Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Kuna mwanetu akawa anatusimulia maskani kuhusu jamaa yake aliyeoa na ana 26 tu. Jamaa hakai nyumbani, pete ya ndoa inampa tabu kuivaa kwa model ya ndoa aliyonayo, kila siku anajilaumu kuoa mapema.
 
Kwani aliekuambia usipo oa ndio maisha yako yanakuwa tulivu raha na starehe kila siku ni nani.???.ww unadhani wazinifu hawauniani au hawagombani?? Ni maisha ya kawaida tu hayo. Ni mitihani ya kawaida ambayo mnaweza kukaa chini na kusolve yakaisha

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app

Kwani Kuna mzinifu..
1. Anayechelewa nyumbani kisa kuna mkorofi ndani?
2. Kuna mzinifu anayeshinda bar kisa nyumbani Kuna makelele?

Yaani HIVI KUNA MZINIFU ANAYEKIMBIA NYUMBANI?

#YNWA
 
Mada za Wanaume kulalamika kunyanyaswa na Wanawake zinazidi kuwa nyingi.
Mi sijalalamika na Wala siwezi kulalamika.

Nimeleta Uzi ikiwa tu nayashangaa maisha ya ndoa. Na sijui alioa ILI IWEJE KAMA HAYA NDIO MAISHA ANAYOISHI.

Nimemuonea tu huruma halafu HAYANIHUSU.

#YNWA
 
Hao wanaoteseka na ndoa zao ni wachache, kuna wengi wanaofurahia maisha ya ndoa.
Asimilia 90 naosikia ni malalamiko tu.
Tena Kuna wale wanaolalamikia ndani, Hawa ndio NAWAONEA HURUMA.
Maana maumivu ya ndani ni hatari sanaa.

Ila kwakuwa WALIAMUA wenyewe, waache tu wapambane.

#YNWA
 
Kusema ukweli mwanamke kuishi nae haitakiwi uwe lege lege kabisa yani unatakiwa asiwe ana kuelewa ...kuna muda uwe kauzu kuna muda uwe mpole kidogo!

Ukweli ni kwamba wanawake hawahitaji mwanaume mpole au zumbukuku lasivyo utaiona ndoa ni chungu hakika na utajuta!

Mwanaume unahama nyumba kisa mwanamke?
Aiseeee hichi ni kiwango cha mwisho kabisa cha unyonge kabisa!
Mwanamke mwenye mdomo mrefubasiye na break wewe mpige mkwara wa kumdunda au mpe makofi mawili au matatu ajue kabisa!
Mwanamke anaongea tuu ana kutusi ana chonga mdomo wewe mwanaume umesimama tuu unamuangalia?
Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mwanaume usipooa unataka uolewe? M
Anyway sijaoa na sina mpango wa kuoa hivi karibuni ila Mwanaume ni lazima uoe labda tu uwe gasho

Mwanaume hutaki kuoa kisa unaogopa kunyanyaswa na mwanamke? Ni Nini maana ya wewe kuwa mwanaume? Mwanaume unatakiwa uwe kichwa uweze kumuongoza mwanamke na siyo kupelekeshwa pelekeshwa,

Mwanamke anakukunja shati anakutikisa na wewe unatikisika? Kmmmake inatakiwa unamfanya kitu ambacho siku nyingine hatajaribu hata kunyanyua sauti yake kuizidi sauti yako, inatakiwa ajue kuwa ili nyumba iwe na amani ni yeye kuwa na heshima vinginevyo nyumba aione chungu yeye na wala siyo wewe mwanaume
 
Mwanaume usipooa unataka uolewe? M
Anyway sijaoa na sina mpango wa kuoa hivi karibuni ila Mwanaume ni lazima uoe labda tu uwe gasho
Kuwa gasho maana ake ni kusukumiwa mpini na kusukuma mpini au kusukumiwa HAKUNA UHUSIANO WOWOTEE NA NDOA.

#YNWA
 
Ujinga wa mateso huja tu hata miaka 100 mbele.

Kuna demu nimemla kumbe ni mke wa mtu na ndoa ina miaka 10.

Baada ya kugundua ndio nikamuhoji kwanini hakuniambia ye ni mke wa mtu?
Ye anasema "tokea niolewe ndio wewe mchepuko wangu wa kwanza"

Alinikwaza sanaa, maana ilibidi aniweke wazi ili Mimi mwenyewe ndio niamue kama naweza kutembea na mke wa mtu ila sio kunificha.

