Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Niliwahi shitakiwa na mtalaka wangu kituo fulani cha polisi jijini Dar,nikaletewa barua ya wito.siku nakwenda kusikiliza nilichoitiwa nilipokelewa kwa maneno ya kejeli na askari wa kike waliokuwa pale kituoni.baada ya mahojiano na kuelezwa yale aliyokwenda kushtaki mtalaka,nikawajibu tu simple kuwa nina ushahidi wa kutosha juu ya vitendo alivyofanya hadi akaamua kuondoka mwenyewe nyumbani
1, kupewa ujauzito na Hawara yake kisha mm nilee mtoto nikijua ni wangu kumbe nimepachikwa.
2,kunitoa roho kwani kwake sikuwa na thamani tena hivyo alitaka kubadili mme.
3,kumuwekea mtoto wangu sumu ili afe kuondoa tofauti utakapojitokeza kati yake na mtoto wa mchepuko.
Baada ya kuweka ushahidi wa audio na kusikilizwa,wale ma wp waliondoka bila kuaga,aliyesalia(inspector) alinipa pole na kunisifu kwa uvumilivu nilionao na kumwambia mtalaka jamaa kwa ushahidi alionao akienda mahakamani hutoboi.sasa hivi hata kutongoza mwanamke naogopa.
Duh pole sana kaka hakika sisi wanawake baadhi yetu tunaroho mbaya hivi unaujasir upi kubeba mimba nje na kumsingizia mume nabado kujarb kutoa uhai wa mtoto kwel anastahil adhabu ya kifo
 
Si niliwaambia msioe?

Mcheki huyu mwamba ndoa inavyomuua.

Hii imetokea kazini,
Huyu jamaa kanihuzunisha sanaaa...

Mkurugenzi kaunda team ya watu 4 kumsaidia Kazi fulani hivi huko field.
Katoa na gari.

Katika hiyo timu tupo wa4 + dereva jumla wa5.

Kati yetu aliyeoa ni mmoja tu na kwakuwa kaenda age kidogo kuliko sisi then tuliamua kumpa ukuu wa msafara.

Sasa bana Kazi yenyewe tuliyopewa ilianza 20/12/2021.

Tulipiga Kazi na kuelewana 23/12 turudi makwetu kimyakimya tukale sikukuu na atakayepigiwa simu ajibu tupo kazini/field.

Ila huyu jamaa aliyeoa alikataa "Lazima tupige kazi mpaka sikukuu (X-Mass), tuheshimu Kazi za watu hizi jamani"

Aisee wotee tulimshangaa "Braza halmashauri ya baba ako?"

Baada ya mzozo mrefu sisi ndio tulishinda.

Tukasepa 23 na kurudi field 27/12.

Hali hiyohiyo ikajitokeza mwaka mpya.

Aligoma kurudi makwetu tarehe 29 ili tukale sikukuu.

Na kuonyesha yupo serious alipiga simu ofisini kuwa tunataka kumfelisha mkurugenzi.

Sasa bana Hawa raia wengine walimkasirikia balaaa.

Kwenye mapumziko ya usiku wa 29/12 Mimi ilinibidi nimpeleke bar fulani hivi chemba na kumuuliza "Braza unataka kutufanyisha Kazi mwaka mpya kwani halmashauri ya baba ako?"

Aisee baada ya bia kukolea mwamba aliamua kufunguka hasaa.

Alisema...

Kazini watu humuona yeye mchapakazi Bora, wanamuona sio mtoro kazini, wanamuona akipiga Kazi mpaka sikukuu, wanamuona ni mpiga Kazi mpaka usiku (huyu mwamba siku nyingine hutoka kazini saa 4 usiku).
Basi raia wanamsifiaaa kwamba ni mchapakazi, kumbe mwamba huwa ANAKIMBIA MAKELELE YA MKEWE NYUMBANI ...!!!

Anasema Ndoa yake ni ngumu sanaa na kinacholeta ugumu ni mdomo wa mkewe.

Mkewe ni mbogo hasa, ukimchokonyoa tu ni kama shimo la siafu, ni full kutapika neno lolote alionalo kwake linamfaa..!!!

Hali hii imemfanya jamaa kukimbia nyumbani na hali hii imemfanya apaone kwake ni jehanamu ya amani yake...!!!

Ndio maana hata zile sikukuu kama tusipoingia kazini basi ni yeye kwenda kuishi na mkewe siku nzima ndani..!!!

Ila kwenye maongezi yake anasema, alioa 2016 na mkewe alimkuta jamaa ana maisha kiasi (gari na nyumba vilikuwepo).

