MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

KXY,

Thanks wakuu

Michango nimeipokea, maji nitayatoa mtoni(permanent water source), naamini nikijenga water storage tank litanipunguzia gharama za kupump mara mbili kwa wiki kama mlivyoshauri
Nilikuwa nimekwama kabisa, hasa kwenye hizo taarifa alizotoa mkuu kubota

nitawajulisha nitakapofikia
 
Aisee kilimo cha mpunga sina hamu nacho aisee,kina garama kubwa sana,alafu kwa mfano mwaka huu bei ya mpunga kwa gunia ni elfu hamsini na mchele kilo ni elf moja na mia mbili,.so kwa mfano mwaka huu kutokana na serikali kuingiza mchele mwingi kutoka nje ya nji.klimo cha mpunga kimekuwa cha hasara mwaka huu.
 
Mkuu Tanzanite klm mtu ambaye hajawahi kulima mpunga akisoma ujumbe wako juu anaweza kukata tamaa pia. Mkuu sijapata sababu hasa kwa nini unakata tamaa! Hiyo bei unayoisema ya gunia alfu hamsini gunia hilo ni lenye uzito gani, au debe ngapi?

Gunia la kilo 100 mpunga ukilikoboa matarajio ni kilo 70 za mchele! Bei ya mchele kama ni 1200 uliyoandika juu mbona bado ni bei nzuri tu! Wakulima mnashauriwa msiuze mpunga badala yake muuze mchele! Kwa nini uuze gunia alfu 50 huku ukishuhudia hapo hapo bei ya mchele ni 1200? Bei ya mpunga mwaka huu ilikuwa juu sana hadi serikali ikaamua kuingiza mchele toka nje? Sasa iwapo bado mwaka huu umeonekana ni mwaka wa hasara je ni mwaka gani italipa?

Mwaka huu ulikuwa mzuri sana kwa mkulima tatizo ni tamaa ya watu kusubiri hadi bei ifikie 150,000 kwa gunia ndiyo wauze! Hilo haliwezi kutokea! Mpunga ni zao la uhakika na ili kuendana na gharama zake kubwa dawa yake ni kutumia utaalamu ili upate mavuno makubwa. Kwa kivuno cha gunia 10 au 15 kwa ekari hata siku moja huwezi kuona faida ya kilimo hiki.

Usivunjike moyo, jifunze zaidi utaalamu wa kilimo cha mpunga ili utajirike!
 
Kubota,

mtaalamu kubota may be problem inayoni face ni utaalamu coz example this year nlipata gunia 20 kwa eka,huko magugu manyara,sijui tatizo ni nini,mbegu nliyotumia ni ya kienyeji inayoitwa super.
 
mtaalamu kubota may be problem inayoni face ni utaalamu coz example this year nlipata gunia 20 kwa eka,huko magugu manyara,sijui tatizo ni nini,mbegu nliyotumia ni ya kienyeji inayoitwa super.

kaka Manyara sehemu gani inafaa kwa mpunga nataka kujisogeza pande hizo kikazi na nataka niingie kwenye kilimo hasa cha mpunga na mahindi....

halafu huko mashamba ni ya kukodi au kununua, ningependa kujua na bei tafadhali?

samahani kwa maswali mengi...
 
Kubota,
thanx mzee kwa hii comment yako wengi tumefaidika,,, ila sijaona mavuno baada ya mda gani au labda sijaelewa...
 
wakuu habari ya siku nashukuru kwa taarifa, ni za kitaalamu hasa;

kwa mwenye info za kitaalamu kuhusu aina za mpunga zijulikanazo kama upland rice atujulishe pia, itakuwa ni vema kwa wajasiriamali wengine ambao wangependa kuventure kwenye aina hiyo ya kilimo cha mpunga (nilibahatika kuona vipeperushi vyake kwenye nanenane lindi lakini sijabahatika kupata maelezo kutoka field kwa mkulima hasa
 
Mimi sitataja aina za mbegu lakini mchango wangu ni huu:
Mpunga kwa kawaida hulimwa sehemu zenye maji mengi kama kwenye mabonde, tunaposema majaruba mara nyingi inahusisha sehemu iliyojaa maji. Sehemu kama kyela, kilosa na nyinginezo zina mabonde yanayopokea maji toka sehemu zenye miinuko.

