MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Lukome, Mkuu unaonekana kuandika kwa hekima sana, na tunakuombea uujue ukweli mapema ili nia yako nzuri hii isiishie kupotoshwa kwa kutolijua neno la mungu vizuri. Kiukweli, hakuna mahali popote katika biblia ambapo awe mtu ama yesu mwenyewe ambapo amesema tukitaka kuomba tufanye hivyo kupitia kwa mama maria.

Yesu mwenyewe anasema; mm ndimi njia, tena ya kweli. Yoyote atakayefika kwa baba lazima apitie kwangu na hakuna njia nyingine. Hapa hakuna sehemu anakosema maombi yapitie kwa mama yake then yaje kwake. Kumbuka pia mistari hii; ombeni lolote kwa jina langu, nanyi mtapata. Hakusema tuombe kwa jina la maria. Kosa lingine tunalofanya ni kumuita maria mama wa Mungu. Kumbu Mungu hana mama, tuna Mungu baba, Mungu mwana na Mungu roho mtakatifu.

Hakuna popote ambapo maria ametajwa kuwa sehemu ya Mungu, kumpa maria sifa ya uungu ni kosa kubwa, na biblia inaeleza jinsi Mungu alivyo na wivu kwa wale wanaoabudu mtu mwingine kwa jina lake zaidi ya yeye Mungu.
 
Wewe unayaelewa...??? Nani kwambia mimi siyaelewi...???

Hebu nifuatilie toka mwanzo naona umekuja kwa kasi sana...
Kama wayaelewa kweli hebu tufumbulie na utuhusianishie mwanamke huyo wa kimaono na Maria. Tujuze pia atawezaje kuvikwa jua halafu chini mwezi. Hebu tupe maana hata Catholic Mary huwa baadhi ya picha kazungushiwa nyota sawa sawa na nyota zilizoko kwenye bendera ya E.U (Europa)
 
Kama wayaelewa kweli hebu tufumbulie na utuhusianishie mwanamke huyo wa kimaono na Maria. Tujuze pia atawezaje kuvikwa jua halafu chini mwezi. Hebu tupe maana hata Catholic Mary huwa baadhi ya picha kazungushiwa nyota sawa sawa na nyota zilizoko kwenye bendera ya E.U (Europa)
Akikujibu hili swali mimi ntahama nchi 😂
 
Utuombee sisi wakosefu... Tatizo nyie mwajifanya watakatifu
Jamani nyinyi wakatoliki vipofu wa kiroho Yesu hakuacha secretary ambaye cc twapaswa kupitia kwake ili sasa yeye apeleke maomb yetu kwa Yesu.....Yesu kwa uwazi kabisa alisema lolote muombalo kwa jina langu mtapewa.....huyo maria ni marehemu anaesubiri siku ya mwsho kama ilivyo kwa wengine mmeng'ang'ana na fundisho la haruc ya kana ilhali baada ya hapo Yesu kuna mengi tu aliyafanya pasipokuombwa na mama yake rejea ile habar yakuwalisha maelfu samaki na mikate jeeee kuna mtu alimwendea mama yake ili awaombee kwa mwanaye
 
cilla,
MKUU NIMEPENDA SANA JINSI ULIVYOTOA SOMO KUHUSU UZUSHI WA HIVYO VITABU 7.....MUNGU AKUHIFADHI UZID KUTUTOA TONGOTONGO SISI WAABUDU PAPA,WASALI ROZALI NA WAABUDU SANAMU LA BIKIRA MARIA.
 
Deogratius Kisandu,
Yaliyotokea yalitokea.. sisi kama Waafrica hayo hayatuhusu hata kidogo. Yanatuhusu labda kwa ujinga wetu, maana tunafuata falsafa za wenzetu ambazo zimekaa dhidi yetu.

Sisi yatupasa tujiulize maswali ya msingi kama vile
1. Kwa nini tulitwaliwa utumwa kwa miaka zaidi ya 300 na hatukujitetea?
2. Kwa nini na kivipi hatuna dini yetu rasmi kama watu wa Africa?
3. Inakuwa vipi hatuna lugha rasmi kama waafrica ambayo ingetumika kuhifadhi historia yetu?

