mtoto wa nje ya ndoa, si mtoto halali kisheria, ila anaweza kuwa mtoto halali hadi pale atakapokuwa amehalalishwa. kuhalalishwa kwa mtoto wa kambo kuna njia nyingi, kila kabila lina desturi zake, cha muhimu ahalalishwe kwa minajiri ya kabila na desturi zinazokubalika na watu wa aina yake na anakuwa mtoto halali kabisa kuweza kurithi mali ya baba yake hata kama hakai na baba yake. sio lazima akae na baba yake, cha msingi ni kuhalalishwa.
kuna desturi zingine, kama ya kabila langu, kuhalalisha mtoto ni kwenda kwa wazazi wa mama wa mtoto, kulipa fungu utakalotajiwa na hao wazee na unakuwa umemkomboa mtoto huyo. pia kama umeoa mambo haya yatatakiwa kuwa wazi na mkeo na ndugu zako wajue ili kumkaribisha ndugu mpya kwenye ukoo halali. hata hivyo, kuhalalishwa huku ni kwa wakristo na wapagani tu, katika uislam mtoto wa kambo si mtoto halali, hata ukimkomboa hataweza kurithi mali ya baba yake (ila anaweza kurithi mali ya mama kwani anatambulika kama mtoto wa mama yake tu na si mtoto wa baba), hata hivyo hata kama si mtoto halali (ni mtoto haram) anaweza kurithi mali ya baba yake muislam kama mtu baki tu akiwa amewekwa kwenye wosia wa ile 1/3, na atawekwa kwenye wosia kama mtu baki na si mtoto halali. ile 2/3 inayobaki itagawanywa kwa minajiri ya quran na yeye hatapata kitu kule kabisa kwasababu hatambuliki.
hii ni kwasababu, sharia ya kiislam inaruhusu mtu baki asiye mrithi kupewa mali kwenye wosia na mwosia hatakiwi kuzidi 1/3. zaidi ya hapo, kwa waislam, mtoto huyo au mtu yeyote ambaye si muislam hawezi kurithi mali ya muislam, hata kama una mtoto wa kambo unataka kumpa mali kwenye wosia (kama mtu baki tu kwani hatambuliki kama ni mtoto halali), utampa tu yule aliye muislam, mtu asiye muislam hawezi kurithi mali ya muislam. bofya hapa
www.sheriakwakiswahili.blogspot.com