Du! Pastor kwa kweli umeniwahi kwa kuuliza hili swali. Nami siku za nyuma nmekuwa nkijiuliza swali hili hili.
Siku moja nlijaribu kuuliza hili swali nkapewa jibu lisilo ridhisha nkasema ningekuja kulileta hapa ili tuweze kujua nn chanzo hasa.
Jibu nlilopewa ambalo sikuridhika nalo ni "Jamaa nliyemuuliza hili suala alinambia kuwa, kutokana na sababu za kimaumbile ndio Maana wanawake wengi huingiwa na Mapepo.
Akanifafanulia akasema kuwa,Mapepo/Majini yana hisia kama Mwanadamu, hivyo Basi Mara nyingi wakati wa Usiku Mwanamke akilala Uchi usiku ni rahisi sana Jini/Pepo kumtamani na kuamua kufanya Makazi katika Mwili wake."
Sababu ya Pili aliyonipa ni hii "Kutoka na wanawake kuwa katika Mzunguko wa hedhi kila Mwezi na kuona siku zao/damu, Asilimia kubwa ya Majini/pepo yanavutiwa na Damu,pia chakula chao kikuuu ni Damu. Hivyo Basi kwa wanawake wanaokaa Muda Mrefu bila ya kujisafi wakati wakiwa katika mzunguko wa Hedhi, Hawa wadudu huwaingia na kujipatia Chakula kutoka hiyo sehemu. Na wakivutiwa na Damu yako Basi hufanya Makazi katika Mwili wako huku wakisubiria kila Mwezi ili waweze kujitwalia Damu yako"
Hizo ndio Sababu Mbili alizonipa.
Kuna Mwanazuoni Mwongine aliyesomea Dini zote Mbili(Uislam & Ukristu)
Yeye baada ya kumuuliza hili suala akanambia kuwa Sababu kubwa inayowafanya wanawake wapagawe, sio kwamba wote wanakuwa na Mapepo/Majini, lah, ila sababu inayopelekea wao kupagawa, ni yale Mafuta ya Upako ambayo yanatokana na Mti wa Mzeituni. Akanielezea kuwa yale Mafuta yana nguvu fulani ambayo yakikutana na Mtu ambaye yuko weak(mdhaifu) kiasilia, basi hutokea ukinzano na kumfanya aenze kurukaruka mithili ya Mtu aliye pagawa.
Sikuishia hapo, Nliwahi kumuuliza Nabii Mmoja maarufu hapa Dar, akanambia angenijibu siku akiwa na wasaa kwani nlimtumia sms.
Tunaomba kwa yoyote yule mwenye kujua zaidi ya haya atujuze ili nasi tujifunze kupitia kwenu.
Nawakilisha.