4. Ni kweli kwamba waafrica hawakuchangia chochote katika historia na ustaarabu wa dunia?

5. Kwa nini hata baada ya maendeleo makubwa yaliyopo duniani, bado waafrica ni watu duni kabisa katika kila aspect?
6. Kwa nini hatuna cargo za kuuza nchi za nje? Kwa maana hatuna bidhaa za kuuza kwa wenzetu kama tunavyonunua kutoka kwao? Namaanisha kwa nini hata hatutengenezi nguo tukawauzie wao?
7. Inakuwa vipi hatuna falsafa katika utawala, uongozi na maendeleo?
8. Kwa nini mahusiano yetu yameshikiliwa na ukabila, ukoo, undugu badala ya uweledi, ujuzi na fursa?
9. Kwa nini bado waafrica hatuthamini maisha? Kwamba mtu anaweza akatekwa tu na akauawa na serikali au majambazi na tukachukulia powa?
10. Kwa nini watanzania waruhusu kuendelea kutawaliwa na ccm japokuwa wanafaham kuwa hakuna faida wala manufaa ya kuwepo hilo li chama?

Ni hayo tu kwa leo.. story za kina Luther zibaki tu kutukumbusha kuwa wao walikuwa na maswali, yalipokosa majibu wakaamua kufanya walivyofanya na matokeo yao waliifanya nchi yao kuwa mahala safi kwa kuishi vizazi vyao. Sisi siyo muafaka kuhoji kuondolewa vitabu kwenye bible, bali kuhoji vitu vinavyitugusa moja kwa moja
 
Kuna sababu kadhaa ambazo waisraeli walivikataa vitabu ambavyo ndivyo badae waprotestanti hawakuviweka katika biblia yao kama walivyo nayo leo ikiwa na vitabu 66 na wakatoliki ikiwa na vitabu 72.

Sababu ya kwanza waisraeli walikubali na kukipokea kitabu katika biblia yao pale tu kilippkuwa na uhusiano was moja kwa moja na Musa. Vitabu vingine vile ambavyo havikuwa na uhusiano na Musa havikukubalika.

Sababu ya pili wasraeli walikipokea na kukikubali kitabu katika biblia yao kama tu kimeandikwa na muyahudi. Vitabu ambavyo havikuandikwa na wayahidi havikupokelewa katika biblia ya kiyahudi.

Sababu ya tatu, kitabu kilikubaliwa na kupokelewa katika biblia ya wayahusi kama tu kina uhusiano wa moja kwa moja na Manabii. Vitabu ambavyo havikuhusiana na manabii havikupokelewa katika biblia ya kiyahudi.

Hivyo, ukiviangalia hivyo vitabu vilivyokataliwa na wayahudi na badae waprotestanti havina sifa hizo nilizozibainisha hapo juu.
 
Kwa nini tulitwaliwa utumwa kwa miaka zaidi ya 300 na hatukujitetea?
2. Kwa nini na kivipi hatuna dini yetu rasmi kama watu wa Africa?
3. Inakuwa vipi hatuna lugha rasmi kama waafrica ambayo ingetumika kuhifadhi historia yetu?
Una uhakika kwamba wewe ni mwafrika? Pia, una hakika kwamba wewe asili yako ni Afrika? Lakini, je unaweza kuthibitisha kwamba matatizo ya wafrika ni kwasababu ya kutokuwa na dini yao? Na kama ni hivyo, hiyo dini ya waafrika mwanzilishi wake ni nani?
 
Nundu_Tanzania,
Acha kupotosha mkuu
Ungefanya kuongeza maarifa kwanza kufaham historia ya biblia na dini kwa ujumla wake.
Wayahudi unaowaongelea ni kwamba wakati biblia inaandikwa walishasambaratishwa na wavamizi. Labda kama unaongelea Wayahudi bandia tunsowaona sasa. Vile vitabu vilikusanywa kutoka maeneo ambako wamiliki walikuwa wameteketezwa katika genocide vikapelekwa Alexandria (Misri) ili kutafsiriwa katika lugha ya kiyunani (kigiriki). Katika kazi hiyo kuna mambo yaliachwa na mambo mapya yakaingizwa. Kimsingi lengo lilikuwa ni kuhifadhi nyaraka nyeti za kihistoria katika maktaba ya Mfalme wa Rumi.

