Mjadala mpya: Ni nani aliwaokoa abiria 24 wa ndege ya Precision Air?

Punguza kujifanya unajua kila kitu,unakopi thd za JF kuhusu hii issue,unaziunganisha kisha unaanzisha Thd kwa ID yako! huu ni zaidi ya ujinga aisee.
Kwani shida nini, ungempinga kwa hoja maana ye ameleta uzi uliojaa hoja kibao fikirishi ila wewe umemjibu kwa matusi! Hivyo ndivyo mnavyofundishwa huko Lumumba?
 
Kwani shida nini, ungempinga kwa hoja maana ye ameleta uzi uliojaa hoja kibao fikirishi ila wewe umemjibu kwa matusi! Hivyo ndivyo mnavyofundishwa huko Lumumba?
Hoja zimeshajibiwa,kuna thd kibao kuhusu hiyo issue,huyo kakopi thd za JF hapa hapa akaziunganisha na kuanzisha thd yake,
Halafu usiwe zuzu wewe,Lumumba ndio nini? unafikiri kila mtu humu ni shabiki wa mambo ya kisiasa?
 
Sasa kulikuwa na haja gani kumshambulia mtoa mada!? Kama aliyoandika umeshakutana nayo kwingine ungepita kimya utuache wengine tuchangie. Kumtusi mtu usiyemfahamu ni kiwango cha juu kabisa cha ukosefu wa busara.
 
Wapuuzi huwa wanapuuzwa hawajibiwi..kwakuwa hawana uwezo wa kuandika hata theluthi ya kitu chenye hoja
Wewe ndio mpuuzi,hoja gani umeweka hapo zaidi ya kukopi mawazo ya watu wa humu JF? ni mara nyingi tu hapa JF kitu kikitrend unasubiri watu wakijadili hapa kisha unakuja kukopi idea za watu na kuanzisha thd kisha watu wanakuona bonge la GT.

😀😀😀😀
 
Sasa kulikuwa na haja gani kumshambulia mtoa mada!? Kama aliyoandika umeshakutana nayo kwingine ungepita kimya utuache wengine tuchangie. Kumtusi mtu usiyemfahamu ni kiwango cha juu kabisa cha ukosefu wa busara.
Wewe uliposema "Ndio mnavyofundishwa hivyo Lumumba" ulikua unamtusi nani? au hiyo ndio busara unayoiongelea hapa?
 
Wewe uliposema "Ndio mnavyofundishwa hivyo Lumumba" ulikua unamtusi nani? au hiyo ndio busara unayoiongelea hapa?
Tusi liko wapi hapo kwenye sentensi yangu? Naona unataka kuchepusha mada, acha watu wajadiliane wawezavyo usiwavuruge.
 
Mshana Jr. kama ukiamua kwa thati kutia mchango katika baadhi ya mambo ni dhahiri shahiri ungeleta matokeo chanya kwa kiasi kikubwa, katika uzi wa awali uliokuwa unahusiana na mvuvi aliyeokoa watu 24, nilidoubt kwa kuuliza kuwa kwanini mvuvi huyo amulikwe kuliko wavuvi wengine waliosaidia kuwaokoa watu, kwa bahati mbaya sana hakuna aliyenijibu, sasa kama na mleta mada kaliona hili na kuamua kulianzishia uzi labda linaweza kusaidia kuleta mwanga wa sintofahamu iliyogubika suala hili.
 
Tufani ikishatulia na taharuki kwisha ndio kuna ukweli halisi hutamalaki.. Hiki ndio kipindi chake sasa...!
 
Mkuu hatukatai kuhusiana na ngekewa, lakini pia tukubali kuwa ngekewa zinaweza kuchochewa na baadhi ya watu kwa masirahi binafsi
 
Mkuu hatukatai kuhusiana na ngekewa, lakini pia tukubali kuwa ngekewa zinaweza kuchochewa na baadhi ya watu kwa masirahi binafsi
Nadhani wengi wamesoma heading tu bila kusoma maudhui
 
Kwa hayo ulizungumza nakanusha inaonyesha yakua huna uchambuzi sahihi juu ya hili..

