Mjadala wa Bandari ni ama tuchague kusikiliza mtaalamu Hamza Johari au mpenda sifa Tundu Lissu

Tanzania hakuna wataalamu boss, wataalamu wako huko NASA wanarusha vyombo anga za mbali. Kungekuwa na wataalamu tungekodisha bandari kwa waarabu?
China wamekodisha bandari sita kwa waarabu hawa hawa, unataka kuniambia kuna kitu chochote tumewazidi kama nchi?.

London na Southampton wamekodisha bandari zao kwa DPW, na wao hawana elimu kama sisi watanzania?.

Punguza kujidharau, punguza hizi akili za mtaani za kujiona hatuwezi katika kila kitu.
 
Ukodishaji wao na kwetu ni tofauti.huko hakuna vifungu vya kijuha kama vya bandari ya dar.huko wamezingatia maslahi ya nchi yao na siyo kama ilivyo kwetu.kwetu ni uporaji kabisa na siyo uwekezaji
 
Hamza mtaalamu wa ndege za bandarini! Huyu alipandikizwa tu aseme ila aliogopa kumkatalia bosi wake.
 
Ukodishaji wao na kwetu ni tofauti.huko hakuna vifungu vya kijuha kama vya bandari ya dar.huko wamezingatia maslahi ya nchi yao na siyo kama ilivyo kwetu.kwetu ni uporaji kabisa na siyo uwekezaji
Tunaviona vifungu vya kijuha baada ya kuwasikiliza kina Nshala na Lissu, hakuna kifungu cha kijuha hata kimoja kutokana na mazingira ya biashara yenyewe.

Wengi wetu tumepotoshwa kwamba IGA ndio inayokwenda kutumika katika biashara ya bandari, hatukujua kuwa mikataba ya Concession na Lease ndio kila kitu.
 
Ishu ni mikataba sio dp world
 
Kumbe ni msomi We Ukraine. Hao alikosa admission Bongo ndiyo wakapitia uchochoroni. Hizo qualifications zake za International Law itakuwa ni vicertifocate tu vya miezi kadhaa.

I am not impressed na qualifications zake.
 
Tumechagua kumsikiliza mpumbavu mwenzetu Lissu.

Case closed
 
Mkuu umesema vizuri na ndiyo maana nikaleta huu uzi hapa. Ukisoma hapa utaweza kuongeza uelewa zaidi
 
Inawezekana ukawa uko sahihi, ebu tusubiri humu tuone watasema tu waliosoma nae.
 
1)Huko vyuo anafundish Nini huyo Hamza?

2)Wanafunzi wake sana maoni gani juu yake?(Rate my professor)

3)Na secondary kasoma wapi?
 
Hivyo vicertificate vya huko India, kwako unaona ni vya pekee sana?

Hivi, wakiitwa wasomi wakubwa wa nchi hii, na huyu naye utamhesabia? Sasa naelewa ni kwa nini mkataba ule wa DP ni wa hovyo kiasi hiki. Huyu wa elimu ya kuunga unga ameliingiza Taifa kwenye hasara tupu.
 
Tunamsikiliza Lissu
Tuondolee wauza nchi
Weh nawe usituchoshe na hadithi za kufikirika
 
Mkuu uko sahihi kabisa, sasa kwenye bandari twende na nani?
 
Mkuu acha hasira, mie sijahukumu mtu hap, siko kwa Johari wala kwa Lissu, hoja yangu kati ya hao wawili kwenye suala la bandari twende na nani? mwenye certificate ya india ila ya usafirishaji, au mwenye LLM ya Warrick?
 
Cv mbovu sana hii ndiyo maana anatetea maamuzi ya kipumbavu na kilofa.cv ya kuungaunga vipande vya ngazi ya cheti
Mkuu ungekuwa mtu makini ungekuwa tayari unaelewa kuwa Johari Hamza ndiye kiongozi wa timu ya Tanzania inayojadiliana na DP World ila kwa vile Lissu hajamtaja hujalipata hilo. Ki msingi ndiye alienshiriki kuandaa IGA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…