Kuhusu Luther, ni vizuri kufaham vema kuhusu Holy Roman Empire, ambayo kwa kiwango kikubwa wakuu wake walikuwa watu wasio albino (blacks).. na zaidi biblia ilikuwa na mambo ya wazi ikionesha ni kina nani haswa (kabila zao na rangi zao) ilikuwa inahusu. Huyu padre Luther na baadaye kina Calvin waliamua kujenga hoja si kwamba mambo yaliyopingwa yalikuwa na shida sana, bali ni kwamba Roma ya wakati ule na tokea kuanzishwa kwake ilikiwa imeshikiliwa na watu wa rangi. Kwa hiyo yeye akiwa mzungu (albino) akaona si vema akaendelea kutukuza mtu mweusi. Vuguvugu lao lilikuwa lina protest baadhi ya mila, mafundisho na utamaduni wa kanisa la Rumi chini ya holy roman empire ya wakati huo. Miaka 150 baada ya luther ku protest, biblia ilichakachuliwa tena na kutengeneza inayotumika kwa wingi na mahali pengi, ilikuja kujulikana kama King James Version.

Hii sasa ndiyo bible ya albino aka wazungu. Ikiwa imetupilia mbali vitabu vyote vyenye dalili ya kuhusisha dini ya kikristo na watu weusi..

Kwenye picha.. ya kwanza inaonesha wayahudi wa Asili walivyofanana

Ya pili inaonesha Pontiff Benedict 16 na aliyemrithi wakisali mbele ya black maddona. Kuonesha kuwa kanisa la Rumi msingi wake ulitokana na watu weusi. Mzungu Luther hakupenda kuona haya yakiendelea (kuwasujudia watu weusi) ndo maana akaanzisha tifutifu.. akisingizia kuwa Papa hana haki wala malaka ya kusamehe dhambi.. Hii hoja huenda ilikuwa kweli lakini kulikuwa na zaidi ambayo Luther hakuyaweka wazi.

Nawasilisha
Church_8.jpg
Brit_91.jpg
 
Wakuu mbona mnabishanana sana wakati wazungu walioleta dini/ madhehebu hayo wakila bata na kupiga hatua za maendeleo kila kukicha?, cha msingi Naona kila mtu abaki na iman yake kukosoana na kutokwa na mapovu namna hii utadhan tulikuwepo wakati biblia inaandikwa hakuna maana. Kila mmoja asidharau iman ya mingine na hakuna aliye bora kuliko mwenzake as long as wote mmeumbwa kwa mf na sura ya Mungu
Ndio nashangaa vitabu vya Mungu, vinafutwa na mtu!!
 
Articles full of gestures.. Unavyosema Luther na wenzake walitaka piga hela kiurahisi, wenzake wapi? Walitaka kupigaje? Je Lurher alikuwa maskini? No research No right to speak brother.
 
Binafsi huwa naamini katika Imani Baina ya Mtu Binafsi na anachoamini kwa Mungu; Mlengo wa madhehebu umekuja ili kutupa Mwanga; baada ya hapo Mtu binafsi anatakiwa awe na Jitihada Binafsi za kumtafuta MUNGU yaan kibinafsi kabisa, na si tena kwa Mlengo wa Kidhehebu; Of which ukishafika hizo Level ukiwa kanisa lolote still hutaweza Fanya Baadhi ya Vitu kwa kufuata Mkumbo na hili linawezekana.

Binafsi nimeona tofauti sana, Ulaya na Huko Africa Especially Nyumbani Tz, Ulaya Issue za Imani huwa zinachukuliwa Personal zaid ya kuchukulia kwa mlengo wa Kundi; Hivyo ni rahisi kuona mtu wa Ulaya anafanya jambo lake kwa namna alivyoelewa yeye si kwa namna ya Mlengo wa kanisa lake.

Mfano: Baadhi ya makanisa Kuna maji unachovya Mkono na Unapiga ishara ya Msalaba; Sasa wako ambao kwa sababu zao wao hawachovyi kwasababu zao binafsi, Ijapokuwa Mlengo wa dini imeruhusu hichi kitu.

Sasa kwa wazungu kwasaababu wao hawana mambo ya Kutenga, Ila Tz nadhani watu wanaongopa mambo ya kutengwa,

Lakini pia nilishakuwa na mwaamini mmoja rafiki yangu tulikuwa tunafanya naye workshop moja, yeye binafsi ni High church Anglican Sala ya Salamu maria haikubali, Hivyo inapofika kuisema yeye hasemi anakausha tu au anafanya maombi yake binafsi, Jamaa alinifungua mambo mengi sana kuhusu Imani, alinisaidia sana.

