Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mahakama ikiamua watoto wabaki na mama, bado baba anatakiwa atunze watoto na awasomeshe ingawa kwenye mgao watoto hawafikiriwi, mgao wa baba ni pamoja na watoto!
Sheria ya ndoa kandamizi ipitiwe kwanza ili mabadiliko ya sheria yazingatie usahihi wa mambo yanayotakiwa ktk mahusiano.

Kwenye mengine yoote wanahitaji haki sawa 50/50 lakini kwenye mahusiano anasulubishwa mwanaume
 
Sawa umeandika vizuri sana, sasa hio Bible unajua imeandikwa mara ngap yaan matoleo mangap na pia unajua kabla ya Bible kufanyiwa tafasiri ilikua kwenye lugha gan?

Nisikuchanganye sana huko turudi huku kwenye sheria ya Ndoa ya kwetu ambayo imetungwa na kuandikwa na Bunge ya mwaka 1971 na kufanyiwa marekebisho mara ya mwisho mwaka 2002, je wewe kwa uelewa wako ulionao unahisi sheria ya Ndoa imenyooka au Ina mashimo mashimo?

Yaan uunde program alafu ikae tu miaka zaidi ya 21 hauifanyii updates ZOZOTE unahisi hio program si inakua imepitwa na wakati au wewe unaonaje?

Hata hii JF unayoitumia tangu ianzishwe haijawa kua dormant tu bila kufanyiwa updates zozote, na sheria ya Ndoa pia inabidi ifanyiwe marekebisho imeshapitwa na wakati miaka 21 bila marekebisho yoyote ni inabaki kua sheria useless,
 
Ahsante sana kwa hoja hii.

Watu wanadhani hili suala ni la utani wa mitandaoni tu.

kila siku mwanaume anaonekana hapaswi kusikilizwa mawazo yake kwa sababu wanawake wamejanjaruka kwa mbinu ya kujitia unyonge huku wakifaidika na sheria kandamizi ya ndoa
 
Mabinti zako nao wakikua watakutana na wakataa ndoa na wataishia kuzalishwa alafu watakua wametimiza lengo lako la kukataa ndoa
Kabsa mkuu kwan ndoa ni uhai mkuu , nawafundisha kukataa kwanzia wakiwa wadogo wakizalishwa nitafurahia wajukuu kazi ya mwanamke ni kuzaa masta
 
Swali lako ungekaa na kutafakari kidogo tu ungejua ni mangapi ambayo ukiishi bila ndoa utayakosa, tatizo ni kuwa hujatafajari.
Binafsi ninaweza kuyapata yote bila ndoa.

Uwe na jioni njema.
 
Ndoa ni ya rohoni, fanya update rohoni.. bible ina miongozo yote ya ndoa.. Miongozo ya serikali ndio inawavuruga wasio elewa origin ya ndoa
 
Ndoa ni ya rohoni, fanya update rohoni.. bible ina miongozo yote ya ndoa.. Miongozo ya serikali ndio inawavuruga wasio elewa origin ya ndoa
Mzee samahani kwa hili swali Ila ningeomba ujibu inapobidi kwa kadri ya uelewa wako, Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 imeandikwa, imeandaliwa na imetungwa na nani?

Jibu hilo swali alafu tuendelee ukiweza jibu kwa ufupi bila maelezo mengi, ukishanipa jibu tuendelee kujadili hili jambo alafu kingine ondoa masuala ya ROHO maana hakuna sehemu kwenye SHERIA YA NDOA pametaja masuala ya ROHO

Naomba tu-base kwenye Sheria ya Ndoa, maana hapo ndio kuna utata kukitokea lolote mamlaka inaenda kufungua vifungu vya Sheria ya Ndoa sio Msahafu wala Biblia
 
Siangalii ndoa kwenye mfumo ambao unauzunguzia .. ndio maana hapa ni kama vuta nikivute.. ukienda kwenye sheri ndoa ina mbemba mwanamke hilo halina ubishi
 
Siangalii ndoa kwenye mfumo ambao unauzunguzia .. ndio maana hapa ni kama vuta nikivute.. ukienda kwenye sheri ndoa ina mbemba mwanamke hilo halina ubishi
Basi kumbe umeelewa nini kinachopingwa na wengi kuhusu Sheria ya Ndoa, huku kwenye masuala ya kiroho patashughulikiwa na viongozi wa kiroho pale inapobidi na hapalalamikiwi Ila Sheria ya Ndoa ndio Ina matatizo ukiisoma vizuri ukaielewa utagundua jambo kwamba hii Sheria mboni ni ya Beijing kabisa hii 1995 mwanamke akiwezeshwa anaweza
 
Serikali ( worldly system ) ipo kinyume na Spiritual system. Ndio maana migogoro ya ndoa kwenye akili humalizia ndani ya kanisa.. Sheria z dunia haziwezi fanya nipinge ndoa ambayo origin yake na muasisi ni Mungu
 
Serikali ( worldly system ) ipo kinyume na Spiritual system. Ndio maana migogoro ya ndoa kwenye akili humalizia ndani ya kanisa.. Sheria z dunia haziwezi fanya nipinge ndoa ambayo origin yake na muasisi ni Mungu
Sawa sikatai kulingana na uelewa wako kwa mujibu wa maandiko kwamba Ndoa imehasisiwa na Our Creator (Almighty God) Ila yapasa utambue kua pamoja na uasisi huo wanaofanya uwepo wa Ndoa ni wanadamu sio Our Creator na hakuna palipoandikwa kua kufunga Ndoa ni mandatory issue, hilo pia ulikumbuke kwa hio wapo wanaoamua kuishi pasina kufunga Ndoa, najua hilo unalitambua vizuri kabisa bila kupepesa macho yako
 
Naona kama unataka kujenga hoja kisha ghafla ukapoteana.

Ipo hivi.
Ndoa ni jambo jema sana lakini namna lilivyotengenezwa kwa sasa ni mwiba mkali kwa mwanaume. Ndoa hass sheria zake zinampa mwanamke faida kubwa na lukuki dhidi ya mwanaume. Maana pamoja na mahari lakini bado atapaswa kugawa kipato chake kwa mwenza ambaye anatambulika kisheria kuwa na haki sawa na mume.

Elewa mada
Elewa somo
Kataa ndoa hadi sheria mbovu zibadilishwe
 
Ndoa kisheria ni mkataba kama mikataba mingine
Hakuna mtu anayelazimishwa kuoa au kuolewa.
Lakini kiasili mwanamme anamwitaji mwanamke and vis versa
Ukikataa ndoa it means unataka yawepo mahusiano yasiyo ya kisheria kati ya hizi pande mbili jambo haliwezekani ni nul and void.
Issue kama Sheria inategemea upande mmoja au imepitwa na wakati ni mda WA kuibadilisha na sio kukataa ndoa, kampeni ingekua. Na maana Zaid kama ingelenga kuibadilisha Sheria ya ndoa.
Kuna mambo yanaweza kuchamgia madai ya kuibadilisha Sheria hiyo
Kwa Sasa WAnawake wengi wanaofanya kazi au Wana kipato kwa hiyo Wana wajibu pia WA kuhudumia familia na iwe kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…