Ila uko hapa unashinikiza watu wakatae ndoa wakati wewe na watoto unao. Akili kumkichwa
Yaan Hawa wanaokataa ndoa 98% hawajui ndoa ni nini.

Mwengine atakwambia nimeoa ila sijafunga ndoa.

Mwingine atakwambia naishi nae mwanamke na watoto Wangu ila sijaoa.

Mwingine atakwambia nitamzalisha mwanamke na kutunza wanangu. Hali ya kuwa anachokikwepa kwenye ndoa muda wowote kinamkuta.
 
Funga ndoa ya cheti then ishi nahuyo mwanamke sku mbili mwache ,then nenda kaishi na mwanamke miaka 40 bila cheti ,then yule ulieishi nae sku mbil mwenye cheti akupeleke mahakamani ndio utajua una wake wawili au mmoja.
Anaamua kujizima data unafikiri haelewi[emoji4]

Lakini hizi sheria za ndoa waliotunga sidhani kama waliwashirikisha wanaume
 
Nilijua una hoja kumbe na ww hauna hoja , mkuu kataa ndoa za sasa, ni utapeli ila kma umeshafunga ww ni kamari umecheza pia mda wowote unaweza kuwa timu kataa ndoa.
Mkuu si umesema mwenyewe kwamba mkeo (huyo unaeishi NAE) ni Kahaba ndio maana humuoi.

Na kama sio hivyo unachokiogopa kurasimisha ndoa ni nini. Mbona unajikanyaga kanyaga.
 
Hahaha, anipe yeye mali zake tuone, tukiachana akikaa na watoto siwahudumii kwani? Na akiolewa je na mali zangu ziwe za mme wake mpya?! [emoji23][emoji23]
Hao ni ile tim kiria super nini sjui [emoji23][emoji23]
Huwezi ukaamini yupo serious eti
 
Mkuu haibadilishi kitu kabla ya wazungu hawajaja hilo neno ndoa lilikua halipo , ndoa ina ambatana na haki sawa , usawa na kijinsia , na haki za mashoga , watetezi wa haki za ndoa ni hao hao watetezi wa haki za mashoga Leo hii taasisi ya ndoa inaweza fungisha ndoa za mashoga na msifanye kitu ,kwa sababu ndoa sio hasili na sheria za kila mtu ana uhuru wa kuchagua ziwabane . Tunakataa sheria zote zinzopingana na nature , kama haki sawa kati ya me na ke , haki sawa mwanaume akizagamuliwa , wakataa ndoa wote wanaongozwa na mfumo dume .
 
Mkuu si umesema mwenyewe kwamba mkeo (huyo unaeishi NAE) ni Kahaba ndio maana humuoi.

Na kama sio hivyo unachokiogopa kurasimisha ndoa ni nini. Mbona unajikanyaga kanyaga.
Dhumuni la kujikanyaga ni kukushtua uache kujizima data mkuu
 
Naona watu ambao wanalalamika walioa au kuolewa wamajuta si kwasababu ya ndoa bali makosa yao wenyewe. Unaambiwa KOSEA VYOTE ILA KUOA AU KUOLEWA ulidhani waliyousema walikurupuka?

Ndugu zangu ndoa hawaangalii uzuri wa umbo au sura ya mwanamke, wala sura ya mwanaume au pochi yake. Kutaka kuoa utafute mtu mwenye akili za maisha anayeweza kuja kusimamisha familia bora nawe na si kukimbilia kuoa kisa umeona ana tako au pisi kali. Mabaharia wana msemo PUNDAMILIA TUNAENDA KUMWANGALIA MBUGANI ILA HATUMLETI NYUMBANI, ILA PUNDA WA KAWAIDA NDIYO TUNAISHI NAYE. Huu msemo wanamaanisha hizo pisi kali mnazokimbilia nyingi hazifai kuweka ndani, ukija kujaribu utajuta sana.

Wengine kinadada wanaingia kwenye ndoa kisa hela au jamaa ni mzuri kupitiliza au kushawishiwa tu aolewe na mtu fulani, wanafikiri hizo pesa au uzuri vitakuja kumfanya awe na tabia njema na akili za kujenga familia. Mambo yakija kwenda kinyume utaanza kusikia ndoa hazifai kabisa, si useme tu maamuzi yako wewe ya kukurupuka kisa mkumbo na kufuata kitu fulani ndiyo hayafai.

HAPA NILIPOSOMA POST ZA MWANZO NIMEONA KADHAA WAMEKOSEA KUOA WANASHAWISHI NA WENGINE WASIOE KISA MAKOSA YAO WENYEWE. JAMANI NDOA NI PEPO MOJA TAMU SANA KAMA UTAPATA MWENYE DIRA YA MAISHA NA KUJITAMBUA. PIA NDOA NI JEHANNAMU KAMA UTAKURUPUKA NA KUIKIMBILIA KISA UZURI AU KITU FULANI AU KUFUATA MKUMBO TU WA KUSHAWISHIWA.

MLIYOIONA JAHANNAMU MSIILAUMU NDOA BALI LAUMUNI MAKOSA YENU YA KUKOSEA WA KUOA AU KUOLEWA NAYE
 
Wakuu emu kabla mdaharo haujaendelea kwanza kasomeni ndoa ni nini na Sheria za ndoa ni zipi, haki za mke ni zipi , haki za mume ni zipi, taratibu za mirathi na talaka zipoje. Ili mkirudi tujue tuchobishana hapa ni kipi ? Naona wengine hata wanachokipinga hawakijui vizuri na wengine wamekifanya wanachokipinga.
 
Mkuu haina haja ya kusoma , tumeona yanayomtokea mwaka ,familia ya mengi na wengi kitaa .
 
Maskin!!!! namwona kabsa Israel alivyotwaa ndoa yako,,, pole ila sasa najiuliza baada ya hayo utawaonaje wanawake wenzake???

Mmh naona kule kwetu bado hawajajanjaruka,, maana ni wavumilivu wa kila hali ya maisha,,,
 
Kufunga ndoa ni kamari tu , haimaanishi kamari ni nzuri ata kama ukila pesa .
 
Mfumo Dume ni kuoa na kuhudumia. Tena sio kuoa tu kuoa kwa sherehe kadri ya uwezo. Alokwambia mfumo Dume ni kuishi na mwanamke ndani pasina kurasimisha uanaume wako kwa jamii kupitia sherehe ya ndoa nani ?
 
Wenye ndoa si ndio hawa huku tunaopoa nao milipo ya bar[emoji3][emoji3]
 
Mfumo Dume ni kuoa na kuhudumia. Tena sio kuoa tu kuoa kwa sherehe kadri ya uwezo. Alokwambia mfumo Dume ni kuishi na mwanamke ndani pasina kurasimisha uanaume wako kwa jamii kupitia sherehe ya ndoa nani ?
Basi wewe ni kataa ndoa ila haujajitambua tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…