Saizi unakataa maelezo yako tena? Ukija kubishana na mimi uwe unaweka records zako straight. Unajifurahisha tu hapa ila hilo swala la kataa ndoa kubali kwamba hujui ndoa ni nini. Haya maelezo hapa chini sio ya kwako? Sasa hivi unasema tena ulimfukuza sijui bla bla.
Hakuna watu nawapenda kama mabinti zangu watatu mama yao na mama yangu , hyo haibadilishi kwamba kwa sasa ndoa ni utapeli kwa mwanaume.
 
Ndivyo alivyomlea. Kipato cha Buku unaongaje laki.
Oooya hujielewi jamaa kaoa baada ya kupata kazi take home 2M, akichukua mshahara wote anaenda kumpa mwanamke sio tia maji tia maji na mwanamke kamtoa choka mbaya uswahilini
 
Yaan usiniletee kipande chochote cha LMA kunielezea huo ushubwada wako nishakwambia hio Sheria ni Mbovu unataka nini kingine?
🀣🀣🀣acha kupanic tubishane kwa hoja. Mimi sikuletei utaenda kukutana nayo mahakamani yakikukuta. Tena bora hiyo sheria tuifanyie kazi ikaze: haiwezekani mwanamke ukamzalisha watoto kama kumbikumbi humuoi eti unategemea siku utamtupa tu na asipate stahiki zake. At the same time unakuta ulimwachisha kazi ili akulelee watoto wako. Huo muda aliopoteza nani anaulipa? You are selfish. Hiyo sheria mnasema haiwasaidii nyinyi ila sheria inayowaruhusu kuacha na kwenda kuoa hovyo inawasaidia vipi wanawake waliopoteza muda kulea familia yako na out of the blue unamtelekeza anaanza tena kukimbizana kwenye madawati kudai ada na matunzo ya watoto. Lazima mnyooke sasa ndo nimeelewa mnachotaka. Hii sheria lazima itiliwe mkazo. Hadi muwe na adabu. Haiwezekani kwenye ndoa shida iwe mwanamke tu. Hata nyie wanaume mnapuyanga vile vile.
 
Uonavyo tu ila hyo sheria nilishaishinda , ndoa zote zinasajiliwa na serikali hyo yako sijui umeitolewa wap
 
Kama umekosa mwanamke ambaye hajafata mali kwako basi ni sawa kutokuoa.
Mkuu, inatupasa kutofautisha kati ya kuoa na kufunga ndoa. Zamani babu zetu walikuwa wanaoa ila baada ya kuja dini za kigeni yapata miaka 100 iliyopita ndo wakaanzisha kufunga ndoa.

Ukiangalia hoja za vijana hawakatai kuoa ila wanakataa kufunga ndoa. Kufunga ndoa kuna masaibu mengi maana wanawake wa siku hizi wana tabia ambazo huwezi kuzivumilia.

Nadhani vijana kwa sasa waoe kwa kupeleka mahari nyumbani kwa binti na watambulike ila wasifunge mkataba wa ndoa.
 
Itoshe kusema Sheria ni mbovu alafu mnataka kuiongeza ubovu basi mtaoana wenyewe hatuoi tunazalisha, kwani lazima?
 
Uonavyo tu ila hyo sheria nilishaishinda , ndoa zote zinasajiliwa na serikali hyo yako sijui umeitolewa wap
Na wale wanaofunga ndoa kimila wanasajiliwa na serikali gani? Yani hiyo hiyo serikali unayosema inasajili inatambua swala ya presumption ya miaka miwili wewe unakuja na nadharia zako. Nasema hiyo sheria acha ikaze. Na tutahakikisha inakaza. Endeleeni kujipa moyo. Lasivyo muwe mapadri msichezee watoto wa watu
 
Mkuu sheria za ndoa ni za kijnga mno , tunachotaka nibadiliko kwnye hizo sheria , tabia za wanawake hubadilika sna unapo funga nao ndoa .
 
Ingekua ni kirahisi hivyo kusingekuwa na maana ya sahihi ya mashaidi ,hyo ndoa ya hvyo inaupenyo wakuiruka kama haina mashaidi na sahihi .
 