Tofauti na kilimo hicho kuna kilimo cha nchi kavu au miinuko, kilimo hiki hutegemea mvua au umwagiliaji na mpunga wake hautaji maji mengi kama wa mabondeni. Hii ndio 'upland rice', naskia mbegu ya TXD 306 (chotara, inapatikana Moro) inafaa kwa kilimo hiki.
Wazoefu watatupa michango zaidi.

NB: Vp maendeleo?
 
kaka Manyara sehemu gani inafaa kwa mpunga nataka kujisogeza pande hizo kikazi na nataka niingie kwenye kilimo hasa cha mpunga na mahindi....

halafu huko mashamba ni ya kukodi au kununua, ningependa kujua na bei tafadhali?

samahani kwa maswali mengi...

Seto.
Vipi habari?,manyara sehemu inaitwa magugu,na mashamba ni ya kukodi,.
Yanakodishwa kati ya laki mbili mpaka tatu inategemea ni sehemu gani.lakini taadhari garama zimeongezeka sana miaka ya karibuni kutokana na bei ya mchele wa magugu ulikuwa 2000 kilo lakini hivi sasa bei imeshuka mpaka 1200,so faida ni kidogo mno ukilinganisha na garama za uendeshaji.
 
Last edited by a moderator:

Shwari tu kaka, thanx for the info...
 
Habari wandugu,

Naomba ushauri wenu kwa biashara ya mpunga.

Nataka kununua magunia baada ya mavuno alafu nauza baada ya jipindi cha navuno kuisha.

Ushauri wenu tafadhali
 
-Kwa sababu ya ugeni ni lazima uwepo wakati wa manunuzi,ili ujifunze na uhakikishe kinachonunuliwa

-Mara nyingi hurudisha mtaji wako ivo unaweza kuanza kidogokidogo na nadhani sehemu nyingi ndo wameanza mavuno i.e ifakara, mbarali
 
Sorry John Deer,unaweza kufahamu mwisho wa mavuno ya mpunga ni lini?...nilikuwa na mpango wa kununua gunia kadhaa but nimekwama so nilikuwa nataka kujua mwisho wa mavuno ni lini ili nijipange kabla bei haijapanda zaidi.
 
nimesikia elf40 had60 - ifakara
magugu na mang'ola ni elf60,
sasa wa nyanguge mwanza sijajua huko ndio bei rahis kabisa mwaka jana ilkuwa had elf35. be vigilant guys.
 
Habari wandugu,

Naomba ushauri wenu kwa biashara ya mpunga.

Nataka kununua magunia baada ya mavuno alafu nauza baada ya jipindi cha navuno kuisha.

Ushauri wenu tafadhali

Hizi Biashara za Kizamani sana ni Bongo tu ndo bado tunafanya hizi biashara, Nchi zingine waliaacha miaka migi sana iliyo pita,

Wkati Wabongo wakinunua Magunia n Kuficha ndani, Wakenya Huja na Kununua Mchele n kwenda Kugred na kuuza nje ya Nchi yao, Huku Hayo mawazo hakuna tuna subilia Seriali itupe hayo mawazo,

Na kama unafutilia Bunge Waziri wa Kilimo alidai kuanzia sasa Mchele huutapanda Kwa Bei ya Kutisha mke Watu wana Vibari vya Kuagiza free kutoka Nje,

Na Hizi Biashara haziwzi kuwa na Tija na ukipiga na Time Value of Money utaona hakuna kitu, ila hilo hatulijui, mke mtu akilindika agunia mwaka mzima na alinunua elifu 50 na kuja kuuza Laki anaona amepata sana ila ukipiga time na kila kitu ni hakuna kitu,

Na Moja ya kwa nini Mchele umeshuka sana bei ni haya haya mambo make watu walificha magunia ila imebidi wayatoe na wayauze kwa bei ya sasa,

Tunashidwa nini Kuw Wabunifu? Ni lazima uhifadhi magunia tu? hakuna njia nyingine? Tujaribu kuwa wabunifu hii ni karine nyingine kabisa, hiwezekani Mfumo wa biashara wa miaka ya 70 utumike hadileo 2013,

Tunazani Biashara ni kupata Faida mara mbili zaidi,hii sio, na kweli tuna safari Moja ndefu sana,
 
Back
Top Bottom