndoa,baada ya baba kufariki yule mama alisema baba hakuacha shamba,ajabu wakati baba anahangaika kutaja shamba mkewe alikuwepo,alimshika kifuani akasema :kumwambia baba sawa tumesikia,hakuweza kuendelea kusema tena,mpaka anafariki,acha hilo,baada ya mazishi alisema yeye anataka mirathi ya kiislam,lengo ni sisi tusiwe kwenye mgao,bali atatupa,kitu gani ?hasemi,mimi kwa upande wangu nimelelewa na baba kwa muda mrefu,huyo mama nilitambulishwa kwake baba alipotaka kumuoa,akaja tukakaa wote,na mwenzangu pia anatambulika cha ajabu,anataka atupe yeye mirathi,kadri atakavyotaka ,ajabu,vitu vya baba tena vingine amevikuta,hiyo ni ngumu,kuikubali,mbio kali sana mahakama kuu ya tanzania,yenyewe ndio itaamuwa ,tumefika tumepokelewa,shauri linaendelea,imekula kwake kwa tamaa yake,tunamshukuru mungu,baba amefariki tuna akili zetu,si pati picha kama tungekuwa wadogo,tungeishia maisha mabaya yeye anakula kuku na wanawe
 
Blablaaaaaa blaaaa nyingi sana, umesoma sheria ya ndoa ya 1971 na Sheria ya Mtoto (The Law of the Child Act)?
mkuu, ili wee usionekane mbumbumbu, weka kifungu cha sheria watoto inayoongea yale unayoyaamini, utajibiwa kwa hoja pia, usije kwa mbwembwe zisizo na point of law. leta hoja ya sheria, argue kama kweli unajua, na mimi nita argue back.
 
wewe umekuja na hoja zipi za kisheria au sharia ?
 
Inakuaje na kwa mtoto wa nje ya ndoa ambaye alibadili dini na kuwa muislamu akaolewa afu baada ya baba yake kufa akaja kudai mirathi kwa baba mkristo. Hii imekaaje kisheria.
watu wapende wasipende, mnachotakiwa kujua ni kwamba, kama mirathi ya muislam yeyote itagawanywa kiislam, mtu asiye muislam hatakiwi kuwa mrithi, pia mtoto wa kambo si mtoto halali na hatakiwi kurithi. labda mirathi igawanywe kwa sheria za kiserikali au kimila ndio mtoto wa kambo anaweza kuhalalishwa na kuwa mtoto halali, kiislam hata ukihalalisha mtoto wa kambo bado tu ni haramu.
 
dini ya kisengerema mnoooo
 
wewe umekuja na hoja zipi za kisheria au sharia ?
hoja iliyopo ni kwamba, ugawaji mirathi upo wa aina tatu, na mirathi hugawanywa kwa kufuata matakwa ya marehemu aliyoyaacha kwenye wosia au kwa kuangalia mwenendo wa maisha yake kabla hajafa. ukifikia hapo unaweza kugawa mirathi kwa kiislam (kuzingatia quran), kwa kiserikali (wakristo) na kimila (watu wasio waislam na sio wakristo wanaofuata mila na desturi). kila mlengo wa ugawaji mirathi nilioutaja hapa juu una misingi yake. kwa mfano, ukigawa mirathi kwa kutumia mlengo wa kiislam, utaratibu wote upo ndani ya quran na hautakiwi kupindisha. kwenye quran mtoto wa kambo ni mtoto haram, hatakiwi kurithi mali ya baba ila atarithi mali ya mama yake. mtu asiye muislam hatarithi mali ya asiye muislam hata kama ni mtoto wake halali.

pia, tukisema mtoto wa kambo kurithi, akili yako inakuja kufikiri kwamba hapa tunaongelea under age tu ndio maana umetamka sheria ya watoto. hapa hata waliozidi miaka 18 tumeweka lugha kwamba ni watoto wa marehemu, hata wewe ni mtoto wa baba yako, hivyo usifikiri hapa tunaongelea kugawa mirathi ya wazazi kwa underage tu, hapa ni kwa wote watoto kwa wakubwa. kinachozingatiwa ni kwamba, yule aliye mrithi tu kisheria ndiye anayeweza kurithi, asiye mrithi hawezi kurithi. sasa, kuna mambo mengi tunaweza kuongea apa, la kwanza ni mirathi, la pili ni mtoto wa kambo kulingana na sheria including sheria ya watoto namba 21 ya mwaka 2009, kuna sheria ya ndoa etc, wewe kitu gani unachobisha ili nikujibu specifically? tafadhali!
 