CHAMBUZI MAKINI JUU YA AJALI YA NDEGE ZIWA VICTORIA MWANZA.
1: Huenda wengi wetu tulibaki na taharuki kubwa baada ya ajali kutokea.
2: Vyombo vingi vya habari vimechangia kutopata taarifa kwa usahihi kulingana na uwasilishwaji wa taarifa.
3: Tukumbuke Tanzania haijawahi kutokea ajali ya ndege yenye kubeba abiri wengi au ndege yenye ukubwa kama hiyo iliyoanguka.
4: Vyombo na vikosi vya uokozi kutofanya kazi kwa ufanisi na kutofika eneo husika kwa wakati.
5: Asilimia ya mashuhuda wa tukio walitokea eneo la kanda ya ziwa na baadae kuwa waokoaji na watoa msaada kwa wahanga wa ajali.

KWA NINI MAJALIWA ALIPASWA KUPONGEZWA NA SERIKALI.
Huyu kijana alijitoa kwa asilimia 100% kwenye swala zima la uokoaji na ukisikiliza baadhi ya mahojiano alifanyiwa na baadhi ya media’s utakundua sio yeye alifungua mlango ila alisaidiana na yule mhudumu wa ndege, Kwani inasemekana kuwa mhudumu alikua akihangaika kufanya kila jitihada kuufungua mlango ukaunamshinda ila baada ya majaliwa kufika na wenzake akasogea kwenye mlango na kuanza kusaidiana na mhudumu kwa kuelewana yule dada aliusuma kuja nje yeye majaliwa anauvuta baada ya kupata mwanya kidogo aliomba kasia kwa mwenzie na kuanza kuugonga ule mlango kisha kuupachua kwakua ulikua umejiloki kwa ndani ghafla kwenye hizo jitihada mlango ulifunguka na hapo ndipo shughuli ya uokozi wa abiria kutoka ndani ya ndege ilipo anza kwa kuwatoa na kuwaweka kwenye ngalawa na kuwavusha ng’ambo wakati huo hayo yanaendelea ilikua ni kundi la majaliwa likifanya hivyo pamoja na majaaliwa mwenyewe, Kilichompa credits ni baada ya kuzirahi kwenye tukio lkn kama sio hivyo angekuwa amebaki kama wenzie tu kwa walifanya shughuli ya uokoaji pamoja na ilipofika taarifa kwa PM ni kunakijana aliefanya kitendo cha ushujaa cha kuokoa abiria kwenye ndege iliyopata ajali na anafanana jina na yeye hicho kilichokua kigezo kikubwa cha Majaliwa kuendelea kupata credits nyingine nyingi kutoka kwa MH. WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA.
Na kwa yule dada mhudumu wa ndege kwa upande wake nadhani huwa tunafahamu kwamba kila kampuni inayokuaji huwa kuna zawadi na tuzo mbalimbali hutolewa kwa mfanyakazi au wafanyakazi bora kila mwaka pale kampuni inapokua ikifanya sherehe zake kwa kuongeza mwaka mwingine hivyo huyu dada yeye credits zake atapewa na kampuni anafanyia kazi na hata ikiwezekana bodi ya usimamizi wa safari za anga Tanzania kumtunuku TUZO kwa ujasiri aliufanya kwenye hilo tukio.
 
Tufani ikishatulia na taharuki kwisha ndio kuna ukweli halisi hutamalaki.. Hiki ndio kipindi chake sasa...!
Mkuu kwa kutumia elimu yako ya kiroho uliyonayo nina imani Kuna mengi umeyaona, ingawa uzi huu umeuleta kwa lugha ya kawaida ili kila mmoja ashiriki kwa amani tunaomba utusanue walau hata kwa dokezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…