Mjadala kwa wanaokubali kuoa (Ndoa)
Mbona hili nimeshakujibu. Nimekuuliza ww unaweza kukaa na mwanamke asiye haramu yako kwa huo muda bila kumgonga. Tuthibitishie huo ushoga wako? Simple tu . Hayo mengine utajua ww
Nimekujibu kwamba, nikisema tulikuwa na ugomvi kwa kipindi cha miezi mitano kati ya 6 na hivyo hapakuwa na unyumba kati yetu ila tulificha tu ili kulea watoto, utabisha?! Wewe umekaza fuvu ushoga.., jibu hiyo hoja
 
hii ni kampeni ya kujaza watoto wa mitaani, watoto wasiokuwa na mapenz ya baba na mama
 
Nadhani mkuu Tatizo ni kwamba watu wanapangiana. Naamini kila mtu akifanya kile ambacho anaona ni sahihi kwake hakutakuwa na ushindani. Nikimaanisha anayeoa aoe, anayefunga ndoa afunge, asiyetaka aachwe n.k
Yaani hivi vitu vikitofautishwa yaani kuoa na kufunga ndoa, vijana wengi wataoa na familia zitakuwa na amani. Na kijana kama anajielewa hatayumbishwa na kufunga ndoa.
 
Wanawake sikuhizi wengi hawafundwi ipasavyo jinsi ya kumuandaa na kuishi na mwanaume , ndio hayo sasa mtu anaamua kununua gunia la mkaa na kumbanika mke wake , hapo unakuta kavumilia kero na maudhi mpaka basi ,mtu anageuka mnyama
 
Wee huniambii kitu nikakuelewa,

Ningekuwa sijawahi kuoa hapo sawa,

Mimi nilifunga ndoa kabisa ya kiislamu ila mwanamke alipoanza kunipangia ratiba ya kwichi kwichi (na mimi hii ndo starehe yangu kubwa), baadae akaanza kuniambia nitaondoka mimi yeye nimuachie nyumba akae na watoto (wakati nyumba yenyewe ya kupanga), ikafika kipindi nikawa hata kurudi nyumbani nachukia nikajikuta nafanya kazi masaa kumi na sita,
Mwanamke unaacha kila kitu ndani lakini hapiki badala yake anaenda kununua chipsi anakula na watoto (huyo alikuwa mama wa nyumbani) nilikuwa nampatia kila anachohitaji mwisho wa siku akawa anajisifu kwa watoto wa dada yangu kwa kuwaambia,
"huyo mjomba wenu mwenyewe nampelekesha"

Siku anaamua kuondoka nyumbani yeye mwenyewe akachukua kila kitu na bado narudi kazini nakuta barua kutoka chang'ombe polisi kanifungulia kesi kwamba nimemfukuza, nimemtolea vyombo nje (ninachoshukuru wale kina dada/mama walikuwa ni waelewa) na walijua kwamba yeye ndo mwenye matatizo hivyo walimuuliza tu, "kwa hiyo wewe unatakaje?"

Akajibu, "nahitaji kila mwezi anipe pesa kwa ajili ya watoto" (kimoyo moyo nikajisemea huyu kumbe anataka kuwatumia watoto kama kitega uchumi chake)
Maana kabla hatujaachana nilishawahi kumwambia, "nakupa miezi mitatu fikiria ni biashara gani utakayoweza kufanya ambayo itakuwezesha kuhudumia watoto hata ikitokea siku nimekufa" huwezi amini ilipita miezi mitatu nakuja kumuuliza umefikia wapi, ananijibu l, "sijaona biashara ya kufanya", shiiit


Kifupi huyu mwanamke kuna kipindi nilikuwa naishi nae kwa tahadhari, maana nilikuwa naona kabisa tunapoelekea kuna siku mmoja atamuua mwenzie


Kisha mnajaribu kutushawishi tuoe, aaah weeee... tena kwa sasa hivi wapo na msimamo wao wa 50 kwa 50

