MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

Makadirio yanarandana na ukweli japo umeweka makadirio ya juu mno kwenye return zako. Punguza hilo pato kwa 15% na ongeza gharama hzo kwa 15%.
 
Habari za mihangaiko wakuu wa inchi.

Naombeni msaada wenu wa mawazo, ishu ni kuhusu business ya mpunga wa hukooo ulanga, Morogoro. Kwa sasa nilivyoambiwa market ya mpunga haiko vizuri kwa sababu ya imported rice from Thailand. Nimefanya shallow feasibility study na kuambiwa kwamba ifikapo mwezi wa 12/2013 na wa kwanza mwaka 2014 bei ya mpunga itapanda mpaka kufikia 80,000/= mpaka 100,000/= tsh.

Hali iko ivi kwa sasa 1 bag of rice with 7 plastics ni 40,000/= tsh. Transportation costs from ulanga to ifakara ni 6000/= tsh per bag. Na storage fee ni 1000/= tsh per bag mpaka hapo utakapo amua kutoa mzigo wako huku kwenye godown za ifakara.

Sasa naomba msaada wa aliefanya hii business anipe maono yake with regards to current market crisis of rice, .Ninataka kununua angalau 100 to 150 bags, nawasilisha .
 
kwa sasa ndo mavuno,debe ni within elf 4 hadi 5. so unachagua unataka gunia la debe 7 au 10, ikifika Dec huwa unapanda bei na huwa ndo msimu wa kuanza tena kulima. unaweza nunua karibu na ifakara insteady of ulanga ili kupunguza transport costs
 
Asante kwa msaada wako...sasa nilifatilia na swala la kuuuhifadhi huo mpunga kwenye magodown ya huku nikaambiwa ni sh. 1000/= kwa kila gunia utalohifadhi mpaka kipindi utapouza huo mpunga. ..swali langu, ulinzi wake ni mzuri? Kama utajari kunisaidia kwa hilo.
 
Mkuu hii biashara imekuwa unreliable kabisa kwa sasa!
Kuna tetesi kuwa mchele hautapanda sana bei miaka 2 ijayo. Hii inashabihiana na hotuba ya waziri wa kilimo, kuwa serikali itaendelea kuingiza Thailand & China rice ili kukabiliana na mfumuko wa bei.

Nakushauri kuwa makini sana, hutapata hasara ila utapata faida kidogo inayoweza kukukatisha tamaa.

Tatizo ni serikali kuingiza mchele badala ya pembejeo zitazowezesha wakulima kuzalisha kwa gharama kidogo.

Mimi pia ni mwathirika wa hii biashara. Unaweka pesa nyingi stock, haifanyi kazi yoyote, mbaya zaidi unakuja kupata unfair return!

NB: Katika bajeti yako usisahau haya;
1. Ushuru wa kila gunia
2. Ubebaji (makuli) + ushushaji na ushonaji
3. Bags/ mifuko.
Zaidi ya hapo nikutakie kila la heri mkuu!
 
GreenCity,
This is the total I want!!! Great advice mkuu nimefatilia sana ishu hii, nimeona nitulie kwanza maana hali si nzuri kabisaaa. Ubarikiwe GreenCity
 
Last edited by a moderator:
Nipo ifakara mkuu

Sasa kama uko hapo hapo Ifakara umeshindwaje kufanya quick analysis ya usalama katika magodown, gharama nyinginezo na hata kujua njia gani utumie kwa ajili ya kupunguza cost za ununuzi, kwa mfano kufata mpunga mashambani badala ya kusubiri huo wa hapo kibaoni. Shughulisha kichwa chako mkuu.

Kwa taarifa yako hakuna biashara isiyo na risk au usumbufu. Utapewa ushauri wa kukatishwa tamaa ukakuta kila biashara unayoifiikiria haifai.

Umewahi kuona mpunga ukiwa kwenye bei ile ile July na Disemba?

Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Yote ni mawazo mazuri, ila mhusika endelea kufanya feasibility study ya kukuridhisha then uanye maamuzi, kuingiza mchele wa thailand na china utaadhiri soko lakini bado quality zitatofautiana kama mchele wa mbeya super umebakia juu mpaka sasa,
 
Naomba anayejua kilimo cha matikiti maji na biashara yake kwa ujumla anipe muongozo, nilifanya feasibility study maeneo ya Ruvu, nikakutana na mdau akaniambia morogoro kunasehemu yanastawi vizuri na hutumii gharama kubwa kama Ruvu au bunju ila bahati mbaya niliondoka nje ya nchi kabda sijakamilisha study yangu na nataka nianze nikiwa huku,
 
Yote ni mawazo mazuri, ila mhusika endelea kufanya feasibility study ya kukuridhisha then uanye maamuzi, kuingiza mchele wa thailand na china utaadhiri soko lakini bado quality zitatofautiana kama mchele wa mbeya super umebakia juu mpaka sasa,

mkuu, mchele wa Kyela ambao ni the best ever, kwa sasa unatembea 1000 tsh per kg kule Kyela, mjini ni kati ya 1500 na 1800 tsh! kwa kawaida huu mchele unakuwaga about 1200 tsh kule kyela na about 2200>tsh na unauzika kwa speed lakini kwa sasa watu wengi wanakula yale makapi ya Thailand ambayo ni 600 tsh per kg!

mchele wa kilombero (incl Ifarakara) ni about 800 tsh per kg kwa kule, wakati Dar ni about 1200>tsh. kimsingi faida ipo, ila imeshuka tofauti na misimu iliyopita! hivyo, kama upo jobless ni vema kuingia na kupambana!
 
Mwambie aje maeneo ya kibaoni nina gunia kama 50 hivi anipe 80000 per bag

Mkuu ninavyokwambia nipo ifakara sikutanii...sasa usinitajie bei kana kwamba nipo Sudan. ..bei ni 35000 kwa 40000 ndo niliopata na godown nishapata nimeanza na 100 bags zen ntaongeza nyingine 50 too soon . Tembo hata akikonda vipi afikii hadhi ya sisimizi. Aluta continua
 
mkuu, mchele wa Kyela ambao ni the best ever, kwa sasa unatembea 1000 tsh per kg kule Kyela, mjini ni kati ya 1500 na 1800 tsh! kwa kawaida huu mchele unakuwaga about 1200 tsh kule kyela na about 2200>tsh na unauzika kwa speed lakini kwa sasa watu wengi wanakula yale makapi ya Thailand ambayo ni 600 tsh per kg!

mchele wa kilombero (incl Ifarakara) ni about 800 tsh per kg kwa kule, wakati Dar ni about 1200>tsh. kimsingi faida ipo, ila imeshuka tofauti na misimu iliyopita! hivyo, kama upo jobless ni vema kuingia na kupambana!

Mkuu kyela hali ikoje kwa gunia la mpunga? Bei yake..
 
Mashamba ya watu binafsi ya kukodi kwa ajili ya kilimo cha mpunga au mahindi yanapatikana Mbarali Mbeya. Bei ya kukodi ni 200,000 kwa ekari 1.

Anayehitaji tuwasiliane.
 
Back
Top Bottom