MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

Misterdennis,

Ndiyo maana nimesema verry funny

Hizo hesabu umepiga kama vile unalima kenya. Subiri nitakuandalia mchanganuo wa kweli.

Kwa hiyo mkuu jamaa amepaisha au ameshusha bei ya mahindi? bei ya mahindi kwa sasa tandale dar ni tsh 45000 kwa gunia. That is si zaidi ya tsh 30,000 mkoani.

Kiukweli ekari moja kukodi kwa tsh 200,000 kwa kilimo cha mazao ya chakula hailipi kabisa.
LABDA KWA KILIMO CHA BANGI
 
Kumbuka tangazo linasema mashamba ya mpunga ya kukodi Mbeya yanapatikana.

Ndani nikaongeza mashamba ya MPUNGA au mahindi. Kwahiyo mahindi ni au, lakini wazo la kwanza ni Mpunga. Je bei ya gunia la mpunga kwa sasa ni ngapi na mwezi desemba mpaka april gunia la mpunga linauzwa bei gani?

Kama ameshusha au ameipaisha bei hiyo ni juu yake. Ukilima mahindi si lazima ukauze TANDALE, unaweza kwenda kuuza NAIROBI, pia si lazima uuze hapo hapo ukishavuna tu, unaweza kusubiri wakati wa msimu wa bei nzuri. Pia cost zake hazipo realistic na si zote unatakiwa kuziingia, mfano huhitaji mbolea wala dawa kwani ardhi ni nzuri na ina rutuba ya kutosha.

Utingo,
 
Kumbuka tangazo linasema mashamba ya mpunga ya kukodi Mbeya yanapatikana.

Ndani nikaongeza mashamba ya MPUNGA au mahindi. Kwahiyo mahindi ni au, lakini wazo la kwanza ni Mpunga. Je bei ya gunia la mpunga kwa sasa ni ngapi na mwezi desemba mpaka april gunia la mpunga linauzwa bei gani?

Kama ameshusha au ameipaisha bei hiyo ni juu yake. Ukilima mahindi si lazima ukauze TANDALE, unaweza kwenda kuuza NAIROBI, pia si lazima uuze hapo hapo ukishavuna tu, unaweza kusubiri wakati wa msimu wa bei nzuri.

unadhani hizo gunia 20-30 utakazopata kwenye mpunga au mahindi baada ya kulima kwa kuwekeza pesa nyingi kukodi, mbolea, vibarua (hata kama utalima mwenyewe), kupalilia, kuvunga, kupura....ukiuza gunia moja utapata hata faidi ya tsh 50,000 hata ukiuza Nairobi?? fikiria kuhusu gharama za usafiri pia?

Hiyo gharama ya kukodi ni kubwa mno labda kama wewe ni dalali na kama wewe ni dalali kupata mtu wa kukodi sahau, labda awe asiyeweza kupiga hesabu hata ya kujumlisha.

think big
 
Unajuwa usilolijuwa ni sawa na usiku wa giza.

Unadhani kukodi hekari 1 kwa laki 2 ni KUBWA?. Usiwe na haraka nitakuthibitishia kuwa unachokiongea hukijuwi ila kwa sababu unao uwezo wa kupata intaneti basi unaweza kuandika tu bila hata kushughurisha kichwa kidogo.

Angalia:
1. Kukodi shamba la mpunga hekta 1 (hekari 2.5) ndani ya mashamba ya mpunga yaliyomo ndani ya miradi ni laki 8 mpaka milioni 1.2. Haya hapa umeelewa?.

2. Kukodi shamba la mpunga hekari 1 nje ya mashamba ya miradi (yaani ya watu binafsi) ni sh laki 2, ili kupata hekta 1 unafanya hekari 1x2+1/2 = 200,000x2+100,000 = 500,000/. Kumbe ndani ya mradi shamba la ukubwa wa hekta 1 linakodishwa kwa sh laki 8 mpaka mil 1.2 wakati nje ya mradi unalipia laki 5 kwa ukubwa wa shamba ule ule sawa na wa shamba la kwenye mradi.

Je kuwa dalali ni dhambi? unadhani kuna nchi inaishi bila dalali? dalali hayupo kisheria? je serikali haitumii madalali? dalali kwa kiingereza anaitwaje?

JE UMEELEWA CHOCHOTE MPAKA SAHIVI?

unadhani hizo gunia 20-30 utakazopata kwenye mpunga au mahindi baada ya kulima kwa kuwekeza pesa nyingi kukodi, mbolea, vibarua (hata kama utalima mwenyewe), kupalilia, kuvunga, kupura....ukiuza gunia moja utapata hata faidi ya tsh 50,000 hata ukiuza Nairobi?? fikiria kuhusu gharama za usafiri pia?

Hiyo gharama ya kukodi ni kubwa mno labda kama wewe ni dalali na kama wewe ni dalali kupata mtu wa kukodi sahau, labda awe asiyeweza kupiga hesabu hata ya kujumlisha.

think big
 
Hongereni kwa kulima kwa vitendo sio kulima kwa maneno.ushuhuda ni darasa kwa wengine,safari ni hatua
 
Natafuta mashamba ya kukodi kwa ajili ya kilimo cha mpunga cont 0756-654524

Kuna wanakijiji wenzangu wanayo mashamba ya kukodi kwa ajili ya kilimo cha mpunga.
Mashamba yako kwenye bonde la mto Ruvu, kijiji kinaitwa Kitomondo, umbali wa kilometa 40 toka Mlandizi.
Ardhi ni nzuri sana , na mashamba hayo yako karibu na mto Ruvu.
Kama maeneo yaliyoko huko Ruvu utayapenda, tuwasiliane nikuunganishe na hao wanakijiji.
Tuwasiliane:
Simu namba : 0789-310981 (airtel) , au 0655-310981 (tigo).
 
Mkuu unaweza kujua wanakodisha kiasi gani kwa ekari?
 
Mjin noma kaka mi mwenyewe nampango wa kwenda katavi au moro nikiwa moro i will find u mr ok
 
Jamani nisaidien mawazo nina milioni mbili nataka kuziingiza kwenye kilimo cha mpunga wenye uzoefu jamani naweza kutoka!
 
Jamani member wa jf nina milioni mbili nataka kuziingoza kwenye kilimo cha mpunga vipi kwa wenye uzoefu naweza kutoka!
 
Jaribu kusoma hicho kitabu nime-attach kinaweza kukupa pa kuanzia. Usiwe mvivu wa kujisomea.

Wataalam na wadau wa kilimo cha zao la mpunga tafadhali naomba ushauri wenu; nina mpango wa kulima ekari 15 za mpunga kwa mwaka huu. Tayari shamba nimeandaa pamoja na mbegu, ninachohitaji kwenu ni ushauri wa dawa aina gani (herbicide) niitumie wakati wa palizi ili nisije nikaathiri au kuua mpunga wangu! Karibuni kwa ushauri.
 
Attachments

Back
Top Bottom