Nakwambia, "Niache kidogo"
kiongozi kwaiyo utafiti wako unaotuoatia apa kumbe ni kwa mwanamke mmoja, kelele zote kumbe ni ako kadem kamoja mmeokotana kwenye vigodoro alaf unamchumbia, dem anayejitambua hawezi kuwa ivyo. jaribu mwingine mkuu achana na mawazo ayo
 
Sawa, tufanye sio kahaba, jibu sasa hoja kwenye post yangu namba 560
Asingekuwa Kahaba usingenifuma nae huyo mama watoto wako.
Okay tufanye sio Kahaba ila umenifuma NAE huyo mama watoto wako na ukamsusa na mm nikamuacha baada ya kupata nilichotaka napata shida Gani ?

Hilo a na b yake, kwani tofauti ya ki haki na kisheria unazozipata ww usie na Cheti ni zipi zinazotofautisha na alie na Cheti.

Maana kama kuacha alie na Cheti na asie na Cheti wote wanaweza kuacha na kitakachompata asie na Cheti nd kilekile kitachompata alie na Cheti .
 
Unataka kumuoa mtu mwenye Talaka sita

Mimi nilimuoa nikamuacha, akaolewa tena akadumu kwenye ndoa mwaka mmoja akaachika tena

Kwa hiyo wanaume wote wawili tumemshindwa ila wewe utamuweza

Njoo PM nikuunganishe nae ila kaa ukijua ana watoto wangu
We kama ulishindwa, wenzio tunaweza, mlete huyo mkeo tumuoe
 
Tofautisha kuoa na kufunga ndoa, hawakatai kuoa, wanakataa ndoa
Nimekwambia

Ndoa ni nomino.
Kuoa ni kitenzi.

Kama kusinzia na usingizi. Et usinzie alafu ukasema Sina usingizi.


Kataa Sheria Mbovu za ndoa lakini kutaa ndoa sio kweli. Maana wengine mna ndoa na hamjui kama mmeoa.
 
Daah sijui ntakuwa nimeelewa tofauti? Naona kama mtoa mada “umeiview ndoa from the point of having sex” tu. Sijui lakini?
 
Huoi ila utaishi na mwanamke? Ama huoi na hauishi nyumba moja na mwanamke? ama huoi na hauhitaji mwanamke kwa chochote?
Sioi ila wanawake nnao na wananiburudisha vizuri tu. Naweza kuishi na mwanamke ila siwezi kufunga ndoa.
 
Saivi ukioa unakaa mwaka mmoja wa amani wa pili na kuendelea ni machafuko ya amani
 
NILICHOKIBAINI JUU YA CAMPAIGN YA KATAA NDOA

Ndugu wanajamvi amani iwe juu yenu!

Poleni na harakati zote za siku nzima na kwa wale ambao kwamba wameshatoka katika harakati Na majukumu yao kwa siku ya Leo na kwa wale ambao bado wapo harakati Na majukumu basi mwenyezi mungu awatilie wepesi muyamalize salama salmin

Naiona weekend ambayo imebeba hisia nyingi sana za mashabiki wa mpira wa miguu tukiwa tunafungua mapuziko ya weekend na watoto watoto wa kariakoo wekundu wa msimbazi simba nguvu moja dhidi ya Raja Casablanca huku tukimaliza mapumziko yetu ya weekend siku ya jumapili na watoto wa jangwani wananchi dhidi ya TP mazembe wa Congo hatujui nani atafurahi nani atalala na viatu ama wafurahi wote kwa pamoja au walie wote..what a weekend!

Ama baada ya utangulizi huo ningependa moja kwa moja niende kwenye maudhui ya thread yangu!

Kumekuwa na wimbi kubwa sana la kampeni kataa ndoa katika mtandao wetu huu wa jf kwa masiku ya hivi karibuni kuanzia mwaka Jana hadi hivi sasa ninavyoandika andiko hili takwimu zaonesha ni kama haupiti mwezi isipokuwa kumeanzishwa thread ya namna hiyo!