dini ya kisengerema mnoooo
sheria za nchi zinaitambua hiyo unayoitukana, halafu, nimpoteza muda kujibizana na wewe, kumbe una maneno machafu. i doubt nisijekuwa naongea na mtoto mdogo. unatakiwa kujifunza kuvumiliana na imani za wengine, na kama hautajifunza ujue siku hizi hayo unayoyatype kama yakileta madhara unaweza kukamatwa na kushitakiwa....hujui sheria ya cyber ilishapitishwa mzee.....
 
nimetukana wapi?
 
ni
hoja iliyopo ni kwamba, ugawaji mirathi upo wa aina tatu, na mirathi hugawanywa kwa kufuata matakwa ya marehemu aliyoyaacha kwenye wosia au kwa kuangalia mwenendo wa maisha yake kabla hajafa. ukifikia hapo unaweza kugawa mirathi kwa kiislam (kuzingatia quran), kwa kiserikali (wakristo) na kimila (watu wasio waislam na sio wakristo wanaofuata mila na desturi). kila mlengo wa ugawaji mirathi nilioutaja hapa juu una misingi yake. kwa mfano, ukigawa mirathi kwa kutumia mlengo wa kiislam, utaratibu wote upo ndani ya quran na hautakiwi kupindisha. kwenye quran mtoto wa kambo ni mtoto haram, hatakiwi kurithi mali ya baba ila atarithi mali ya mama yake. mtu asiye muislam hatarithi mali ya asiye muislam hata kama ni mtoto wake halali.

pia, tukisema mtoto wa kambo kurithi, akili yako inakuja kufikiri kwamba hapa tunaongelea under age tu ndio maana umetamka sheria ya watoto. hapa hata waliozidi miaka 18 tumeweka lugha kwamba ni watoto wa marehemu, hata wewe ni mtoto wa baba yako, hivyo usifikiri hapa tunaongelea kugawa mirathi ya wazazi kwa underage tu, hapa ni kwa wote watoto kwa wakubwa. kinachozingatiwa ni kwamba, yule aliye mrithi tu kisheria ndiye anayeweza kurithi, asiye mrithi hawezi kurithi. sasa, kuna mambo mengi tunaweza kuongea apa, la kwanza ni mirathi, la pili ni mtoto wa kambo kulingana na sheria including sheria ya watoto namba 21 ya mwaka 2009, kuna sheria ya ndoa etc, wewe kitu gani unachobisha ili nikujibu specifically? tafadhali!
likuwa nahitaji hiki ulichokuja nacho, ahsante sana.

swali, inakuwaje pale kama mzazi atafariki testate na ndani ya Will kamueka mtoto aliye mzaa nje ya ndoa?
 
Sheria ya dini ya kiislamu MTOTO huyo hana URITHI lakin ameruhusiwa baba kabla ajafa awe amemuandalia mazingira mapema......HII NI KWASABABU ZINAA NI HARAMU LAKINI KWAKUA MTOTO HANA HATIA AMEONEWA HURUMA KIDOGO.
 
Jibu rahisi ni Hivi, Mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kurithi kwenye mirathi ya babake au mamake. huo ndio ukweli wenyewe. vitabu vya sheria vipo na vinasema hivyo hivyo.
Lakini pamoja na hayo kuna Familia ambazo zinajumuisha watoto wa nje ya ndoa kwenye Mirathi ya marehemu kwa kigezo cha kwamba ni watoto wanao tambulika kifamilia na ukoo, Matokeo yake inapofika kwenye mgao wa mali nao wanapewa chao.
Ushauri wangu kwa wakina baba ambao wamshachepuka na kuzaa nje, ni heri wakae na hao watoto na kufanya tathmini ya maisha yao, kisha waandike wosia kwa ajili yao. Hii itasaidia sana kuondoa migongano, usumbufu, lawama kwa marehemu, matukio ya kudhulumiwa na ndugu au watoto wa kambo, au mama wa kambo nk. bila ya kufanya hivyo itakuwa shida kwasababu sheria tayari haitambui watoto wa nje ya ndoa.
 
