TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Siku moja niliku pm ila naamini uliona meseji hiyo japo haukunifeed back.

Hiki ulichokiandika hapa kiko wapi dada?
Naweka video, ni kubwa ndo mana inachukua muda

Asnt sana kwa kufatilia mjadala na maendeleo ya jimbo letu[emoji120]
 
BUKOBA[emoji24] [emoji24] [emoji24]



Mwonekano wa mji wa Bukoba 1972, 2014 na 2016 kwa kufuata mtiririko wa picha zote tatu (3). Hakuna kilichobadilika cha maana[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
MKOA WA KAGERA TARATIBU WAANZA KUREJEA KATIKA ENZI ZA NSHOMILE KATIKA ELIMU WASHIKA NAFASI YA TANO KATIKA KUMI BORA KITAIFA DARASA LA VII

Na: Sylvester Raphael

Kutokana na usimamizi na uongozi thabiti chini ya Mkuu wa Mkoa mahili wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kiwango cha Elimu mkoani hapa kimeanza kupanda kwa kasi na kuifanya Kagera kuanza kurejerea katika miaka ya 1980 wakati ule mkoa ulipokuwa unasifikakwa jina la “Nshomile”

Katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2016 Mkoa wa Kagera umeendelea kufanya vizuri na kushika nafasi ya tano kati ya mikoa 10 bora, Aidha mwaka 2014 Kagera ilishika nafasi ya 10 kati ya mikoa kumi bora, mwaka 2015 mkoa ulishika nfasi ya 7 kati ya mikoa 10 bora na mwaka huu umepanda juu nafasi mbili za ufaulu.

Halmashauri iliyoongoza katika mkoa wa Kagera ni Ngara iliyofaulisha kwa asilimia 87.82% na kitaifa imekuwa ya 12, mwaka jana 2015 ilikuwa ya 18. Ya pili ni Biharamulo iliyofaulisha kwa asilimia 85.11% na kitaifa imeshika nafasi ya 21, mwaka jana ilikuwa ya 3. Halmashauri ya tatu kimkoa ni Muleba liyofaulisha kwa asilimia 83.69% na kitafa kushika nafasi ya 24 ambapo mwaka jana 2015 ilishika nafasi ya 43.

Halmashauri ya nne ni Manispaa ya Bukoba iliyofaulisha kwa asilimia 83.23% na kushika nafasi ya 26 kitaifa aidha, mwaka jana ilishika nfasi ya 47. Ya tano ni Missenyi liyofaulisha kwa asilimia 78.80% na kushika nafasi ya 46, mwaka jana ilikuwa ya 19. Kyerwa ya sita imefaulisha kwa asilimia 77.60% na kushika nafasi ya 53 ambapo mwaka jana 2015 ilishika nafasi ya 68 kitaifa.

Karagwe ya saba iliyofaulisha kwa asilimia 76.79% na kushika nafasi ya 54 kitaifa ambapo mwaka jana 2015 ilishika nafasi ya 72 kitaifa. Halmashauri ya mwisho ni Bukoba iliyofaurisha kwa asilimia 74.86% na kushika nafasi ya 69 kitaifa ambapo mwaka jana ilishika nafasi ya 102, aidha, imepanda nafasi 33 kitaifa japo imekuwa ya mwisho katika mkoa wa Kagera. Shuleiliyoongoza mkoani Kagera na kuwa katika shule 10 bora zilizofanya vizuri kitaifa ni St. Achileus Chiwanuka kutoka Wilaya Muleba .

Akiongelea matokeo hayo Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Bw. Aloyce Kamamba alisema mkoa wa Kagera unaendelea kufanya vizuri na miaka ijayo mkoa huu utaweza kushika nafasi ya kwanza kama ilivyokuwa zamani. Aidha, Afisa Elimu kamamba alisema yeye na wataalam wake watafanya tathmini ya kina kujua kwanini Halmashauri ya Biharamulo imeshuka katika ufaulu ukilinganisha na mwaka jana .

