Hata kama tukikataa kuwa biblia si mali ya kanisa katoliki tutakuwa tunadanganya,kumbuka mpaka unafahamu Martin luther ni kwa sababu alifuzu mafundisho ya kanisa na akawekwa wakfu kuwa Padri,na ndio maana hata alikokwenda aliweza kumudu kuwalisha watu neno la MUNGU kutokana na falsafa na teologia ambayo alikuwa tayari anayo kichwani kumbuka binadamu huendeshwa na wakati Martin Luther alikuwa na nia njema tu ambayo haikuendana na wakati aliokuwa nao yawezekana labda angekuwa flexible na kuyachukulia haya yote kwa upole kama Padre yawezekana kanisa lingechota mambo mengi sana kutoka kwake.
Tukumbuke kanisa limepita katika misukosuko miingi sana si rahisi kila kitu kwamba kanisa lingekifanya kiusahihi,hata leo kanisa linafanya sinodi mbalimbali ili kulipyaisha kanisa kulingana na mahitaji ya wakati husika.Kuanzisha kanisa si suluhisho bali ni kuwanyima watu ukweli ulio mpana zaidi ambao wanastahili kuujua kama waamini.
Tumuombe MUNGU atujalie umoja wa kanisa na kudumisha undugu kama wana wa baba mmoja na chini ya mkombozi mmoja YESU KRISTU BWANA WETU.