Mjadala: Ni jambo gani kwenye Maisha yako lilichelewa sana? Ila sasa unaona kawaida sana

Mjadala: Ni jambo gani kwenye Maisha yako lilichelewa sana? Ila sasa unaona kawaida sana

Nilitamani sana kuwa na
1 Familia,Watoto yaani ile kuitwa mama na mume pia aniite mama(napenda mno), nitoke kazini nikirudi home kuna viumbe wananiita mama🥰
2 Kuwa na CPA.
Nk.

Cha ajabu hamna hata kimoja kilichotimia hapo, CPA nayo inanipa za uso😔 but Mungu ni mwema i hope yote yatatimia hata kama kwa kuchelewa.🙏
Trust the Lord,

Kila unachotamani kitatimia.
Na utafurahia sana wala hutajuta kuchelewa.

Mungu wa Mbinguni aonae haja za Mioyo yetu na akufanikishe kila hatua.

Utabarikiwa uingiapo na Utokapo.

Amen!!
 
Kupata kazi nzuri nimepata naona kawaida pia ndoa nlikua natamani Sasa naona kawaida nimegundua kwenye maisha Kila level Ina changamoto zake hakuna siku utasema sasa nimemaliza kila kitu nipumzike ni enjoy so Kila hatua uliyopo jifunze kua grateful na kutafuta furaha hapo usiseme mpaka nipate kitu flani na flani coz utapata hivyo vitu na zitakuja changamoto mpya
Kabisa nkakisali2
 
Kupanda ndege aisee, nilikuwa naziangalia anganitu.

Safari ya kwanza naingia kwenye pipa kutoka kwa mamaenu mpaka Nairobi then Dubai then na connect Papua new guinea Daah.

Kuanzia sikuyakwanza natoka terminal 1 nilikuwa na sali kabla hatuja takeoff na landing lakini sasaivi duuh[emoji23][emoji23][emoji23] niki Bod in tu nachapa usingizi daaah.[emoji205]

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Naomba Mungu anisaidie maana natamani sana niwe na

1. homestead yangu yenye ekari 500 humo niwe nina ng'ombe wengi, mbuzi wengi, kuki wa kienyeji, kondoo, na familia yangu iishi humo humo.

2. Nipande ndege niende nje ya mipaka ya nchi hii.

3. Nipate kazi nzuri zaidi ya hii niliyonayo sasa hivi.
 
Back
Top Bottom