Japo nimekata mawasiliano baada ya kugundua, ila roho ili niuma kiasi.

Kutembea na mke wa mtu hiyo kwangu ni DHAMBI KUBWA SANAA.

Back to the point.

Huyu ukute miaka yotee 9 alikua anajisifia kaoa mke Bora ila mwaka wa 10 mke wake kachepuka..

What if angetufumania?

#YNWA
Tuko pamoja mzee. Ila huyo demu kakupanga, wewe sio mchepuko wake wa kwanza, ashatoa sana sema ndio lugha zao usimuone malaya na ujiskie hali fulani ya 'uspesho'
 
Inawezekanaje uone nabado unakula maisha mkuu,tupe mbinu zakivita nahatutaki kukurupa ,natanguliza shukrani
Kwanza kubwa zaidi lazima ujue kwanini unaoa, je kwa ajili ya kupata mbususu tupu, mwenza(ili mradi nyumbani awepo mtu), msaidizi(kukufulia, maji ya kuoga, kupigiwa pasi n.k) tulizo la nafsi na mambo kedekede.

Ukishajua unachotaka ndio starting point yenyewe hiyo. Kuoa ni jambo ambalo bila ya collabo na mungu hutoboi ng'o, kwanza yeye ndio katuambia tuoe, sasa cha kustaajabisha tunapofikia hatua ya kuoa tunajiolea tu. Kuoa ni lazima ila baada ya ulazima wa kuoa kuna muongozo(ushauri) huu hatuufati hata kidogo, mwishowe tunaangukia kwenye majini..

Jingine kubwa kabisa mzee, oa mwanamke ambae bila ww hawezi(yaani hapindui kwako), hapa mzee inabidi ukaze saana moyo, unaweza ukapenda jitu halikupendi sasa kwa usalama wa moyo wako oa mtu ambae yeye anakupenda, hata kama we humkubali kihivyo ila usalama wako, oa huyo.
 
Tuko pamoja mzee. Ila huyo demu kakupanga, wewe sio mchepuko wake wa kwanza, ashatoa sana sema ndio lugha zao usimuone malaya na ujiskie hali fulani ya 'uspesho'
Kutembea na mke wa mtu sio sifa na hakuna uspesho wowotee...

#YNWA
 
Si niliwaambia msioe?

Mcheki huyu mwamba ndoa inavyomuua.

Hii imetokea kazini,
Huyu jamaa kanihuzunisha sanaaa...

Mkurugenzi kaunda team ya watu 4 kumsaidia Kazi fulani hivi huko field.
Katoa na gari.

Katika hiyo timu tupo wa4 + dereva jumla wa5.

Kati yetu aliyeoa ni mmoja tu na kwakuwa kaenda age kidogo kuliko sisi then tuliamua kumpa ukuu wa msafara.

Sasa bana Kazi yenyewe tuliyopewa ilianza 20/12/2021.

Tulipiga Kazi na kuelewana 23/12 turudi makwetu kimyakimya tukale sikukuu na atakayepigiwa simu ajibu tupo kazini/field.

Ila huyu jamaa aliyeoa alikataa "Lazima tupige kazi mpaka sikukuu (X-Mass), tuheshimu Kazi za watu hizi jamani"

Aisee wotee tulimshangaa "Braza halmashauri ya baba ako?"

Baada ya mzozo mrefu sisi ndio tulishinda.

Tukasepa 23 na kurudi field 27/12.

Hali hiyohiyo ikajitokeza mwaka mpya.

Aligoma kurudi makwetu tarehe 29 ili tukale sikukuu.

Na kuonyesha yupo serious alipiga simu ofisini kuwa tunataka kumfelisha mkurugenzi.

Sasa bana Hawa raia wengine walimkasirikia balaaa.

Kwenye mapumziko ya usiku wa 29/12 Mimi ilinibidi nimpeleke bar fulani hivi chemba na kumuuliza "Braza unataka kutufanyisha Kazi mwaka mpya kwani halmashauri ya baba ako?"

Aisee baada ya bia kukolea mwamba aliamua kufunguka hasaa.

Alisema...

