MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

Wandugu, kwa aliyeko Ifakara, naomba anipe bei ya Mpunga kwa debe. Asanteni.

amelenga wateja wa ndan ya nchi, lakin ushaur wako mzuri ingawa unautusitusi kama kule jukwaa la siasa, customer care hakuna
 
Sorry John Deer,unaweza kufahamu mwisho wa mavuno ya mpunga ni lini?...nilikuwa na mpango wa kununua gunia kadhaa but nimekwama so nilikuwa nataka kujua mwisho wa mavuno ni lini ili nijipange kabla bei haijapanda zaidi.
Sehemu nyingi ni mwishoni mwa mwezi wa saba mkuu
 
Chasha,

Hujamsaidia huyu kijana bado maana yeye anataka muongozo.

Hapo utakuwa umemchanganya zaidi.
 
Habari wandugu,

Naomba ushauri wenu kwa biashara ya mpunga.

Nataka kununua magunia baada ya mavuno alafu nauza baada ya jipindi cha navuno kuisha.

Ushauri wenu tafadhali


Neanne,

Sikushauri ufanye hiyo biashara kwa sasa maana serikali inatolea macho sana bei za vyakula kwakuwa ndio zinaongoza kupandisha mfumuko wa bei na gharama za kuishi.

Mwaka jana wenzako walifanya hivyo wakalia. Serikali ilipostukia kwamba mchele umefichwa kwenye maghala wanasubiri bei ipande ikatoa vibali mchele ukaja kutoka nje na bei ikashuka ghafla. Maana jamaa walikuwa wanaisubiri tu iendelee kupanda ifike kileleni ndio wauze ambacho ni kipindi cha mwisho kabla mavuno.
 
Asante kwa ushauri.

Mbali na kununua mpunga na kuuza, je, nikiamua kulima mpunga itaniletea faida?
 
Asante kwa ushauri.

Mbali na kununua mpunga na kuuza, je, nikiamua kulima mpunga itaniletea faida?

Yeah, kulima kutakupatia faida halali zaidi kuliko kununua na kufungia ndani wakati wenzako wanakufa njaa. Ila ukilima usiuze mpunga, nashauri uongeze thamani kwa kuuza mchele
 
Chodoo,

Kwenye hayo mahesabu kuna contingency? what if mvua haikunyesha? what if mvua ikapitiliza ikanyesha kipindi haitakiwi?

Tuwekee what ifs halafu utupe projections ambazo ni pessimisstic ili tuelewe hali halisi

Inaonesha una elimu ya uchumi. Ktk project preparatn lazima umaximize cost na uminimize revenue(output). Lengo ni kupata picha halisi. Bt wakati wa utendaji unakomaa kuminimize cost, na wakati wa kuuza unakomaa ku maximize revenue
 
kilimo cha kutegemea mvua siyo cha uhakika sana, nililima mpunga pale signali - kama 20km toka ifakara kuelekea ruaha/kilombero, ukweli nilipata lakini cyo ktk matarajio yangu, ila maeneo yote ya ifakara ni mazuri kwa mpunga lkn ishu ni mvua kwa yale maeneo yasiyo na umwagiliaji, kuna sehemu moja inaitwa 'pawaga' ipo iringa na ni 45km kutoka pale mjini iringa kule ni kilimo cha umwagiliaji kwa kwenda mbele na maji niya uhakika, twendeni hata huko jamani tuweze kudiversify risks ya mvua kwa kuwekeza kotekote wakuu.
 
Habari wandungu,

Mimi si mzoefu wa kilimo, naomba wataalamu na wazoefu wa kilimo wanijulishe kuwa ni kilimo kipi kipo juu zaidi (faida kubwa) kati ya mahindi na mpunga?

Asanteni wana jamvini
 
Habari wandungu,

Mimi si mzoefu wa kilimo, naomba wataalamu na wazoefu wa kilimo wanijulishe kuwa ni kilimo kipi kipo juu zaidi (faida kubwa) kati ya mahindi na mpunga?

Asanteni wana jamvini

Vyote viko juu inategemea na location. Kwa mfano, Musoma/Tarime kwa Wakurya mla ugali ndio anaonekana kala chakula, ilhali huku Pwani mla wali/ubwabwa/biliani anaonekana ndio mambo safi. Musoma ugali ni very expensive kuliko wali.

Tuangalie swali lako kibiashara zaidi, kwa sasa mpunga na mahindi ni ngoma draw.
Wewe kwa sasa hivi uko wapi, hapo ulipo wanalima nini?
 
Nipo D'salaam, nataka kwenda mkoa kujishughulisha na kilimo.

Asante mkuu
 
Back
Top Bottom