Binafsi huwa naamini katika Imani Baina ya Mtu Binafsi na anachoamini kwa Mungu; Mlengo wa madhehebu umekuja ili kutupa Mwanga; baada ya hapo Mtu binafsi anatakiwa awe na Jitihada Binafsi za kumtafuta MUNGU yaan kibinafsi kabisa, na si tena kwa Mlengo wa Kidhehebu; Of which ukishafika hizo Level ukiwa kanisa lolote still hutaweza Fanya Baadhi ya Vitu kwa kufuata Mkumbo na hili linawezekana.
Binafsi nimeona tofauti sana, Ulaya na Huko Africa Especially Nyumbani Tz, Ulaya Issue za Imani huwa zinachukuliwa Personal zaid ya kuchukulia kwa mlengo wa Kundi; Hivyo ni rahisi kuona mtu wa Ulaya anafanya jambo lake kwa namna alivyoelewa yeye si kwa namna ya Mlengo wa kanisa lake.
Mfano: Baadhi ya makanisa Kuna maji unachovya Mkono na Unapiga ishara ya Msalaba; Sasa wako ambao kwa sababu zao wao hawachovyi kwasababu zao binafsi, Ijapokuwa Mlengo wa dini imeruhusu hichi kitu.
Sasa kwa wazungu kwasaababu wao hawana mambo ya Kutenga, Ila Tz nadhani watu wanaongopa mambo ya kutengwa,
Lakini pia nilishakuwa na mwaamini mmoja rafiki yangu tulikuwa tunafanya naye workshop moja, yeye binafsi ni High church Anglican Sala ya Salamu maria haikubali, Hivyo inapofika kuisema yeye hasemi anakausha tu au anafanya maombi yake binafsi, Jamaa alinifungua mambo mengi sana kuhusu Imani, alinisaidia sana.
Muhimu ni wewe kufahamu MUNGU binafsi, pia ninachoamini Mungu anatufahamu kuwa sisi tu Viumbe dhaifu, na tena Tumepungukiwa na utukufu wake, Hivyo hatuwezi sisi kujifanya kuweka taratibu nzuri za ibada, utaratibu fulani wa kusema sala kana kwamba Mungu ndio atakuwa kwenye Mlengo wetu, no Mungu haangalii Mlengo mungu ataangalia Mtu mmoja mmoja, Hivyo tujitahidi kusoma Vitu vingi zaidi, pia usijiwekee mipaka soma Biblia lakini pia soma Vitabu vya kihistoria,
Kuumbuka kwamba hata baadhi ya waandishi wa bile walisema kwamba waliandika mambo machache sio kila kitu kiliandikwa maana isingetosha, sasa kwa nini usisome zaidi? tena kama mtu anayetafuta maarifa, kwanini usiwe na biblia zote mbili? kwanini utenge biblia za mlengo fulani, je ni kweli unahitaji kufahamu mambo?
Kama imani ni suala binafsi kwanini wewe usiwe na bible yako yenye vitabu vingi zadi hata nyumbani kwako ukawa unajisomea? yaan kwasababu Mlengo wa dhehebu lako hawatumii na wewe usitumie? Africa kuna tatizo mahali, lakini naamini ni suala la Muda tu, mambo yatakaa sawa; maana watu wanapata expsure taratibu.
Ukiweza hayo mambo hutapata shida na dhehebu la mtu, ama taratibu zo namna wanavyosali/swali kwenye Hekali zao/ Sinagogi/misikiti yao;
Lakini kitu kingine ambacho mimi huwa naamini ni kwamba Moja wapo ya Vitu amabvyo Yesu alisisitiza ni UPENDO, na akasema kwamba Amri ya kwanza ni Kumpenda Mungu kwa Moyo wako wote,akili na Roho na ya pili akasema ni Kumpenda jirani yako kama nafsi yako; Ukiangali kwa karibu zaidi Hakuna Mlengo wa Dini ambayo inapinga UPENDO au haihubiri Upendo ( Achilia mbali watu amabao kwa itikadi zao binafsi wanafanya mauaji/ vurugu kwa mwamvuli wa dini etc, nazungumzia Msimamo wa hiyo dini katika ujumla wake) Maana kama ni vurugu wapo watu katika Christianity, Muslim, Budhist etc huwa wanafanya vurugu, lakini sio dini yao ni wao binafsi wanakuwa wamekengeuka.
Ni muhimu sana Kuheshimu Taratibu za watuwengine, na si kutoa maneno ya kashfa na yasiyofaa kuhusu taratibu zao; Infact sisi sote haya mambo tumepokea kutoka mahali, na kama ujuavyo kupokea kitu toka mahali mpaka kikufikie wewe ni nadra sana kukipata kama kilivyo.
Hata tu story tu za habari za cnn,bbc etc, the same information inakuwa reported tofauti kwa sababu mbalimbali, na ikitokea imekuwa the same tegemea kuwepo kwa tofauti kwa wapokeaji wa taarifa hiyo, kila mtu ataelewa kwa namna yake mwenyewe, naye anaweza kuelezea kwa namna alivyoelewa.
Last kabisa, Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi, ikumbukwe kwamba Vitabu hivyo viliandikwa Enzi hizo (Karne nyingi zilizopita) Si sawa kuleta tafsiri ya Moja kwa moja kwenye kipindi chetu hichi.
Ukiona kwenye biblia wanasema Farao alikuwa na magari na jeshi kubwa, lazima ufahamu gari hazikuwa kama izi za leo; ndio maana nikasema ukisoma Bible peke yake unaweza ukamiss baadh ya vitu, ndio maana ni vizuri kusoma vitabu vingine pia ili uongeze maarifa (Mimi naamini hata kama vitabu visingetolewa, bado isingewezekana kuandikwa kila kitu, hivyo kwa mtazamo wangu binafsi sioni tatizo sana, bado naweza tumia hivyo vilivyopo)