Kazini watu humuona yeye mchapakazi Bora, wanamuona sio mtoro kazini, wanamuona akipiga Kazi mpaka sikukuu, wanamuona ni mpiga Kazi mpaka usiku (huyu mwamba siku nyingine hutoka kazini saa 4 usiku).
Basi raia wanamsifiaaa kwamba ni mchapakazi, kumbe mwamba huwa ANAKIMBIA MAKELELE YA MKEWE NYUMBANI ...!!!

Anasema Ndoa yake ni ngumu sanaa na kinacholeta ugumu ni mdomo wa mkewe.

Mkewe ni mbogo hasa, ukimchokonyoa tu ni kama shimo la siafu, ni full kutapika neno lolote alionalo kwake linamfaa..!!!

Hali hii imemfanya jamaa kukimbia nyumbani na hali hii imemfanya apaone kwake ni jehanamu ya amani yake...!!!

Ndio maana hata zile sikukuu kama tusipoingia kazini basi ni yeye kwenda kuishi na mkewe siku nzima ndani..!!!

Ila kwenye maongezi yake anasema, alioa 2016 na mkewe alimkuta jamaa ana maisha kiasi (gari na nyumba vilikuwepo).

Kwahiyo mkewe alikuja kwenye maisha yake akiwa na maisha tayari.

Yeye na mkewe Wana watoto Wa3.

Hawezi kumuacha kwasababu ya watoto ila pia mdomo wake umemshinda...!!!

Nilibaki kumuonea huruma tu.

Sasa mi najiuliza....

1. Yaani alioa ili aikimbie nyumba yake aliyoijenga kwa gharama?

2. Kama anarudi usiku means yeye na watoto hawaonani, Kwahiyo alioa ili Awe ANAKIMBIA watoto?

3. Sasa kama alikua tayari na maisha KWENYE NDOA ALIENDA KUTAFUTA NINI?

ILA KUNA RAIA WABISHI...

Msioe ndugu zangu MTAKUFA.

We una nyumba una gari UNAOA ILI UTAFUTE NINI?

Inakuaje mwanamke uliyemtolea Mahari akufanye ukimbie nyumba?

Ila bana mwisho wa siku kama pole nilimpa na field hatukuingia...!!

Nilimwambia aende tu kupambana na mkewe sisi ma single men tukale sikukuu na usingle wetuu..!!!

Yaani baharia...

Unamuona mwamba anakomaa na Kazi mpaka usiku KUMBE NYUMBANI PAMOTO.

Unamuona baharia aondoki mapema bar KUMBE NYUMBANI PAMOTO.

Unamuona mkulungwa kila siku akitoka job ni kuzurura KUMBE NYUMBANI PAMOTO..

MSIOE MTAKUFA.

Tuendelee kutafuta hela

"If you think money can't bring happiness then go and ask the homeless and the Jobless"

#YNWA

Huyo Mwamba anakilia vyeo, mwambie ampandishe cheo huyo awe Bi Mkubwa. Bi Mkubwa abaki na maneno yachomayo kuliko pasi Raha akale na Bi Mdogo.

Bi Mdogo naye akizingua utaratibu ni uke Ile, ampandishe cheo. We live once oooh!
 
Huyo Mwamba anakilia vyeo, mwambie ampandishe cheo huyo awe Bi Mkubwa. Bi Mkubwa abaki na maneno yachomayo kuliko pasi Raha akale na Bi Mdogo.

Bi Mdogo naye akizingua utaratibu ni uke Ile, ampandishe cheo. We live once oooh!
Yaani azidi kuongeza matatizo maishani?

#YNWA
 
Ndoa zenye amani bado zipo msi generalize maisha kuna watu wana enjoy sema wanaogopa kuleta ushuhuda wasije wakaambiwa hayajakukuta.
👆👆👆👆
Soma comment #25

#YNWA
 
Wanaume wenzangu bhana mnahangaikaaaa!!!
Ukitaka kuishi kwa amani na furaha ndani ya ndoa Bila kuona mdomo mrefu, makelele yasiyo na maana , ugomvi wa hovyohovyo Bila sababu maalumu kitu unachotakiwa kukifanya ni
"KUMROGA" narudia "MROGE"
Hii ndio maana ya kuishi nao kwa AKILI
Mnafikiri tulivyoambiwa tuishi nao kwa akili ni akili ipi mnadhani?
Acheni kupata tabu
Ukiona anaanza makelele na ugomvi unaenda kuongeza nyundo (UPDATE)
Hadi unakufa hutopata tabu ndani ya ndoa
 
Back
Top Bottom