Itoshe kusema Sheria ni mbovu alafu mnataka kuiongeza ubovu basi mtaoana wenyewe hatuoi tunazalisha, kwani lazima?
Unamzalisha akiwa mawinguni? Unaweza ukamzalisha akaondoka kwenda kwa mwanaume mwengine mwenye uelewa na akalea mtoto wako bila wewe kutambulika kama baba. Hizo sheria zote lazima zikae sawa. Mtanyooka. Hamuwezi kuchezea watoto wa watu mnawazalisha, mnakuja kuwatukana humu eti single mothers huku nje bado mnawazalisha tu bila mpango. Ni sheria mbovu kwa wanaume selfish kama nyinyi. Bado tunakusanya hoja zenu. Tunapita mule mule kuhakikisha hayo mnayoyapinga yanaongezwa kwenye vipengele. Hamtaki wanawake strong mnawaita feminists kwasababu mnajua wanajua haki zao. Mnataka hawa ambao mnawazalisha na kuwatelekeza hamjui mtoto anaishije alafu mnarudi baada ya miaka ishirini kujifanya umeikumbuka damu yako. Nasema endeleeni kujieleza tutajua hoja zipi za kuzitilia mkazo.
 
Ingekua ni kirahisi hivyo kusingekuwa na maana ya sahihi ya mashaidi ,hyo ndoa ya hvyo inaupenyo wakuiruka kama haina mashaidi na sahihi .
Unairuka sheria ambayo ushahidi wake ni wa watu wanaokuzunguka?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Sheria mbovu ndio mnazozipenda nyinyi wapigaji au sio?
 
Mkuu ata ukioa usifunge ndoa ,kataa ndoa ndoa ni utapel.
Hapo sawa mkuuuu niko pamoja na wew[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hakuna kufunga ndoa ila unakuwa Umeoaaaa. Huu ndo unyamaaa yani. Akikubali inakuwa piaaa shidaa nae anakuwa anazingua anatakaa ndoa ndani amani hakuna
 
Ulitaka nisiwe na upendo kwa mama wa mwanangu eti kisa nimeachana nae ? Ata kma sasa ninaishi na mwingne? Ww ndio haujaelewa apo ninazungzia wanawake wawli single mother na ninae ishi naye.
 
Hahaha nahsi wew ni mdada
Mdada ni jinsia ya KE pia akiwemo, mama ako, Shangazi ako, Bibi ako, Dada ako, Binti ako na huyo Demu wako unaeishi NAE .

Sasa kuwa Mdada ndio nini? Kama kuwa Mdada ni laana wameanza kuifanya hao akiwe mama ako.
 
Mkuu sheria za ndoa ni za kijnga mno , tunachotaka nibadiliko kwnye hizo sheria , tabia za wanawake hubadilika sna unapo funga nao ndoa .
Mabadiliko yatakuwepo vipi wakati wanaume mnakazana kupoteza muda wa mabinti za watu. Unamzalisha mtoto wa mtu akiwa form four alafu hutaki kumuoa, shule alishasimama anashinda analea mtoto. Hasomi shule hana kazi. Wengine mnaenda mbali mnasema mwanamke anaefanya kazi au aliesoma ni feminist so mnataka wa kushinda vibarazani kwasababu ni weak na hawana uwezo wa kudai haki zao. Alafu unakuja huku unasema sheria haikulindi wewe. Nani analipa muda wa huyo binti uliempotezea muda?

Kwanza Nani alikutuma ufungue zipu? Kuweni mapadri ili mali zenu zisiende kwa hao wanawake mnaosema ni wabaya.

Alafu inamaana ndoa zote duniani, chanzo cha matatizo ni mwanamke? Nyie mnaoenda kuzaa nje na kuleta viumbe ndani wanalelewa na huyo mwanamke hamna matatizo? Nyie mnaofanya uhuni huko nje eti kwa kivuli cha uanaume, inamaana ulichukua mwanamke ambae hana moyo akuone unalala na mabaamedi akuchekee tu uje umuue na ukimwi. Ndo maana nawaambia you are selfish. Acha sheria zinawanyooshe na zitawanyoosha kisawa sawa
 
Ulitaka nisiwe na upendo kwa mama wa mwanangu eti kisa nimeachana nae ? Ata kma sasa ninaishi na mwingne? Ww ndio haujaelewa apo ninazungzia wanawake wawli single mother na ninae ishi naye.
Unaeishi NAE unamuitaje ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…