Kwahiyo mkewe alikuja kwenye maisha yake akiwa na maisha tayari.

Yeye na mkewe Wana watoto Wa3.

Hawezi kumuacha kwasababu ya watoto ila pia mdomo wake umemshinda...!!!

Nilibaki kumuonea huruma tu.

Sasa mi najiuliza....

1. Yaani alioa ili aikimbie nyumba yake aliyoijenga kwa gharama?

2. Kama anarudi usiku means yeye na watoto hawaonani, Kwahiyo alioa ili Awe ANAKIMBIA watoto?

3. Sasa kama alikua tayari na maisha KWENYE NDOA ALIENDA KUTAFUTA NINI?

ILA KUNA RAIA WABISHI...

Msioe ndugu zangu MTAKUFA.

We una nyumba una gari UNAOA ILI UTAFUTE NINI?

Inakuaje mwanamke uliyemtolea Mahari akufanye ukimbie nyumba?

Ila bana mwisho wa siku kama pole nilimpa na field hatukuingia...!!

Nilimwambia aende tu kupambana na mkewe sisi ma single men tukale sikukuu na usingle wetuu..!!!

Yaani baharia...

Unamuona mwamba anakomaa na Kazi mpaka usiku KUMBE NYUMBANI PAMOTO.

Unamuona baharia aondoki mapema bar KUMBE NYUMBANI PAMOTO.

Unamuona mkulungwa kila siku akitoka job ni kuzurura KUMBE NYUMBANI PAMOTO..

MSIOE MTAKUFA.

Tuendelee kutafuta hela

"If you think money can't bring happiness then go and ask the homeless and the Jobless"

#YNWA
Kama haya unayoyasema ni ya msingi basi hata baba yako asingeoa na badala yake angekuzaa wewe kwenye uzinifu mitaani. Lakini alioa na huenda yupo na mama yako hadi leo wanaishi kwa raha mustarehe!!

Sio kila aliyeoa anakimbia nyumba yake, wengine tunafurahia ndoa zetu kama tupo peponi!!!

Chagua familia njema ya kuoa, sio unavamia vamia tu viruka njia vya madanguroni utaona ndoa chungu. Sio kweli kwamba kila ndoa ni jehanamu kama ya huyo nduguyo.

Pia kumbuka usipoa utazini na kuzaa watoto wa zinaa na hiyo ni dhambi mbele za Mola wako.

Karibu ndoani bwana mdogo!!
 
Walio oa na masingle nyote hamna kesi ya kujibu-----------nolle prosequi. Jumaa Karim
 
Hayo uliyoandika hapo ndo yalinifanya niache mwanamke tukiwa na watoto wadogo wawili, niliacha mwanamke tukiwa na mtoto mmoja wa miaka miwili na nusu na mwingine wa miezi mitatu
Yaani changamoto nilizopitia ningeendelea kuishi na yule mwanamke angeweza kuniua au mimi kumuua yeye, yaani ilifikia kipindi nikawa naishi nae kwa tahadhari,

Kuna kipindi hata kurudi nyumbani nikawa sitamani, yaani nikiwa kazini ukifika muda wa kurudi nyumbani naanza kunyong'onyea, furaha yote inaisha, nikawa najikuta napachukia nyumbani

Wacha niishie hapa, nimeshachukua kadi ya uanachama kwa Liverpool VPN
Tatizo lilikuwa nini? Ungetueleza! Alikuwa anamdomo sana au hakupi mbususu?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo lilikuwa nini? Ungetueleza! Alikuwa anamdomo sana au hakupi mbususu?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Mkuu, alikua akiniweka wiki mbili bila kunipa mbususu, pia alikua na dharau yaani alikuwa anataka yeye ndo awe mwanaume mimi niwe mwanamke (anitawale).

Alikua anaishi maisha ya tamthilia

Mkuu nenda kwenye uzi wa Mshana Jr unaoitwa MADA MAALUM KWA WANANDOA kyle nimefunguka kwa uchache
 
Kama haya unayoyasema ni ya msingi basi hata baba yako asingeoa na badala yake angekuzaa wewe kwenye uzinifu mitaani. Lakini alioa na huenda yupo na mama yako hadi leo wanaishi kwa raha mustarehe!!

Punguza abuse and Pessimism.
Hakuna MTOTO aliyezaliwa UZINIFUNI.
Hakuna MTOTO aliyezaliwa MTAANI.

