Jobless_Billionaire
JF-Expert Member
- Aug 9, 2022
- 3,106
- 8,101
Wakuu habari za wakati huu.
Samahani, nimekuja na mjadala tata kidogo ila nitafurahi kama wachangiaji watatoa hoja zenye mantiki tofauti na kuzozana pasipo misingi. Sijasimamia upande wowote, kila upande uwe huru kutoa hoja zao ili nipate kujifunza jambo. Kikubwa tu hoja ijibiwe kwa hoja.
Kwa mujibu wa maandiko ya dini tulizo nazo, tunaelezwa kuwa matendo yako ndio yataamuru upande gani mtu husika atasimama kipindi cha kutolewa hukumu.
Kama mtu alitenda maovu, machukizo au makatazo basi ataelekea jehanamu au kwenye ziwa la moto na huko ndipo atakapokuwepo milele kama adhabu au mshahara ya yale aliyoyatenda. Na endapo mtu alienenda sawasawa na mapenzi ya Mungu au Allah, basi atafurahi milele kwa kuimba, kucheza na kutunukiwa tunu nyingi kama malipo ya wema aliotenda.
MSINGI WA HOJA YANGU
Je, baada ya yote hayo kufanyika (hukumu kutoka na kila mmoja kusimama anapostahili), watu watakuwa na kumbukumbu zote walizokuwa nazo toka duniani? Yaani wataendelea kukumbuka, kuwa na utambuzi uleule wa kujua wema na ubaya au vitadhibitiwa na kufanywa kuwa na akili mpya iliyotambua lolote?
Kama jibu ni ndio, itakuwa ni kwa wale wema tu? kwa nini ifanyike kuwa hivyo? Ili wasijue kama waovu wanaadhibiwa?
Na kama ni hadi kwa wote hadi walio motoni, hawatakuwa wakijua wameadhibiwa? Kama ndivyo, itakuwaje ni adhabu ingali hawafahamu?
Na kama utambuzi utabaki huuhuu, watu watafikiria nini akilini mwao? Watamtazamaje mwenyezi Mungu? Hisia zao juu ya wapendwa wao, wazazi wao na watoto wao ambao hawatokuwa sehemu ya furaha kwakuwa wameadhibiwa tena adhabu ya milele? Itakuwa ni furaha ya kweli?
Tujadili tupate kujifunza