Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Tunachojaribu kushauri ni wanawake kuacha kuwa tegemezi kwa wanaume.
Mwanamke kuwa tegemezi mume wake hakuna ubaya wowote ule. Kwasababu atakaa Nyumbani na kuihudumia familia vizuri. Yeye atafanya kazi za Nyumbani ambazo sio kazi cha mtoto
 
Mwanamke kuwa tegemezi mume wake hakuna ubaya wowote ule. Kwasababu atakaa Nyumbani na kuihudumia familia vizuri. Yeye atafanya kazi za Nyumbani ambazo sio kazi cha mtoto
Ukifa?
 
Kama mwanaume akifa ni bahati mbaya . Ila ni kumpa uzoefu wa kazi mbalimbali mfano kilimo, biashara ndogo inatosha sio laxima Mwanamke awe mtumishi
Uzoefu huo unampaje kwa kumuacha afanye shughuli za nyumbani na kulea watoto pekee?
 
Uzoefu huo unampaje kwa kumuacha afanye shughuli za nyumbani na kulea watoto pekee?
Lazima utengee mda kiasi . Ila watoto wakilelewa vizuri na mama wanakuepo watoto supa Sana.
 
Ukweli mchungu ni kwamba ni ngumu sana, sio tu mwanaume akiwa kama mume bali hata tukizungumzia akiwa kama baba, ni ngumu sana kuongoza familia kama kipato hakiruhusu.
 
Ukweli mchungu ni kwamba ni ngumu sana, sio tu mwanaume akiwa kama mume bali hata tukizungumzia akiwa kama baba, ni ngumu sana kuongoza familia kama kipato hakiruhusu.
Kipato kinachoruhusu kinaanzia kiwango gani?
 
Kama umeoa na mkeo kwa miaka yote ya ndoa yako anatewa n.a. wapenzi wa zamani n.a. wapya wewe upo sasa kuna faida gani ya kuoa? Kuoa kwa mifano ya jamaa zangu ni upimbi kbsa
 
Ni mwanaume kapuku ndo anaweza andika maelezo meengi marefu yanayohusu mwanamke,, hata mwanaume kuchangia kwenye upupu wa hivi ni ukapuku tu unawasumbua,, kazaneni fainali uzeeni
 
Si niliwaambia msioe?

Mcheki huyu mwamba ndoa inavyomuua.

Hii imetokea kazini,
Huyu jamaa kanihuzunisha sanaaa...

Mkurugenzi kaunda team ya watu 4 kumsaidia Kazi fulani hivi huko field.
Katoa na gari.

Katika hiyo timu tupo wa4 + dereva jumla wa5.

Kati yetu aliyeoa ni mmoja tu na kwakuwa kaenda age kidogo kuliko sisi then tuliamua kumpa ukuu wa msafara.

Sasa bana Kazi yenyewe tuliyopewa ilianza 20/12/2021.

Tulipiga Kazi na kuelewana 23/12 turudi makwetu kimyakimya tukale sikukuu na atakayepigiwa simu ajibu tupo kazini/field.

Ila huyu jamaa aliyeoa alikataa "Lazima tupige kazi mpaka sikukuu (X-Mass), tuheshimu Kazi za watu hizi jamani"

Aisee wotee tulimshangaa "Braza halmashauri ya baba ako?"

Baada ya mzozo mrefu sisi ndio tulishinda.

Tukasepa 23 na kurudi field 27/12.

Hali hiyohiyo ikajitokeza mwaka mpya.

Aligoma kurudi makwetu tarehe 29 ili tukale sikukuu.

Na kuonyesha yupo serious alipiga simu ofisini kuwa tunataka kumfelisha mkurugenzi.

Sasa bana Hawa raia wengine walimkasirikia balaaa.

Kwenye mapumziko ya usiku wa 29/12 Mimi ilinibidi nimpeleke bar fulani hivi chemba na kumuuliza "Braza unataka kutufanyisha Kazi mwaka mpya kwani halmashauri ya baba ako?"

Aisee baada ya bia kukolea mwamba aliamua kufunguka hasaa.

Alisema...

Kazini watu humuona yeye mchapakazi Bora, wanamuona sio mtoro kazini, wanamuona akipiga Kazi mpaka sikukuu, wanamuona ni mpiga Kazi mpaka usiku (huyu mwamba siku nyingine hutoka kazini saa 4 usiku).
Basi raia wanamsifiaaa kwamba ni mchapakazi, kumbe mwamba huwa ANAKIMBIA MAKELELE YA MKEWE NYUMBANI ...!!!

Anasema Ndoa yake ni ngumu sanaa na kinacholeta ugumu ni mdomo wa mkewe.

Mkewe ni mbogo hasa, ukimchokonyoa tu ni kama shimo la siafu, ni full kutapika neno lolote alionalo kwake linamfaa..!!!

Hali hii imemfanya jamaa kukimbia nyumbani na hali hii imemfanya apaone kwake ni jehanamu ya amani yake...!!!

Ndio maana hata zile sikukuu kama tusipoingia kazini basi ni yeye kwenda kuishi na mkewe siku nzima ndani..!!!

Ila kwenye maongezi yake anasema, alioa 2016 na mkewe alimkuta jamaa ana maisha kiasi (gari na nyumba vilikuwepo).

Kwahiyo mkewe alikuja kwenye maisha yake akiwa na maisha tayari.

Yeye na mkewe Wana watoto Wa3.

Hawezi kumuacha kwasababu ya watoto ila pia mdomo wake umemshinda...!!!

Nilibaki kumuonea huruma tu.

Sasa mi najiuliza....

1. Yaani alioa ili aikimbie nyumba yake aliyoijenga kwa gharama?

2. Kama anarudi usiku means yeye na watoto hawaonani, Kwahiyo alioa ili Awe ANAKIMBIA watoto?

3. Sasa kama alikua tayari na maisha KWENYE NDOA ALIENDA KUTAFUTA NINI?

ILA KUNA RAIA WABISHI...

Msioe ndugu zangu MTAKUFA.

We una nyumba una gari UNAOA ILI UTAFUTE NINI?

Inakuaje mwanamke uliyemtolea Mahari akufanye ukimbie nyumba?

Ila bana mwisho wa siku kama pole nilimpa na field hatukuingia...!!

Nilimwambia aende tu kupambana na mkewe sisi ma single men tukale sikukuu na usingle wetuu..!!!

Yaani baharia...

Unamuona mwamba anakomaa na Kazi mpaka usiku KUMBE NYUMBANI PAMOTO.

Unamuona baharia aondoki mapema bar KUMBE NYUMBANI PAMOTO.

Unamuona mkulungwa kila siku akitoka job ni kuzurura KUMBE NYUMBANI PAMOTO..

MSIOE MTAKUFA.

Tuendelee kutafuta hela

"If you think money can't bring happiness then go and ask the homeless and the Jobless"

#YNWA
 
Back
Top Bottom