#YNWA
 
Tulishakubaliana mwanaume ukishindwa kuishi na mke akili huna,,
Kauli ya kujidanganya hii.

Fanya ujinga maksudi usingizie akili?

Kwanini inakuja baada ya miaka kadhaa na siyo mwanzoni.
 
Kama haya unayoyasema ni ya msingi basi hata baba yako asingeoa na badala yake angekuzaa wewe kwenye uzinifu mitaani. Lakini alioa na huenda yupo na mama yako hadi leo wanaishi kwa raha mustarehe!!

Sio kila aliyeoa anakimbia nyumba yake, wengine tunafurahia ndoa zetu kama tupo peponi!!!

Chagua familia njema ya kuoa, sio unavamia vamia tu viruka njia vya madanguroni utaona ndoa chungu. Sio kweli kwamba kila ndoa ni jehanamu kama ya huyo nduguyo.

Pia kumbuka usipoa utazini na kuzaa watoto wa zinaa na hiyo ni dhambi mbele za Mola wako.

Karibu ndoani bwana mdogo!!
Furaha ya ndoa kama peponi iko mwanzoni tu,Kaa ukijua hiyo furaha hata ifike miaka 10 kuna muda itaisha na utaona kero.

Ni wewe utaamua sasa uvumilie au ujiondoe!!

Walioko kwenye ndoa wengi wanavumilia tu kwa sababu ya watoto,anaona bora avumilie alee watoto tu kusudi wasihangaike,Lakini ukweli anaujua yeye.[emoji14]
 
Kauli ya kujidanganya hii.

Fanya ujinga maksudi usingizie akili?

Kwanini inakuja baada ya miaka kadhaa na siyo mwanzoni.
Heeey unamkasirikia Nani sasa, kwani mi ndo niliwaambie mtumie akili au ukose akili!!! Hebu pita huko
 
Heeey unamkasirikia Nani sasa, kwani mi ndo niliwaambie mtumie akili au ukose akili!!! Hebu pita huko
Mimi nikasirike kwani naolewa?

Anae kasirika ni yule anae hisi Kwa Uzi huu hataolewa maana ni WA kupotosha wanaume wanao oa na kujipa moyo wa mwanaume Mwenye akili ndiye anao.[emoji14].
 
Mimi nikasirike kwani naolewa?

Anae kasirika ni yule anae hisi Kwa Uzi huu hataolewa maana ni WA kupotosha wanaume wanao oa na kujipa moyo wa mwanaume Mwenye akili ndiye anao.[emoji14].
Kama mke humuwezi maana yake akili hauna, period,, usilete bla bla
 
Furaha ya ndoa kama peponi iko mwanzoni tu,Kaa ukijua hiyo furaha hata ifike miaka 10 kuna muda itaisha na utaona kero.

Ni wewe utaamua sasa uvumilie au ujiondoe!!

Walioko kwenye ndoa wengi wanavumilia tu kwa sababu ya watoto,anaona bora avumilie alee watoto tu kusudi wasihangaike,Lakini ukweli anaujua yeye.[emoji14]
Kama ni kero za wanawake hata usipomuoa utakutana nazo tu kero zao unless uamue kuwa hanithi au mpiga punyeto. Kwani ndoa ikikushinda si unaivunja tu na kuoa mwingine.
 
Kama ni kero za wanawake hata usipomuoa utakutana nazo tu kero zao unless uamue kuwa hanithi au mpiga punyeto. Kwani ndoa ikikushinda si unaivunja tu na kuoa mwingine.
Kero za ndani ya ndoa na nje ya ndoa ni tofauti ndio maana VPN Liverpool kasema msioe.

Utaachana na wanawake wangapi na kuoa wanawake wangapi wengine?

Si bora uache tu kuepukana na kero.
 
Wakuu habarini za sasa ...
Nasisitiza vijana musioe wanawake bora mkaishi wenyewe miaka yote ...cha msingi tafuta pesa ...mtafute Mungu...tena na tena tafuta pesa ....
Yaliyonikuta baada ya kuoa najuta hapa nilipo nipo dawati la jinsia na nimenyang'anywa mali zangu zote nilizotafuta kwa jasho langu ...narudia tena vijana musioe
 
Kwakua yamekukuta wewe, basi sisi wengine tusioe? We mwehu nini!

Mimi nitaoa soon. Likinikuta jambo, napiga chini then naoa tena. Sio atoke mlamba asali mmoja huko, aje kuniambia eti niachane na asali kwakua yeye ameng'atwa na nyuki.

Asee tuheshimiane!
 
Back
Top Bottom