Bw. Kamamba aliipongeza Halmashauri ya Bukoba kuwa pamoja na kushika nafasi ya mwisho katika mkoa kama mwaka jana lakini imepandisha asilimia za ufaulu aidha, imepanda nafasi 33 kitaifa. Bw. Kamamba alisema kuwa juhudi za walimu zimeonekana lakini akatoa wito kwa Halmashauri hiyo kuhakikisha inaongeza juhudi ili iweze kutoka nafasi ya mwisho kimkoa.

Katika hatua nyingine Afisa Elimu Bw. Kamamba alisema mkakati wa mkoa ni kuhakikisha Kagera inashika nafasi ya kwanza kitaifa ambapo yeye pamoja na timu yake ya Elimu chini ya uongozi wa mkuu wa Mkoa wa Kagera wataendelea kufanya usimamizi wa kina ili kuhakikisha kiwango cha elimu kinaendelea kupanda mkoani Kagera.

Mikoa kumi iliyofanya vizuri kitaifa ni Geita iliyofaulisha kwa asilimia 86.92% mwaka jana 2015 ulishika nafasi ya 6. Wa pili ni katavi uliofaulisha kwa asilimia 86.80%, mwaka jana ulikuwa 1, Iringa ulishika nafasi ya 3 na ulifaulisha kwa asilimia 82.87%, mwaka jana ulikuwa wa 10. Dar es Salaam umeshika nafasi ya 4 kwa kufaulisha kwa asilimia 82.59%, mwaka jana ulishika nafasi ya 2. Kagera numeshika nafasi ya 5 kwa kufaulisha kwa asilimia 80.99% na mwaka jana ulishika nafasi ya 7.

Mkoa wa sita ni Mwanza uliofaulisha kwa asilimia 79.13%, mwaka jana ulikuwa wa 3 kitaifa. Kilimanjaro umeshika nafasi ya 7 na kufaurisha kwa asilimia 79.10%, mwaka jana ulikuwa wa 4. Arusha umekuwa wa 8 kwa kufaurisha kwa asilimia 77.58%, mwaka jana ulishika nafsi ya 5. Njombe umekuwa wa 9 kwa ufaulu wa asilimia 77.10% na mwaka jana ulikwa wa 9. Tabora umekuwa wa 10 kwa ufaulu wa asilimia 71.35% na kushika nafasi ya 10aidha mwaka jana ulikuwa mkoa wa 25, wa pili kutoka mwisho.
 
TATHMINI YA MIEZI MITATU (3) YA HALI YA USHIRIKISHWAJI WA WAWANCHI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO TOKA KUANZA KWA MRADI WA "TUSHIRIKISHANE"




Hiyo[emoji115] ndio dira ya BMC. Dira hii mpk sasa imefanikiwa kwa 10% tu kwa kuwa na halmashauri na watendaji wa mitaa na kata.

Vinginevyo, ushiriki wa wananchi katika swala zima la maendeleo si wa kuridhisha. Wananchi hawafahamu kinachoendelea katika mipango na utekelezaji wa miradi yote ya manispaa na hawana jinsi ya kupata taarifa. Hii inatokana na kwamba;

-Website ya BMC inataarifa za 2012, idara ipo na inawatumishi kadhaa wengine wana masters.

-Meya hana kurasa za mitandao ya kijamii kama JF, fb, twitter, IG ambayo angeweza itumia kutoa taarifa

-Naibu meya kwa kurasa zake zote hakuna haongelei chochote cha Bkb au Nshambya ambayo ni kata yake. Anatumia kurasa zake kuongelea mambo mengine ya kitaifa.


-Mbunge kama taasisi ana ukurasa maalum fb lkn anapost mara chache sana kwa kadirio la mara moja kwa miezi miwili au hata zaidi. Mipango, utekelezaji na ahadi haviko katika ukurasa wake.

