Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mwanamke anahitaji mwanaume mbabe, mshenzi asiye na huruma

Ukijifanya Mr.love umekwenda na maji.

Usiwajali watoto kuliko kujijali wewe MWENYEWE. Hawatakusaidia lolote.

Jifunze kuwa Mwanaume ndipo uoe.

Usiendeshwe na maneno ya Mwanamke.

Akikuzingua mara moja tambaa naye mara elfu mpaka Ajue amekosea njia.

Timua
Usipotimua utatimuliwa.

Mtu ni mwanaume bado mwanamke akusumbue huo ni upumbavu
 
Unajua vijana mnadanganyana sana. Saiz unaona kama unajimudu kuwa peke yako kwamba kila kitu unaweza kufanya lakin amin mwanaume bila mwanamke hajakamilika kuna mda unakuja wew mwenyewe bila kulazimishwa utao.
.
Sasa bas omba sana uo wakati unavyokuja uwe umempata mtu sahii la sivyo hayo majuto unayoona walioa wanajututia ndio yatayokukuta wewe...
 
Unajua vijana mnadanganyana sana. Saiz unaona kama unajimudu kuwa peke yako kwamba kila kitu unaweza kufanya lakin amin mwanaume bila mwanamke hajakamilika kuna mda unakuja wew mwenyewe bila kulazimishwa utao.
.
Sasa bas omba sana uo wakati unavyokuja uwe umempata mtu sahii la sivyo hayo majuto unayoona walioa wanajututia ndio yatayokukuta wewe...
Kuoa muhimu ila kama unakimbia nyumba sababu ya mke bora ukae mwenyewe
 
Sisi tunaoa na tunakula raha kama kawaida.

Msikurupukie kuoa, mtaoa majini yatawafyonza damu, shauri yenu.
Ujinga wa mateso huja tu hata miaka 100 mbele.

Kuna demu nimemla kumbe ni mke wa mtu na ndoa ina miaka 10.

Baada ya kugundua ndio nikamuhoji kwanini hakuniambia ye ni mke wa mtu?
Ye anasema "tokea niolewe ndio wewe mchepuko wangu wa kwanza"

Alinikwaza sanaa, maana ilibidi aniweke wazi ili Mimi mwenyewe ndio niamue kama naweza kutembea na mke wa mtu ila sio kunificha.

Japo nimekata mawasiliano baada ya kugundua, ila roho ili niuma kiasi.

Kutembea na mke wa mtu hiyo kwangu ni DHAMBI KUBWA SANAA.

Back to the point.

Huyu ukute miaka yotee 9 alikua anajisifia kaoa mke Bora ila mwaka wa 10 mke wake kachepuka..

What if angetufumania?

#YNWA
 
Si niliwaambia msioe?

Mcheki huyu mwamba ndoa inavyomuua.

Hii imetokea kazini,
Huyu jamaa kanihuzunisha sanaaa...

Mkurugenzi kaunda team ya watu 4 kumsaidia Kazi fulani hivi huko field.
Katoa na gari.

Katika hiyo timu tupo wa4 + dereva jumla wa5.

Kati yetu aliyeoa ni mmoja tu na kwakuwa kaenda age kidogo kuliko sisi then tuliamua kumpa ukuu wa msafara.

Sasa bana Kazi yenyewe tuliyopewa ilianza 20/12/2021.

Tulipiga Kazi na kuelewana 23/12 turudi makwetu kimyakimya tukale sikukuu na atakayepigiwa simu ajibu tupo kazini/field.

Ila huyu jamaa aliyeoa alikataa "Lazima tupige kazi mpaka sikukuu (X-Mass), tuheshimu Kazi za watu hizi jamani"

Aisee wotee tulimshangaa "Braza halmashauri ya baba ako?"

Baada ya mzozo mrefu sisi ndio tulishinda.

Tukasepa 23 na kurudi field 27/12.

Hali hiyohiyo ikajitokeza mwaka mpya.

Aligoma kurudi makwetu tarehe 29 ili tukale sikukuu.

Na kuonyesha yupo serious alipiga simu ofisini kuwa tunataka kumfelisha mkurugenzi.

Sasa bana Hawa raia wengine walimkasirikia balaaa.

Kwenye mapumziko ya usiku wa 29/12 Mimi ilinibidi nimpeleke bar fulani hivi chemba na kumuuliza "Braza unataka kutufanyisha Kazi mwaka mpya kwani halmashauri ya baba ako?"

Aisee baada ya bia kukolea mwamba aliamua kufunguka hasaa.

Alisema...

Kazini watu humuona yeye mchapakazi Bora, wanamuona sio mtoro kazini, wanamuona akipiga Kazi mpaka sikukuu, wanamuona ni mpiga Kazi mpaka usiku (huyu mwamba siku nyingine hutoka kazini saa 4 usiku).
Basi raia wanamsifiaaa kwamba ni mchapakazi, kumbe mwamba huwa ANAKIMBIA MAKELELE YA MKEWE NYUMBANI ...!!!

Anasema Ndoa yake ni ngumu sanaa na kinacholeta ugumu ni mdomo wa mkewe.

Mkewe ni mbogo hasa, ukimchokonyoa tu ni kama shimo la siafu, ni full kutapika neno lolote alionalo kwake linamfaa..!!!

Hali hii imemfanya jamaa kukimbia nyumbani na hali hii imemfanya apaone kwake ni jehanamu ya amani yake...!!!

Ndio maana hata zile sikukuu kama tusipoingia kazini basi ni yeye kwenda kuishi na mkewe siku nzima ndani..!!!

Ila kwenye maongezi yake anasema, alioa 2016 na mkewe alimkuta jamaa ana maisha kiasi (gari na nyumba vilikuwepo).

Kwahiyo mkewe alikuja kwenye maisha yake akiwa na maisha tayari.

Yeye na mkewe Wana watoto Wa3.

Hawezi kumuacha kwasababu ya watoto ila pia mdomo wake umemshinda...!!!

Nilibaki kumuonea huruma tu.

Sasa mi najiuliza....

1. Yaani alioa ili aikimbie nyumba yake aliyoijenga kwa gharama?

2. Kama anarudi usiku means yeye na watoto hawaonani, Kwahiyo alioa ili Awe ANAKIMBIA watoto?

3. Sasa kama alikua tayari na maisha KWENYE NDOA ALIENDA KUTAFUTA NINI?

ILA KUNA RAIA WABISHI...

Msioe ndugu zangu MTAKUFA.

We una nyumba una gari UNAOA ILI UTAFUTE NINI?

Inakuaje mwanamke uliyemtolea Mahari akufanye ukimbie nyumba?

Ila bana mwisho wa siku kama pole nilimpa na field hatukuingia...!!

Nilimwambia aende tu kupambana na mkewe sisi ma single men tukale sikukuu na usingle wetuu..!!!

Yaani baharia...

Unamuona mwamba anakomaa na Kazi mpaka usiku KUMBE NYUMBANI PAMOTO.

Unamuona baharia aondoki mapema bar KUMBE NYUMBANI PAMOTO.

Unamuona mkulungwa kila siku akitoka job ni kuzurura KUMBE NYUMBANI PAMOTO..

MSIOE MTAKUFA.

Tuendelee kutafuta hela

"If you think money can't bring happiness then go and ask the homeless and the Jobless"

#YNWA
Bwege tu huyo
 
Back
Top Bottom