Mjadala: Mwanza Vs Dar Es Salaam. Nani ni mfalme wa majiji Tanzania?

Mjadala: Mwanza Vs Dar Es Salaam. Nani ni mfalme wa majiji Tanzania?

Sifa za kuwa Jiji ni zipi?...tukijibu hili swali basi tutakuwa tumeokoa muda mwingi sana, maana hofu yangu ni kwamba tusije tukawa na "majiji-vijiji" tukawa tumepoteza maana
 
Nipo sawa kabisa
Basi Mwanza sio ya kuifananisha na Dar es salaam.
Hususan sasa ambapo sehemu kubwa ya mji inabomolewa na kurekebishwa.
Pia hata kwa uchangiaji wa pato la taifa.
Pia hata kiutafutaji huwezi fananisha Dar na Mwanza.
Dar kupo juu sanaaaaaaaa.
 
Sifa za kuwa Jiji ni zipi?...tukijibu hili swali basi tutakuwa tumeokoa muda mwingi sana, maana hofu yangu ni kwamba tusije tukawa na "majiji-vijiji" tukawa tumepoteza maana

1. Idadi ya Watu.
- Mara nyingi, idadi ya watu ni kigezo muhimu. Kwa mfano, mkoa unahitaji kuwa na idadi kubwa ya wakazi ili kutimiza hadhi ya jiji. Nchini Tanzania, idadi ya watu inaweza kuwa zaidi ya 500,000 ili mkoa uanze kufikiriwa kuwa jiji.

2. Maendeleo ya Kiuchumi.
- Mkoa unahitaji kuwa na kiwango kikubwa cha shughuli za kiuchumi, viwanda, biashara, na huduma za kifedha. Jiji lazima liwe na uwezo wa kutoa ajira nyingi kwa wakazi wake na kuwa na uchumi unaokua kwa kasi. Uwepo wa viwanda vikubwa, biashara za kimataifa, na huduma za kitaifa ni muhimu.

3. Miundombinu.
- Jiji lazima liwe na miundombinu bora kama barabara, mfumo wa maji safi na taka, umeme, hospitali, na shule. Uwepo wa usafiri wa umma na uwezo wa kushughulikia ongezeko la watu na maendeleo ya kiuchumi ni muhimu.

4. Huduma za Kijamii
- Mkoa lazima uwe na huduma bora za kijamii kama elimu, afya, na burudani kwa wakazi wake. Shule, vyuo, hospitali, vituo vya burudani, na viwanja vya michezo ni alama ya ukuaji wa kijamii unaohitajika kwa jiji.

5. Utawala na Uongozi.
- Mkoa ambao unataka kuwa jiji lazima uwe na utawala unaojitegemea, unaoweza kushughulikia changamoto za kiutawala, kiuchumi, na kijamii kwa ufanisi. Pia, ni lazima uwe na utaratibu wa bajeti inayojitosheleza ili kusaidia mahitaji ya kijiiji.

6. Mchango katika Maendeleo ya Taifa
- Mkoa unahitaji kutoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa kupitia kodi, ajira, na kuwa kitovu cha shughuli za kibiashara, kiuchumi, na kimataifa.

Kuhitimisha, miji mikubwa kama MWANZA NA DAR ES SALAAM imepata hadhi ya kuwa majiji kutokana na kukidhi vigezo hivi, ambavyo vinaonyesha uwezo wa jiji katika kutoa huduma za msingi kwa wakazi wake na kuchangia katika maendeleo ya kitaifa.
 
Basi Mwanza sio ya kuifananisha na Dar es salaam.
Hususan sasa ambapo sehemu kubwa ya mji inabomolewa na kurekebishwa.
Pia hata kwa uchangiaji wa pato la taifa.
Pia hata kiutafutaji huwezi fananisha Dar na Mwanza.
Dar kupo juu sanaaaaaaaa.
Oyy okay hayo n mawazo yk, lakini pia kwanza ni jiji ambalo lina vigezo vyote
 
Basi Mwanza sio ya kuifananisha na Dar es salaam.
Hususan sasa ambapo sehemu kubwa ya mji inabomolewa na kurekebishwa.
Pia hata kwa uchangiaji wa pato la taifa.
Pia hata kiutafutaji huwezi fananisha Dar na Mwanza.
Dar kupo juu sanaaaaaaaa.
Dar onoda bandari hamna lolote! Angalia Nairobi lile ndio jiji ila nisije kuwa nabishana na ambae hata dar au Nairobi hajafika
 
Back
Top Bottom