Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,199
- 7,562
Wakuu,
Mjadala huu unawahusu wale ambao 'in a serious note' wanafikiri Tanzania tunahitaji 'tume huru' ya uchaguzi tofauti na hii tuliyo nayo. Kama wewe ni miongoni mwao, fuatilia mjadala huu kwa karibu, utakujengea uelewa ambao haukuwa nao hapo kabla.Kama pia wewe unadhani ndio unatakiwa kuongoza wenzako, fuatilia pia; utapata matokeo makubwa, yanayoeleweka, kwa gharama na fuu na bila mtu kuumia.
Angalizo; Tayari kuna hoja kwamba wanaotetea au kudai mambo kadha wa kadha hata kama yanaonekana yana umuhimu mbele ya macho ya jamii; wengi wao wanakuwa hawako serious, wanachokifanya inakuwa ni utata tu lakini wanakuwa hawamaanishi.
Ushahidi unaotumika kuhalalisha hoja hii ni kwamba, pale wanapopata nafasi ya kufanikisha kile wanachodai hupindisha, kwa mfano wanapopewa mbinu ambayo inaweza kuwasaidia kufikia lengo, huikwepa na kushika mbinu ambazo zinawakwamisha ili wakwame halafu kila siku waonekane wapo wana struggle. Wanakuwa ni sawa na mchezaji anakimbia na mpira kwa shida sana halafu akifika golini anarudisha mpira alikotoka.
Tunaleta mada hii chini ya falsafa ya usidhanie mtu ubaya kabla ya kujiridhisha kwanza. Unatakiwa ummchukulie kila mtu kwamba ana nia chanya juu ya mambo ya msingi hadi pale atakapodhihirisha vinginevyo.Usidhani ukimpa mtu hela yako atakula, mpe kwanza ale ili ukimlaumu umlaumu kwa haki.
Mjadala huu utalenga kujibu maswali makubwa (5) ambayo ni?
1.Tatizo la msingi hasa ni nini na linatokana na nini?
2. Je! wanaodai tume 'huru' ya uchaguzi wanaelewa wanachodai hasa ni nini, na wana uelewa wa pamoja au kila mmoja anadai kitu anachokijua mwenyewe kichwani mwake?
3. Nani anafanya nini, kwa nini, na matokeo yake ni nini?
4. Nani anatakiwa afanye nini ili iwe nini na asipofanya itakuwa nini? na
5. Kwa nini wanaotakiwa wafanye wanachotakiwa kufanya hawafanyi na pengine pamoja na mjadala huu hawatafanya na wataendelea kulalamika?na ni nini cha kufanya katika hali kama hiyo?
Kwa kuwa tumesema mjadala huu ni "mpana", tutaenda taratibu sana ili kila anayetaka kuelewa aelewe.