Inaendelea;
========
Hatua za kuchukua kwa sasa;
1. Kuhusu Kumshirikisha Mh. Rais;
Kwanza nianze kwa kumshukuru mkuu
zitto junior kwenye mchango wake namba 34. ameonesha kuwa mwezi uliopita yalishaandaliwa mapendekezo na 'CHADEMA' na kuwasilishwa kwa Mh.Rais akiombwa awezeshe mchakato kuanza kuanza kufanyiwa mapitio ya mapendekezo hayo . Hatua hiyo ni hatua ya kwanza muhimu ambayo ndio tulitaka kuanza kushauri kama hatua ya kwanza kuchukua(kwa bahati sikujua kuhusu kuwepo kwa rasimu ya mapendekezo hayo kabla) kwa hiyo
zitto junior kafanya jambo la msingi ku share.
Kimsingi ili maboresho au mabadiliko kwenye mambo makubwa ya kitaifa yaweze kufanyika na kufanikiwa kama hili tunalojadili leo, sio tu kwamba ni lazima Mh.Rais ashirikishwe kikamilifu na akubaliane na mchakato lakini pia yeye mwenyewe kuwa kiongozi mkuu wa mabadiliko hayo, vingenevyo mabadiliko hayo yanakuwa hayawezekaniki.
Kwenye mabadiliko ya kutoka siasa za chama kimoja kwenda vyama vingi, Mwl. Nyerere na Mzee Mwinyi, sio tu kwamba walishiriki bali wao ndio walikuwa vinara wa kuhamasisha mabadiliko hayo.
Kwenye mchakato wa Katiba mpya, sio tu kwamba Mzee Kikwete alishiriki, bali yeye ndiye alikuwa kinara wa mchakato huku akifanya mambo mbalimbali kuhalikisha Katiba mpya inapatikana huku akisisitiza kwamba asingependa amalize kipindi chake cha urais bila katiba mpya kupatikana. Kwa bahati mbaya hilo halikuwezekana kwa sababu ya misuguano ya kimakundi ambapo baadae tutaeleza kwamba ni nini kinaweza kufanyika ili kupunguza misuguano hiyo kwenye mambo mengine ya msingi ili yasije yakakwama kama la katiba mpya.
Kwa imani yangu binafsi, mchakato wa maboresho ya Tume utaanza chini ya Mh.Magufuli hivi karibuni na atausimamia, ila kama watu wengine wasipotimiza wajibu wao, utakwama kama ishu ya katiba mpya ilivyokwama licha ya jitihada za Mzee Kikwete.
Tunachoweza kuongeza katika hili la kumshirikisha na kumuomba Mh. Rais asaidie mchakato huu wa uboreshaji wa tume ni kwamba; ziendelee kutumika mbinu za kumshauri na kumshawishi kidiplomasia. Hapa tusisitize 'Kidiplomasia'. Lugha za kukejeli na kuoneshana umwamba zinaweza kuharibu zaidi kuliko kujenga, ni bora kujiepusha nazo.
"Jishushe tu, kujishusha hakukufanyi usiwe kiongozi na kujimwambafai hakukufanyi uwe kiongozi Zaidi" (Kikwete, 2019). Hii kauli ilikuwa na fundisho pana kidogo japo wengi waliitafsiri kwenye duara dogo sana.
Hii ni kwa sababu, mwanadamu '
Hasa mwanaume' ana tabia ya ku
'resist' anapohisi kama anashinikizwa au kuburuzwa. Ha 'resist' kwa sababu ya ubaya wa jambo, bali kwa sababu hataki kuona akiburuzwa au kupelekwa. Hili ni suala la kimaumbile, liko hivyo tu.
Nina Imani ukiendelea kufanyika ushawishi wa kidiplomasia na kama ungeanza mapema (ingekuwa vizuri Zaidi), Mh. Rais anaweza kutoa solutions ambazo zitatoa muelekeo kwenye mchakato wa maboresho ya tume. Wakati huo huo mambo mengine ya kuendelea kufanya katika kipindi hiki, tutashauri mbeleni.
===========
Itaendelea