MJADALA: Kwanini Wanawake wanaongoza kuwa na majini/mapepo kwa kasi kuliko Wanaume?

MJADALA: Kwanini Wanawake wanaongoza kuwa na majini/mapepo kwa kasi kuliko Wanaume?

Nashuku

Nashukuru kwa majibu mzuri, ila naomba maelezo kidogo kwa namba mbili. Umesema majini au mapepo hayapendi watu wachafu hivyo hupenda kuwaingia watu walio wasafi kimwili kimatendo nk. Lakini kupa mtaani kwetu kuna dada mmoja ambaye ni popo, lakini kwake kupandisha ni kama kawaida.

Je, hilo limekaaje mwanajamvi?
Kuna mapepo Kazi yao ni kukuharibia tu hayo yakikuingia yanakufanya unakuwa Malaya sana ni mapepo mahaba hayo
 
Kuna mapepo Kazi yao ni kukuharibia tu hayo yakikuingia yanakufanya unakuwa Malaya sana ni mapepo mahaba hayo
........hahahaha! Nimekupata mwanajamvi. Je, huwa inakuaje pale pepo mzuri anapomwingia mtu? [kama pepo wazuri wapo lakini]
 
Mapepo, majini, manyamkera, mashetani, popobawa, vibwengo, ibilisi na vingine vya aina hiyo ni stori tu...
Inasikitisha sana kuona watu wengi sana wanaamini katika upuuzi wa aina hiyo!
 
kwa hiyo " Mpaka upandishe majini " ndio ujijue "" kuwa una majini "" karagabaho""....

Sio lazima upandishe majini, wanaume wengi wenye majini unaweza kuwajua kwa tabia zao. Hata mtu mwenyewe anaweza asijue kama ana jini/majini mpaka anakufa.
 
Sio lazima upandishe majini, wanaume wengi wenye majini unaweza kuwajua kwa tabia zao. Hata mtu mwenyewe anaweza asijue kama ana jini/majini mpaka anakufa.
Anhaaa ....kwahiyo kila mtu anayo ""? hebu nipe sbabu inayopelekea mpaka kila mtu awe na hayo majini "",!
 
1-pepo ni roho ambayo haina mwili sasa inatanga tanga kutafuta makazi sasa anaweza kuingia kwenye kichwa cha MTU aliyempenda pia anaweza kuingia kwa kutumwa aingie kwa MTU

2-mapepo hayapendi mtu mwenye vurugu na mchafu sasa wanaume wengi ni wachafu kuanzia mwili, matendo nk. Mwanaume unakuta anakuwa na mademu kila mtaa ,mapepo hayapendi, pia mwanaume utakuta anashinda bar na kulewa ,mapepo hayapendi na Kazi za wanaume ngumu muda Mwingi unatoka jasho mapepo hawapendi...mapepo yanapenda harufu nzuri ya perfume muda wrote

3-makazi ya majini na mapepo ni baharini na malkia wao anaishi chini ya bahari
Nawasikitikia sana masela ambao hawali mademu,hawapigi ulabu..... Kwa comment hii naanza kuvuta na ganja
 
Sio lazima upandishe majini, wanaume wengi wenye majini unaweza kuwajua kwa tabia zao. Hata mtu mwenyewe anaweza asijue kama ana jini/majini mpaka anakufa.
Kitu usichokiona na usichokijua maana yake ni hakipo katika ulimwengu wako, hivyo mtu atakaekuwa na mashetani kichwani kwake na asijue inamaana hana hayo mashetani.
 
Yaani hata huko kwenye nyumba za ibada kwenye kuombewa kwa asilimia kubwa wengi wanaoamsha haya mapepo wanakuwa ni wanawake tuu.

Sijawahi kuona eti mtu mzima tena alovaa suti na tai yake eti anagalagala chini kaamsha mapepo hivi kuna siri gani kwenye hii jinsia ya kike kushambuliwa na hawa viumbe.
 
labda mapepo yatakuwa yanaheshimu sana suti, btw ngoja tuwasubiri wajuvi watudadavulie hapa..
 
Back
Top Bottom