MJADALA: Ni changamoto gani unakumbana nayo kwa kuchelewa kuoa/kuolewa?

Nimekuelewa sana khofu ondoa ni kweli wapo wengi sana
 
Hivi vitu huwa mnavikuza sana. Mara nyingi havipo kama vinavyoonekana usoni. Nina miaka 9 toka niachane na mzazi mwenzangu lakini hii habari ya kupasha kiporo haijawahi kutokea na huwa tunaonana na kuwasiliana mara kadhaa na tuko mji mmoja. Kama hofu yako ni usaliti hata ukiolewa na mtoto au mjukuu wa askofu usaliti unaweza kutokea. Mtu anaweza kupasha kiporo wa wapenzi wake aliokuwa nao kabla yako au akaanzisha mapishi mapya na mtu mwingine wakati yuko na wewe. Wanawake wengine wanahofia kuwa na wanaume wenye watoto kwa sababu hawana hela za kuwapa kwa sababu wana majukumu ya kutunza watoto. Hii kwako veepe?
 
"Jamani kwanini haujaolewa!! Unachagua sana jamani!!"
Utadhani wao walijibebea tu. Alafu akijisahau anaanza kukuelezea majanga yake na kukutamania wewe ambae haujaolewa basi tafrani tu!!
Haya mambo bwana!!!

Yaani unakuta hawataki hata kukusikiliza maana tayari wana majibu yao ya kwa nini hujaolewa. Wengine wanakusimanga kuwa unaringa kwa sababu ya hicho kijumba na kigari!! Wengine wanakutafutia mtu bila kukupa taarifa au bila wewe kuwaomba. Unashangaa tu mbona aunt Fulani au shosti siku hizi anakutembelea au kukupigia simu sana na kuongelea mambo ya ndoa? Kumbe anacheki progress!! Wengine hasa wamama wakubwa wanakukazania uolewe unafikiri ni upendo kumbe wana wasiwasi utawachukulia waume zao! 😛 Usipokuwa na helmet kwenye moyo unaweza kuingia kwenye hayo maisha ili watu wafurahi.
 
Its not about kupasha kiporo,uuhusiano unatakiwa uwe wa watu wawili. Ukizaa na mtu nikakuoa tayari uhusiano unakuwa wa watu watatu kiungo mtoto.
Kataa kubali hii inaleta complications, hamna mtu yuko taysri kuona mpenzi wake anawasiliana na ex wake, bond yako na baba wa mtoto haiwezi kuvunjika kamwe.
Mbaya zaidi wengi wanatamani sana baba mtoto abadili mawazo waishi pamoja! Unless ulizaa kwa bahati mbaya kama kubakwa.
 
To be honest sijui nani anaoa bila kuchagua. Na hii notion kuwa 'unachagua sana' sijui kipimo ni kipi? Mtu ambae nitaishi nae hadi kifo kitutenganishe lazima niridhike nae.
 
Mhhhh huu uzi mpaka leo unaendelea??? Kweli mahusiano ni janga la Taifa
 
Mhhhh huu uzi mpaka leo unaendelea??? Kweli mahusiano ni janga la Taifa
Hapana. Mahusiano ni jambo linaloendelea haliishi, kwahio mnaweza kujadili kwa muda wowote ule. Vingi vinajadiliwa humu sio mahusiano tu, chit chat za hapa na pale as well.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…