NILICHOKIBAINI JUU YA CAMPAIGN YA KATAA NDOA
Ndugu wanajamvi amani iwe juu yenu!
Poleni na harakati zote za siku nzima na kwa wale ambao kwamba wameshatoka katika harakati Na majukumu yao kwa siku ya Leo na kwa wale ambao bado wapo harakati Na majukumu basi mwenyezi mungu awatilie wepesi muyamalize salama salmin
Naiona weekend ambayo imebeba hisia nyingi sana za mashabiki wa mpira wa miguu tukiwa tunafungua mapuziko ya weekend na watoto watoto wa kariakoo wekundu wa msimbazi simba nguvu moja dhidi ya Raja Casablanca huku tukimaliza mapumziko yetu ya weekend siku ya jumapili na watoto wa jangwani wananchi dhidi ya TP mazembe wa Congo hatujui nani atafurahi nani atalala na viatu ama wafurahi wote kwa pamoja au walie wote..what a weekend!
Ama baada ya utangulizi huo ningependa moja kwa moja niende kwenye maudhui ya thread yangu!
Kumekuwa na wimbi kubwa sana la kampeni kataa ndoa katika mtandao wetu huu wa jf kwa masiku ya hivi karibuni kuanzia mwaka Jana hadi hivi sasa ninavyoandika andiko hili takwimu zaonesha ni kama haupiti mwezi isipokuwa kumeanzishwa thread ya namna hiyo!
Na katika kila thread ambayo kwamba imeanzishwa kuhusu operation kataa ndoa
Ndoa ni utapeli
Ndoa ni wizi
Ndoa ni ujambazi
Ndoa ni mradi wa mwanamke
Ndoa ni jela
Ndoa ni kufa mapema kwa mwanaume
Ndoa ni stress huwa Mara nyingi katika thread kwa mizani yangu Mara nyingi ambao wanasapoti kampeni kataa ndoa huwa wanakuwa wengi au Mara nyingine hoja zao wanazozitoa huwa hawapatiwi majibu yanayowatosheleza hivyo Mara nyingi thread huwa inaisha bila muafaka au hats kwa kutazama ukaona kuwa ni pande ipi imetoa hoja nzito na hazikupata mwenye kukinzana nazo kwa hoja.
Nini Mimi nimekibaini na kukileta kwenu?
Binafsi sjaja na majibu ya kuwashauri watu wanao kataa ndoa ili waone kuwa wapo katika nje ya mstari warudi njia kuu japo tunashukuru kuna baadhi ya watu kama vile
Mshana Jr ameshakuja na thread ya kujaribu kudadavua sababu ambazo zawapelekea wengi kufika hatua hiyo ya kataa ndoa....
Mwenyezi mungu amtie nguvu sasa wake kina mshana Jr na wengine Na namna sasa ya kuwa council na kuwatibu kisaikolojia namna ya kuwatoa huko na kuwaleta njia juu.
Nilichokibaini Mimi na pia kikanitisha sana ni kuwa nilikuwa naamnini hizi campaign za kataa ndoa zipo jamiiforums pekee yake au kwenye mitandao ya kijamii pekee yake ila kiuhalisia mtaani ni vijana wachache wenye mindset hizo kama nilivyozoea sometimes ukiingia kule Twitter unaweza hisi dunia inaisha kesho na kesho ni WW III au ukahisi Tanzania kesho watu wote wanaingia barabarani kudai mambo yao muhimu ya kikatiba ila ukija mtaani kwenye uhalisia unawakuta watu wapo bize na majukumu yao kila siku hata hawana habari Na wengi katika wao they even don't know what's trending at the moment!
Hivyo nilikuwa naamini kadhalika hii kampeni ya kataa ndoa ni kama issue za Twitter au BBC na baadhi ya vyombo vya habari vya magharibi vinavyo exaggerate mambo mambo unajawa upepo hapa Africa kufika mwezi wa tano maiti za corona victims zitakuwa mitaroni na mabarabarani kumbe laa! Ni kweli but too exaggerated! Basi kumbe kwenye kampeni ya kataa ndoa sehemu kubwa ya vijana wa kike kwa kiume ni kweli imekwisha athirika na jambo kama hili sababu zinaweza zikawa kama vile alizo zitoa japokuwa alijikita sana kwa wanaume ila hili wimbi pia naliaona hata kwa wanawake wanaojiita hustlers tayari wengi katika wao wapo kwenye wimbi hili.
Naandika hivi na kusema kuwa nimebaini ni baada ya kuongea na vijana wengi wa like kwa wa kiume ana kwa ana katika maongezi ya kawaida wengi katika wao wanapinga ndoa vikali na wengi katika wao ni wale town hustlers.... Japokuwa wote niliongea nao ni watu wa mjini sjajua watu kutoka vijijini wao wameathirika au laa! Na nilikuwa naongea nao kwa namna ambayo kwamba ni maongezi ya kwawaida ya stori Paso nawao kujua nafanya data collection by observing!
Hivyo nichukue fursa hii kuwaomba wanajamvi na wataalam wa issue za kijamii za hizi waje na hoja nzuri na nzito za kujaribu kuwanusua vijana kutoka kwenye wimbi hilo... Wengi wamekuja na sababu zinazowapelekea huko, sasa waje na majibu ya kuwatoa huko.
Naomba kuwasilisha!