Kuhusu Tume Huru kwa sasa kwa mtazamo wangu inasukumwa na jambo moja kubwa; wapinzani wanataka wajione wana nafasi sawa na CCM kwenye battle field, yaani wakati wa uchaguzi, mgombea wa CCM na wa upinzani, wote wawe na haki sawa, nguvu sawa za kuwashawishi wapiga kura, kura zihesabiwe kihalali bila kuwa na influence toka nje (wakuu wa mikoa, wilaya, polisi, wakurugenzi wa majiji na halmashauri) mpaka mshindi atapotangazwa.
Kuna issue ya msingi ya m/kiti wa Tume ya uchaguzi, huyu nae anateuliwa na Rais, ambae kimsingi ni m/kiti wa chama cha siasa ambacho kinakwenda kwenye chaguzi mbalimbali kushindana na vyama pinzani, sasa huyu m/kiti anaetegemewa kuwa referee halafu hapo hapo tena anamuona bosi wake akitolewa jasho kwenye mechi anaweza kuwa na ujasiri wa kuchezesha fair bila kumpendelea bosi wake kwa namna yoyote?!
Suala la kuwa na Bunge huru hili limezungumzwa sana, tunajua ili mtu awe mbunge kwa sasa lazima jina lipitishwe kwenye kikao cha mkutano mkuu ambapo m/kiti wa kikao ndie huyo huyo Rais wa nchi. Baada ya hapo jina likishapitishwa ndio mtu anakuwa na nafasi ya kugombea ubunge kama katiba inavyotaka, then ndio aje awe Spika wa bunge akifanikiwa kupita. Sasa hapo utaona m/kiti wa mkutano mkuu akiamua kumpoteza huyo mtu mapema uwezo huo anao, hii inasababisha Spika wa bunge baadae akipata nafasi ajione ana deni kwa m/kiti wa chama chake, na hii inatokea hata kwa wabunge wengine wa chama chake, ndio maana wengi huunga mkono kila hoja ya chama chao hata kama ni ya kijinga, sasa hapa uhuru wa Bunge kufanya mambo yake utatoka wapi?!.
Mahakama; majaji wa mahakama kuu wote wanateuliwa na Rais ambaye nae ni m/kiti wa chama cha siasa, sasa litapokuja suala la kudai haki litakalohusisha chama kingine ambacho ni mshindani wa chama cha m/kiti huyu jaji atatoa wapi ujasiri wa kuamua hilo jambo kwa haki bila kuwepo na hisia za upendeleo? na wakati mwingine hizi hisia ndio hufanya wengi waone haki haitendeki, hata kama itakuwa inatendeka.
Baada ya hapo sasa, ndio tutajua kama hao wapinzani walikuwa na mengine binafsi waliyoyaficha, but kwa sasa ni muhimu hayo hapo juu yafanyike ili kuleta ushindani sawa.
Sent using
Jamii Forums mobile app