Du sijakuelewa,wewe ni mwanasheria au hayo ni mawazo yako!kama ni mwanasheria taja vifungu ,nashindwa kuelewa mbona wengine wanataja sheria ya mtoto,
 
SURA YA 352
SHERIA YA UTHIBITISHO WA WOSIA NA USIMAMIZI WA MIRATHI

14. JE WATOTO WA NJE YA NDOA WANARITHI?

Mahakama ya Rufaa katika kesi namaba 72 katika ripoti ya sheria ya mwaka 1990 kati ya VIOLET ISHENGOMA dhidi ya KABIDHI WASII MKUU NA MWENZAKE imetoa tafsiri ya mtoto katika sheria ya ndoa kwamba haihusishi mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hivyo,watoto hao hawatambuliwi chini ya sheria ya ndoa kama watoto.
Watoto walizaliwa nje ya ndoa hawaruhusiwi kurithi,wanaweza kurithi tu kama wamehalalishwa kwa kufuata desturi au taratibu zinazojulikana na kutambulika katika jamii hiyo.
Vilevile inashauriwa kwamba ni muhimu kuandika wosia ambao katika kugawa mali utamjumuisha mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa.Hii itasaidia kuondoamateso yanayowapata watoto walizaliwa nje ya ndoa.
mie pia naona hii sheria imeamua kumhukumu huyu mtoto kama ambavyo jamii tayari imeshamhukumu
hivi kwan mtoto hapa anakosa gani yeye?
sheria je inatueleza vipi kuhusu haki za lazima na za msingi za mtoto huyu kama vile kuheshiwa, kupendwa na kutunzwa?
kwaann sheria ione mtoto aliyezaliwa kwenye ndoa ndo mwenye haki zaid, kuliko huyu ilihali wote wamezaliwa na baba mmoja? tena huyu wa ndani ya ndoa anapewa ahueni mara mbili kwamba wazazi wote wawili wanamlea katika mapenzi mema lkin huyu wa nje ni mhanga wa maisha yasiyo rasmi, kukataliwa, kubaguliwa na mwisho wa siku ananyimwa hata haki.

what i know hapa dunian tutawabagua sana lkn mbele za Mungu sote tutasimama kila mmoja kwa nafasi yake ambako hakuna upendeleo.

thank God hakunaga maduka, nyumba wala magari yaliyo maalum kwaajili ya wa waotot wa ndani ya ndoa tu
 
Watu wanadharau sana kuhusu swala la kuandika Wosia kiufupi kama umeshaona una watoto wako nje ya ndoa na uliogopa kuwaleta kwa mke wako kuwatambulisha basi andika wosia kwa mwanasheria ugawe mali kwa haki na uhifadhi hizo document au, kama ushamzalisha huko na uwezo unao nunue eneo mjengee kabsaa eneo kwa jina lake na unaandika na wosia kabsaaa, pindi ukifa huyu wa nje hasumbui wa ndani wala wa ndani hawamsumbi wa nje mana wosia umeeleza kila kitu ila jitahidi sana utende haki juu ya wosia huo au jinsi utakavyogawa hizo mali.

Kama muulizaji swali ni Muislam na mali zikigawiwa kiislam hutakiwi kurithi hata kijiko cha chai, urithi wako ni kwa mama yako tu, labda huyo baba tangu akiwa hai akupe baadhi ya mali zake akiwa yuko hai, hiyo inahesabika amekugaia lakin akifa tu, sahau kurithi kitu, labda ndugu zako wa ndani ya ndoa warithi kwanza wao halafu wakugaie kidogo ila usiite ni kama umegaiwa yani sadaka.
 
Back
Top Bottom