Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)

Ona Sasa haya mambo, kabla ya sasa jamaa alikuwa yupo vzr ila mke ndokamfilisi. Jamaa kawajengea wakwe zake ila wazazi wake wa kumzaa wanaishi kwenye banda la nyasi na kuta la Mavi ya punda. Mke wake waliyeachana saizi yupo Kwa wazazi wake anakaa kwenye mjengo mpyaa ambao jamaa aliwajengea
Unamlaumu mwanamke wakati mwanamme mwenyewe ndiye zwazwa.

Imekuwaje unajengea wakwe wakati wewe mwenyewe huna sehemu ya kuishi? Hizo priorities zimekaa kivipi?
Angekuwa kijana wangu ningemchapa viboko ijapokuwa ni mkubwa
 
Ngoja ufike umri fulani, uone atakavyokubadilikia.
Wewe mwenyewe hujafikia huo umri ila tayari usha feed akili yako negativity za kutosha, hivi haukijui kitu kinachoitwa law of attraction. Unapowaza mambo kijinga jinga yanakuja kujidhihirisha kiuhalisia kupitia matendo yako aidha kwa kujua au kutokujua.
 
Hakuna mtu asiyependa jambo la kheri kama kuwa na ndoa na familia yenye furaha, hili jambo ukilitizama kwa mtazamo chanya ni jambo zuri sana.


Tatizo ni sisi watu wenyewe kutokana na changamoto za maisha na mabadiliko katika kila nyanja za ukuaji tumekuwa hatufai tena ku fit katika hili jambo,matendo yetu yanafanya liwe jambo baya na la kujutia sometimes..

Hata ambao kwa sasa wapo ndoani wanapitia changamoto ngumu sana wengi wao.

Asilimia kubwa ya vitu ambavyo mungu alitia baraka ni chanya sana.
Tatizo ni sisi wenyewe...
Kuna haja ya kutafakari kama Jamii ni wapi tulipokosea.

Wimbi la wengi wanaokataa ndoa ni vijana waliozaliwa miaka ya 1987 kuja juu.

Ni kweli maisha ni magumu na kupata wenza wenye uwezo wa kuvumilia uduni wa maisha ni changamoto pia.

Lakini nimekutana na Mabinti na Wanawake wengi wanaliochoshwa na Usingo maza na wako tayari kuolewa na kutulia.

Vyema kumshirikisha Mungu kwenye hili.

Lakini bado ndoa ni Jambo la kheri sana kuelekea Ustawi wa familia na kesho ya watoto wetu
 
Hiyo ni zaman dhama zimebadilika sana nowadays..

Tuliwaona wazungu wajinga na hawajielewi wameweka ndoa za mikataba na wengi hawaoi kumbe lilikuwa swala la muda tu now tunaiga life style yao kwa speed sana.

Itoshe kusema wazungu ni akili kubwa wale watu.
Bado sijaona sababu zenye mashiko kukataa kuoa
 
Wamebembelezwa sana hadi wanaona kuwa maisha bila wao hayawezekani. Sasa sisi tuwabembeleze na bills tunalipa mwenyewe, achana na hizo mbaga.
Suala la kuhudumia Mwanamke bado ni Jukumu la Mwanaume.

Hilo ni takwa la Kimungu kabisa.

Muhimu tuendelee kumshirikisha Mungu kwenye kila jambo hasa la ndoa
 
Jamii yetu ilipofikia ni kwamba tuna hadi viongozi wa umma ambao wanaonekana tu wakilea watoto au mtoto huku baba wa mtoto hajulikani, huko mbele tutegemee kuona viongozi mashoga na mabasha.
Sahihi kabisa Mkuu, kama Mtoto analelewa Na Mama pekee manake atakuwa anajifunza vitu vingi vya kike. Sasa akiwa Mwanaume ndiyo zile traits za Kike zinaanza kumuandama hivyo kujikuta Ana tabia za kike kike.

Mungu atusaidie Wanaume turejee kwenye Uanamme wetu na kukubali kuoa
 
Ni Utapeli na ni Ujinga , Ujambazi wa mchana kweupee
Ndoa Ni Parasitic mode of nutrition

ME anaumia, KE ananeemeka
Huo Ni Upumbavu mbwa haruki
Ni wajinga pekee wanaopigwa, werevu kamwe HAWAOI
Kwamba ni dhambi kumuhudumia mwanamke anayelea watoto wako, anatekupa utamu kila siku?

Tena sisi wengine tulishajizoelea kwenda round zone zile then tushindwe kuhudumia ili aendelee kupendeza?
 
Nashangazwa na mnaopenda kutumia mahusiano ya watu ambao sio jamaa zenu wala ndugu zenu. Hivi kwenye ukoo wenu wote umekosa ndugu yako hata mmoja ambaye anaweza kuwa role model wako ?

Uache ujinga, hakuna mfano ambao kila mtu anaweza uelewa na kuujua kama huu, once you put your life in public utatumika kama mfano.

Ndo maana kwenye rulling mahakaman wanatumia kesi zilizopita kama mfano!
 
Hivi hizi Kampeni zinazoendeshwa za Wanaume kukataa Ndoa zina fadhiriwa na nani na kwa lengo gani?

Imagine Wazee wetu wasinge mwoa Bi Mkubwa wako, leo hii mngekuwa hapo mlipofikia?

Familia ndiyo Msingi wa Jamii bora, ndiyo msingi wa Serikali imara.

Nadhani badala ya kuhimizana kukataa Ndoa, ni vyema kuhimizana kupiga goti kwa Mungu kuomba akujalie kupata mke mwema. Wanasema Mke mwema hutoka kwa Bwana.

Tukiacha haya mambo yakue na kuchipua kuna hatari ya kuwa na jamii ya hovyo sana huko mbele ya safari.
na huu ujinga umeshamir kwelikweli vijana wamechagua a wayout kwakujikita kuifanya hii kampeni hiyo yote ni kukimbia/kukwepa majukumu hawataki kuumiza kichwa kabisa mwisho wa siku ndomishoga inaongezeka
 
Ona Sasa haya mambo, kabla ya sasa jamaa alikuwa yupo vzr ila mke ndokamfilisi. Jamaa kawajengea wakwe zake ila wazazi wake wa kumzaa wanaishi kwenye banda la nyasi na kuta la Mavi ya punda. Mke wake waliyeachana saizi yupo Kwa wazazi wake anakaa kwenye mjengo mpyaa ambao jamaa aliwajengea
Unamlaumu mwanamke wakati mwanamme mwenyewe ndiye zwazwa.

Imekuwaje unajengea wakwe wakati wewe mwenyewe huna sehemu ya kuishi? Hizo priorities zimekaa kivipi?
Angekuwa kijana wangu ningemchapa viboko ijapokuwa ni mkubwa
 
Back
Top Bottom