Na katika kila thread ambayo kwamba imeanzishwa kuhusu operation kataa ndoa
Ndoa ni utapeli
Ndoa ni wizi
Ndoa ni ujambazi
Ndoa ni mradi wa mwanamke
Ndoa ni jela
Ndoa ni kufa mapema kwa mwanaume
Ndoa ni stress huwa Mara nyingi katika thread kwa mizani yangu Mara nyingi ambao wanasapoti kampeni kataa ndoa huwa wanakuwa wengi au Mara nyingine hoja zao wanazozitoa huwa hawapatiwi majibu yanayowatosheleza hivyo Mara nyingi thread huwa inaisha bila muafaka au hats kwa kutazama ukaona kuwa ni pande ipi imetoa hoja nzito na hazikupata mwenye kukinzana nazo kwa hoja.

Nini Mimi nimekibaini na kukileta kwenu?

Binafsi sjaja na majibu ya kuwashauri watu wanao kataa ndoa ili waone kuwa wapo katika nje ya mstari warudi njia kuu japo tunashukuru kuna baadhi ya watu kama vile Mshana Jr ameshakuja na thread ya kujaribu kudadavua sababu ambazo zawapelekea wengi kufika hatua hiyo ya kataa ndoa....

Mwenyezi mungu amtie nguvu sasa wake kina mshana Jr na wengine Na namna sasa ya kuwa council na kuwatibu kisaikolojia namna ya kuwatoa huko na kuwaleta njia juu.

Nilichokibaini Mimi na pia kikanitisha sana ni kuwa nilikuwa naamnini hizi campaign za kataa ndoa zipo jamiiforums pekee yake au kwenye mitandao ya kijamii pekee yake ila kiuhalisia mtaani ni vijana wachache wenye mindset hizo kama nilivyozoea sometimes ukiingia kule Twitter unaweza hisi dunia inaisha kesho na kesho ni WW III au ukahisi Tanzania kesho watu wote wanaingia barabarani kudai mambo yao muhimu ya kikatiba ila ukija mtaani kwenye uhalisia unawakuta watu wapo bize na majukumu yao kila siku hata hawana habari Na wengi katika wao they even don't know what's trending at the moment!

Hivyo nilikuwa naamini kadhalika hii kampeni ya kataa ndoa ni kama issue za Twitter au BBC na baadhi ya vyombo vya habari vya magharibi vinavyo exaggerate mambo mambo unajawa upepo hapa Africa kufika mwezi wa tano maiti za corona victims zitakuwa mitaroni na mabarabarani kumbe laa! Ni kweli but too exaggerated! Basi kumbe kwenye kampeni ya kataa ndoa sehemu kubwa ya vijana wa kike kwa kiume ni kweli imekwisha athirika na jambo kama hili sababu zinaweza zikawa kama vile alizo zitoa japokuwa alijikita sana kwa wanaume ila hili wimbi pia naliaona hata kwa wanawake wanaojiita hustlers tayari wengi katika wao wapo kwenye wimbi hili.

Naandika hivi na kusema kuwa nimebaini ni baada ya kuongea na vijana wengi wa like kwa wa kiume ana kwa ana katika maongezi ya kawaida wengi katika wao wanapinga ndoa vikali na wengi katika wao ni wale town hustlers.... Japokuwa wote niliongea nao ni watu wa mjini sjajua watu kutoka vijijini wao wameathirika au laa! Na nilikuwa naongea nao kwa namna ambayo kwamba ni maongezi ya kwawaida ya stori Paso nawao kujua nafanya data collection by observing!

Hivyo nichukue fursa hii kuwaomba wanajamvi na wataalam wa issue za kijamii za hizi waje na hoja nzuri na nzito za kujaribu kuwanusua vijana kutoka kwenye wimbi hilo... Wengi wamekuja na sababu zinazowapelekea huko, sasa waje na majibu ya kuwatoa huko.

Naomba kuwasilisha!
 
Back
Top Bottom