Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Utawasikia nataka mwanaume anitunze, anipende anipe pesa...yeye mwenyewe ameshindwa kujitunza mpaka kuoipoteza ile kitu kwa wahuni, kama unataka matunzo baki kwa wazazj wako wawe wanakupa pocket money
Kuna wanaume wanatetea humu, Hatukatai wao kuangalia na kuchagua wenye nazo Ila twende mbele turudi nyuma, Je, wenye nazo na wasionazo wapi no wengi? Je, bila hela wanamaanisha Mapenzi hakuna?
 
Hivi kutimiza jukumu lako la kumhudumia mke wako nako ndiyo kupenda hela? Basi tuvunje huu mgawanyo wa majukumu ili iwe rasmi sasa wote mwanaume na mwanamke waingie mzigoni kutafuta pesa wasaidiane kulipa bills halafu na kazi za nyumbani pia liwe ni jukumu la wote unaonaje hapo?
 
Uchambuzi murua kabisa na wenye mashiko
 
Kuna wanaume wanatetea humu, Hatukatai wao kuangalia na kuchagua wenye nazo Ila twende mbele turudi nyuma, Je, wenye nazo na wasionazo wapi no wengi? Je, bila hela wanamaanisha Mapenzi hakuna?
Hivi kwanini mnalazimisha wanawake tu ndiyo wawe na mapenzi ya kweli wakati dunia ya sasa wanaume ndiyo wanaongoza kukosa mapenzi ya kweli? Siku hizi usaliti umeshamiri na wanaume mnajisifia kabisa kuwa ni nature hamtosheki na mwanamke mmoja sasa kama wewe kujicommit umeshindwa kwanini utake mwanamke ajicommit?
 
Kwa ufupi anasema kwanza tumpende mtu jinsi alivyo na utu wake na si vitu vyake. Vitu au mali ni ziada na mara nyingi mtafaidi vitu vizuri ikiwa upendo ulitamalaki bila hivyo vitu.

Watu ambao wanapenda vitu mara nyingi huvurugana bila vitu na wakiwa navyo napo huvurugana! Tanguliza upendo vitu vifuate, hata visipokuwepo amani itakuwepo.
 
Kwani huo mgawanyo upo?
 
Mapenzi ya kweli tuwape wenye Mapenzi ya uongo sio?
 
Umeeleweka mkuu
 
Husifanishe enzi za babu zako na sasa ktk ulimwengu huu wa kwenda na wakati na mitandao ya kijamii ,Smart phones na TV ni vitu viwili tofauti.Kaa chini jiulize kwa nini viongozi wengi siku hizi wa kiroho (masheikh, mapadri na wachungaji nk),wanatumia mda mwingi kusuluhisha matatizo ya ndoa kuliko kutoa huduma nyingine za kiroho.

Babu yako aliweza kuwacontrol hao wanawake wote sababu walikuwa watii na wasikivu, sasa hivi ukioa wanawake wawili, tuu unakuwa umejitengenezea moto wako wa Jehanum humu humu duniani.Kweli zipo ndoa zenye furaha chache sana, kila siku nikienda kanisani mapadri wanakazia sana maswala ya ndoa,manake wameshaona sababu wao kila siku wana deal na maswala ya ndoa.
 
[emoji736][emoji736]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…