Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NIMEKUELEWA SANA HATA WAKIJA KUKUPINGA ILA UJUMBE UMEELEWEKA,ATAKAYEJIDAI HAELEWI IPO SIKU ATAJIBU HATA KATIKA WANAFUNZI WA YESU MBONA HAPAKUWA NA MWANAMKE KWANI YESU HAKUWAONA,HAWAKUWEPO,WALIKUWEPO ILA ALIMAANISHA HAWA WATU SIO ACHA WABAKI KUWA HAWA
Pia shetani (Mapepo) huwatumia wanawake zaidi kufanikisha adhma yao kwakuwa ni viumbe dhaifu kuliko wanawake.Rejea kwa Eva pale bustanini,Rejea kwa Delilah alivyomlaghai Samson kwa wafilisti,Rejea kwa mke wa Ayubu (Japo hakufanikiwa).Mifano ni mingi mno katika Maandiko,Kasome utaelewa.
Kwa akili ya kawaida adui hawezi kumshambulia mdhaifu ili mdhaifu akamshambulie mwenye nguvu. Huanza na mwenye nguvu, hivyo shetani alimshawishi kwanza mwanamke kwa kuwa ndiye mwenye nguvu na ndiye lango la maisha ya binadamu. Angeanza na Adam kusingekuwa na impact yoyote kwani Adam alishaonekana dhaifu tangu mwanzo ikabidi kuumbiwa msaidizi mwenye nguvu. Ikabidi msaidizi aumbwe kwa mfupa. Mfupani imara mara 1000 kuliko udongo. Au? Wafalme na wanaume wote waliokuwa na nguvu za kimwili na kisiasa na kiuchumi hawakuweza kusimama mtikisiko wa mwanamke. Si Daudi, si Sulemani, si Samsoni, si Ahabu mbele Jezebel, si Xerxes mbele ya Esther, si Yuda mbele ya Tamari, si wapelelezi mbele ya Rahabu.
Nafikiri juu ya kiumbe ambaye ni Msaidizi (Kwa mujibu wa Biblia na Quran tukufu) tunapompa nafasi za kuongoza eti kwa kigezo cha HAKI SAWA/USAWA WA KIJINSIA huku tukisahau kabiisa kuwa Mwanamke hapaswi kuwa kiongozi.Binafsi nasema kuwa huu ni muendelezo wa hila za hawa Mapepo na siyo vinginevyo (Mapenzi ya Allha).
Mungu yupi unamuongelea? Miriam alikuwa kiongozi sambaba na Musa na Haruni. Katika Waamuzi 4 tunamuona mwanamke nabii Debora akiongoza taifa. Kaangalie mchango wake kwenye vita ya Sisera na Barak. Hapo utamkuta na mwanamke mwingine aitwaye Jael. Ni watumiaji wazuri wa akili. Ndo maana mkaambiwa muishi nao kwa akili (knowledge).
Hizi ni hila za hao Mapepo tu,Si Mapenzi ya Mungu mwanamke kumuongoza Mwanamke japo Uwezo huo anao ila MUNGU HAKUWAPA MAMLAKA HAYO.Ndiyo tafasiri ya Mwanamke kutolewa ubavuni mwa Mwanaume,ili tu Mmoja awe chini ya Mwenzake na siyo kama tulivyokubali kuliwa Vichwa na hawa Mapepo kwa vigezo vya kipuuzi.
Mtu mwenye nguvu na akili hawezi kuliwa kichwa na kitu dhaifu. Ndo maana mapepo hayahangaiki na vitu dhaifu tayari kwa sababu havina impact kwenye falme na mamlaka. Yanashambulia wenye nguvu. Hakuna mahali biblia imesema wanaume ni jeshi kubwa, bali wanawake ni jeshi kubwa.
Hakuna Dhambi ambayo hatutosamehewa kwa Mungu kama kumpa nafasi za uongozi Mwanamke.Mwanamke ni msaidizi,ni mtu wa Nyumbani na siyo vinginevyo.Huku kufanya kazi,Kuwa Boss,Mmiliki wa Kampuni,Asasi mbali mbali nk ni uzembe wa baadhi ya Wanaume kutotimiza wajibu wao ipasavyo hivyo kumpelekea mwanamke kuwa mtu fulani/kujishughulisha.
Hii ni kinyume na Quran na Biblia takatifu. Navyojua Bi Khadija alikuwa mfanyabiashara mkubwa. Na katika Biblia mke katika kitabu cha Mithali 31(Epilogue: The Wife of Noble Character) ni mwanamke anayejishughulisha. Kama unajua historia vijana walikuwa wakienda vitani. Akioa alikuwa anapumzika kupigana kwa muda wa mwaka mmoja kisha hurudi vitani. Kama kazi ya mwanamke ni kukaa nyumbani, ni nani alikuwa akilisha familia wanaume wakiwa vitani? Ni nchi gani duniani iliyopoteza utukufu kwa kuwa wanaume wake wamekufa au kufulia au kulewa gongo? Wanawake wanaweza kuhimili maisha bila wanaume kwa kiasi kikubwa kuliko wanaume. Mwanaume akifiwa na mke atahangaika hajui afanye nini. Lazima atatafuta msaada wa mwanamke: kama si mama yake basi dada yake au housegirl au mwalimu wa day care. Ndo hivyo. Sasa hebu tusikie wanawake wa Rombo wameanza nao kulewa gongo uone kama Rombo haitabaki mahame ya kihistoria ndani ya miaka mitano.
Mungu atupe Macho pamoja na Maarifa tuyaone haya
Hapa umenena vyema. Mungu awape macho na maarifa. Wanaume wengi mmepoteza nafasi zenu. Hamtulii kwenye nafasi zenu. Kilichomtuma Adam kuondoka kwenye ulinzi wa mkewe ni nini? Matokeo yake shetani mwenye nguvu kuliko mwanamke akapata nafasi ya kumpa mlinzi mwenye nguvu kuliko mwanamume hila yakatukuta yaliyotukuta. Au hujui imeandikwa mke atamlinda mumewe? Je, mlinzi aweza kuwa dhaifu kuliko alindwaye? Ukijidai una nguvu kwa kuwa ni mwanaume ukajifanyia mambo bila kutambua nafasi ya mwanamke popote alipo mwanaume, na mwanamke asipotambua nguvu zake na majukumu yake shurti tupatwe.
Wote tunahitaji maarifa. Tukianza kudharauliana kwa vigezo vya udhaifu na nguvu hatutafika. Tunahitaji kuheshimiana na kupendana ili tuweze kufanya kusudio la Mungu.
Mshikaji wewe ni noma yaniYanawaingia kiurahisi wakichuchumaa