Balqior
JF-Expert Member
- Jun 8, 2021
- 2,406
- 8,039
Hujamwelewa mtoa mada, shida sio mwanamke kuolewa na mtu mwenye mali nyingi, shida ni kuwa wanawake wengi wanaolewa kwasababu ya pesa ya mwanaume tu, na hawana hisia za kimapenzi na mwanaume aliolewa nae, sasa utakuta mdada akikuona anatamani atapike, jinsi anavyoona una sura mbaya, ila kwasababu una hela nyingi basi ataigiza kuwa anakupenda ili apate hela zako, yani wanaingia ndoani sababu ya pesa ya mwanaume tu.Babu yangu alioa wanawake Saba,na kila mmoja akazaa nae watoto kumi na mbili,na kila mmoja alijengewa nyumba na kupewa shsmba la ekari mbili.
Mengi uliyoyataja ni mahitaji ya kawaida ya mwanamke.
Je Kuna wanawake wabaya,gold diggers,yees wapo wengi!!!je Kuna ndoa zinazoumiza wanaume,zipo kibao,
Je Kuna ndoa na wanawake wazuri,?wapo weeengi tu.
Lakini Cha msingi tangu Dunia iumbwe,hakuna ndoa isiyo na matatizo!!!
Kuna ubaya gani binti,kutaka kuolewa na mtu mwenye uwezo au na mwelekeo wa kipato!?sasa unataka aolewe na kapuku,harafu uzao wake nao uishi kwa shida!umetoka familia maskini,umesoma kwa shida,uolewe Tena na kapuku harafu wanao Tena waishi maisha magumu!!!
Kijana Bado hujakomaaa,kama unatsfuta mwanamke wa kukupenda kwa mspenzi ya muvi za kifilipino na kihindi,usioe kabisa.
Ndoa ni maisha halisi sio maagizo,unaishi na binadamu sio maraika.
Sidhani kama wewe utafurahi ukigundua mke ulie naye yuko na wewe sababu ya pesa zako tu, na hana hisia za kimapenzi na wewe JUAN MANUEL