Muhimu ni wewe kufahamu MUNGU binafsi, pia ninachoamini Mungu anatufahamu kuwa sisi tu Viumbe dhaifu, na tena Tumepungukiwa na utukufu wake, Hivyo hatuwezi sisi kujifanya kuweka taratibu nzuri za ibada, utaratibu fulani wa kusema sala kana kwamba Mungu ndio atakuwa kwenye Mlengo wetu, no Mungu haangalii Mlengo mungu ataangalia Mtu mmoja mmoja, Hivyo tujitahidi kusoma Vitu vingi zaidi, pia usijiwekee mipaka soma Biblia lakini pia soma Vitabu vya kihistoria,

Kuumbuka kwamba hata baadhi ya waandishi wa bile walisema kwamba waliandika mambo machache sio kila kitu kiliandikwa maana isingetosha, sasa kwa nini usisome zaidi? tena kama mtu anayetafuta maarifa, kwanini usiwe na biblia zote mbili? kwanini utenge biblia za mlengo fulani, je ni kweli unahitaji kufahamu mambo?

Kama imani ni suala binafsi kwanini wewe usiwe na bible yako yenye vitabu vingi zadi hata nyumbani kwako ukawa unajisomea? yaan kwasababu Mlengo wa dhehebu lako hawatumii na wewe usitumie? Africa kuna tatizo mahali, lakini naamini ni suala la Muda tu, mambo yatakaa sawa; maana watu wanapata expsure taratibu.

Ukiweza hayo mambo hutapata shida na dhehebu la mtu, ama taratibu zo namna wanavyosali/swali kwenye Hekali zao/ Sinagogi/misikiti yao;

Lakini kitu kingine ambacho mimi huwa naamini ni kwamba Moja wapo ya Vitu amabvyo Yesu alisisitiza ni UPENDO, na akasema kwamba Amri ya kwanza ni Kumpenda Mungu kwa Moyo wako wote,akili na Roho na ya pili akasema ni Kumpenda jirani yako kama nafsi yako; Ukiangali kwa karibu zaidi Hakuna Mlengo wa Dini ambayo inapinga UPENDO au haihubiri Upendo ( Achilia mbali watu amabao kwa itikadi zao binafsi wanafanya mauaji/ vurugu kwa mwamvuli wa dini etc, nazungumzia Msimamo wa hiyo dini katika ujumla wake) Maana kama ni vurugu wapo watu katika Christianity, Muslim, Budhist etc huwa wanafanya vurugu, lakini sio dini yao ni wao binafsi wanakuwa wamekengeuka.

Ni muhimu sana Kuheshimu Taratibu za watuwengine, na si kutoa maneno ya kashfa na yasiyofaa kuhusu taratibu zao; Infact sisi sote haya mambo tumepokea kutoka mahali, na kama ujuavyo kupokea kitu toka mahali mpaka kikufikie wewe ni nadra sana kukipata kama kilivyo.
Hata tu story tu za habari za cnn,bbc etc, the same information inakuwa reported tofauti kwa sababu mbalimbali, na ikitokea imekuwa the same tegemea kuwepo kwa tofauti kwa wapokeaji wa taarifa hiyo, kila mtu ataelewa kwa namna yake mwenyewe, naye anaweza kuelezea kwa namna alivyoelewa.

Last kabisa, Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi, ikumbukwe kwamba Vitabu hivyo viliandikwa Enzi hizo (Karne nyingi zilizopita) Si sawa kuleta tafsiri ya Moja kwa moja kwenye kipindi chetu hichi.
Ukiona kwenye biblia wanasema Farao alikuwa na magari na jeshi kubwa, lazima ufahamu gari hazikuwa kama izi za leo; ndio maana nikasema ukisoma Bible peke yake unaweza ukamiss baadh ya vitu, ndio maana ni vizuri kusoma vitabu vingine pia ili uongeze maarifa (Mimi naamini hata kama vitabu visingetolewa, bado isingewezekana kuandikwa kila kitu, hivyo kwa mtazamo wangu binafsi sioni tatizo sana, bado naweza tumia hivyo vilivyopo)
 
Back
Top Bottom