Hivyo vicertificate vya huko India, kwako unaona ni vya pekee sana?
Hivi, wakiitwa wasomi wakubwa wa nchi hii, na huyu naye utamhesabia? Sasa naelewa ni kwa nini mkataba ule wa DP ni wa hovyo kiasi hiki. Huyu wa elimu ya kuunga unga ameliingiza Taifa kwenye hasara tupu.
Mwanzo nilidhani unajua unachoandika kumbe ni mtupu tu usiye na data wala ufahamu wa unachoandika.
Hamza alipambana mpaka Ziwa Malawi kwa sasa linamilikiwa nusu kwa nusu enzi za hayati Benard Membe na JK, sijui kama hilo unalifahamu.
Hamza alipambana mpaka mamlaka ya anga TCAA wakapewa tuzo maalum ya ubora baada ya kupata asilimia 65, wakati miaka ya nyuma mwisho wetu ulikuwa ni asilimia 35 na akakabidhiwa hayati JPM, sijui kama hilo unalifahamu!.
Hamza ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya ICAO shirika linaloongoza masuala ya ndege duniani, utungaji sera wote wa masuala ya sekta ya anga unamhusu yeye pia, sijui kama hili pia unalifahamu!.
Hao maprofesa wa kibongo wanaokuzuzua kichwa wamefanya lipi la maana, usije ukataka kumvunjia mtu heshima kwa sababu humuoni sana saa mbili kamili usiku akiongea ITV au TBC, wapo wengi wenye impact zao na huwezi kuwajua kwani hawana makuu.
Mkataba wa Consession na ule wa Lease ndiyo yenye umuhimu kwani huko ndiko biashara kwa kina zinakwenda kuwekewa vifungu, hili na wewe uliingia kichwa kichwa ukadanganya watu humu!.
Leo unawaponda watu wanaopambana usiku na mchana kwa ajili ya nchi yao!.