SPACE CADET
JF-Expert Member
- Dec 15, 2022
- 2,280
- 3,555
Kataaa ndoaWee huniambii kitu nikakuelewa,
Ningekuwa sijawahi kuoa hapo sawa,
Mimi nilifunga ndoa kabisa ya kiislamu ila mwanamke alipoanza kunipangia ratiba ya kwichi kwichi (na mimi hii ndo starehe yangu kubwa), baadae akaanza kuniambia nitaondoka mimi yeye nimuachie nyumba akae na watoto (wakati nyumba yenyewe ya kupanga), ikafika kipindi nikawa hata kurudi nyumbani nachukia nikajikuta nafanya kazi masaa kumi na sita,
Mwanamke unaacha kila kitu ndani lakini hapiki badala yake anaenda kununua chipsi anakula na watoto (huyo alikuwa mama wa nyumbani) nilikuwa nampatia kila anachohitaji mwisho wa siku akawa anajisifu kwa watoto wa dada yangu kwa kuwaambia,
"huyo mjomba wenu mwenyewe nampelekesha"
Siku anaamua kuondoka nyumbani yeye mwenyewe akachukua kila kitu na bado narudi kazini nakuta barua kutoka chang'ombe polisi kanifungulia kesi kwamba nimemfukuza, nimemtolea vyombo nje (ninachoshukuru wale kina dada/mama walikuwa ni waelewa) na walijua kwamba yeye ndo mwenye matatizo hivyo walimuuliza tu, "kwa hiyo wewe unatakaje?"
Akajibu, "nahitaji kila mwezi anipe pesa kwa ajili ya watoto" (kimoyo moyo nikajisemea huyu kumbe anataka kuwatumia watoto kama kitega uchumi chake)
Maana kabla hatujaachana nilishawahi kumwambia, "nakupa miezi mitatu fikiria ni biashara gani utakayoweza kufanya ambayo itakuwezesha kuhudumia watoto hata ikitokea siku nimekufa" huwezi amini ilipita miezi mitatu nakuja kumuuliza umefikia wapi, ananijibu l, "sijaona biashara ya kufanya", shiiit
Kifupi huyu mwanamke kuna kipindi nilikuwa naishi nae kwa tahadhari, maana nilikuwa naona kabisa tunapoelekea kuna siku mmoja atamuua mwenzie
Kisha mnajaribu kutushawishi tuoe, aaah weeee... tena kwa sasa hivi wapo na msimamo wao wa 50 kwa 50
Nakwambia, "Niache kidogo"
Ndoa ni kwa wasio na akili