Misterdennis
JF-Expert Member
- Jun 4, 2007
- 1,741
- 481
Hizo hesabu umepiga kama vile unalima kenya. Subiri nitakuandalia mchanganuo wa kweli.
Mkuu, umenichekesha kweli, hivi kulima kenya na huku kwetu ipo tofauti?
Ninausubiri mchanganuo....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizo hesabu umepiga kama vile unalima kenya. Subiri nitakuandalia mchanganuo wa kweli.
Mavuno yameisha mwezi uliopita, msimu mpya unaanza tena november.
Hizo hesabu umepiga kama vile unalima kenya. Subiri nitakuandalia mchanganuo wa kweli.
Kumbuka tangazo linasema mashamba ya mpunga ya kukodi Mbeya yanapatikana.
Ndani nikaongeza mashamba ya MPUNGA au mahindi. Kwahiyo mahindi ni au, lakini wazo la kwanza ni Mpunga. Je bei ya gunia la mpunga kwa sasa ni ngapi na mwezi desemba mpaka april gunia la mpunga linauzwa bei gani?
Kama ameshusha au ameipaisha bei hiyo ni juu yake. Ukilima mahindi si lazima ukauze TANDALE, unaweza kwenda kuuza NAIROBI, pia si lazima uuze hapo hapo ukishavuna tu, unaweza kusubiri wakati wa msimu wa bei nzuri.
unadhani hizo gunia 20-30 utakazopata kwenye mpunga au mahindi baada ya kulima kwa kuwekeza pesa nyingi kukodi, mbolea, vibarua (hata kama utalima mwenyewe), kupalilia, kuvunga, kupura....ukiuza gunia moja utapata hata faidi ya tsh 50,000 hata ukiuza Nairobi?? fikiria kuhusu gharama za usafiri pia?
Hiyo gharama ya kukodi ni kubwa mno labda kama wewe ni dalali na kama wewe ni dalali kupata mtu wa kukodi sahau, labda awe asiyeweza kupiga hesabu hata ya kujumlisha.
think big
Natafuta mashamba ya kukodi kwa ajili ya kilimo cha mpunga cont 0756-654524
Kuna wanakijiji wenzangu wanayo mashamba ya kukodi kwa ajili ya kilimo cha mpunga.
Mashamba yako kwenye bonde la mto Ruvu, kijiji kinaitwa Kitomondo, umbali wa kilometa 40 toka Mlandizi.
Ardhi ni nzuri sana , na mashamba hayo yako karibu na mto Ruvu.
Kama maeneo yaliyoko huko Ruvu utayapenda, tuwasiliane nikuunganishe na hao wanakijiji.
Tuwasiliane:
Simu namba : 0789-310981 (airtel) , au 0655-310981 (tigo).
Mkuu unaweza kujua wanakodisha kiasi gani kwa ekari?
jamani nisaidien mawazo nina milioni mbili nataka kuziingiza kwenye kilimo cha mpunga wenye uzoefu jamani naweza kutoka!
Wataalam na wadau wa kilimo cha zao la mpunga tafadhali naomba ushauri wenu; nina mpango wa kulima ekari 15 za mpunga kwa mwaka huu. Tayari shamba nimeandaa pamoja na mbegu, ninachohitaji kwenu ni ushauri wa dawa aina gani (herbicide) niitumie wakati wa palizi ili nisije nikaathiri au kuua mpunga wangu! Karibuni kwa ushauri.
Jamani member wa jf nina milioni mbili nataka kuziingoza kwenye kilimo cha mpunga vipi kwa wenye uzoefu naweza kutoka!