-Mkurugenzi wa manispaa ni mgeni. Lakini pia watendaji wengine wa BMC kama wakuu wa idara hawaongelei chochote popote na sheria haziwaruhusu

-Mkanasha huu wa JF ulilenga kusaidia mbunge na katibu wake pamoja na halmashaufi kujibu maswali na kuwapa mwelekeo wa halmashauri wananchi lkn bado haujatumika ipasavyo.

-Ukurasa wa katibu wa mbunge katika mitandao ya kijamii pia hauna msaada kwa yeyote anayetaka taarifa.

-Ukifika manispaa kupata taarifa yeyote unaambiwa uandike barua kwa mkurugenzi kwanza ili idara ziruhusiwe kutoa taarifa. Hivyo njii hii si rahisi sana kwakua inakua na mlolongo mrefu

-Viongozi hawajaweza kutumia radio zetu na Tv kuelezea chochote kuhusu BMC, maendeleo n.k

-Kuna njia zilipendekezwa kwenye warsha ya "Tushiikishane" za namna ya kuwafikishia wananchi taarifa kama kuandaa namba maalumu na kutuma jumbe fupi kupitia simu, bado hazijafanyiwa kazi

Katika kata kadhaa nilizopita kufatilia maendeleo ya mradi wa Tushirikishane, watendaji wake wote hawajawahi sikia kuhusu mradi, hawafahamu hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa soko kuu na stand, mtendaji wa Nyaga tu ndo alikua anafahamu kuh ujenzi wa stand. Mahojiano mbali mbali niliyofanya na wananchi wa kawaida, wengi hawafahamu chochote. Nilifanikiwa kuhoji hata bodaboda wa pale nje ya ofisi za manispaa nao hawafahamu chochote

Aidha, ninampongeza na kumshukuru Mh. mbunge pamoja na halmashauri, wameahidi kulifanyia kazi swala hili kwa haraka sana. Na kwa kuanza wameahidi kuwa baraza la madiwani litakua likirushwa moja kwa moja katika radio zetu na Tv ili wananchi wengi zaidi waweze kufikiwa na taarifa. Hii ni habari njema sana[emoji120]


Bukoba Kazi, Amani na Maendeleo!
 
Kama hukuweza kuona taarifa ya mradi ni hii hapa[emoji115]
 
Hivi kuna tofauti gani leo ukiiangalia manispaa chini ya CDM na ile ikiwa chini ya CCM (2010-2015)?, kuna tofauti gani kati ya Lwakatare na Kagasheki (2010-2015)?, kuna tofauti gani kati ya wapinzani na CCM?

Nikiwasema hawa jamaa watu wapuuzi wanakimbilia kwenye vyama na kuanza kusema we fulani eti uko CCM, maendeleo hatuhitaji tena kuanza kuchunguzana vyama, ili iweje? Usikosoe, utaitwa hivi. Usisifie, utaonekane vile, basi tu ilimradi u-vyama wao.

Naamini kabisa, hawa nao ni kama wengine tu, hawana kipya, manispaa nzima iko chini yao lakini hamna kitu. Sijuhi kwanini hawaendi hata kujifunza kwa sugu kidogo ama kwa dogo janja? Lwakatare ni mtu hasiye jituma na mwoga wa kuwasiliana, ni mbunge asiye na ubunifu hata kidogo. Kwanza miradi wanayohangaika nayo ilibuniwa wakati wa CCM, yeye ni kitu gani kawahi kubuni na kakisimamia kikazaa matunda? Tumefeli sana, it's another downfall upon our mission and vision, hatuwezi kuendelea kwa aina ya viongozi wa (kisiasa) walio chini ya mbunge ukianza na mbunge mwenyewe kwasababu hawaelewi vitu vingi sana kuanzia mawasiliano mpaka uongozi kwa ujumla. Huyo meya hata exposure hana, sasa atajifunza wapi na kwa nani?

Vyama vya siasa havina tija Tz, ni mzigo na ni upuuzi mtupu.
 
Kama hukuweza kuona taarifa ya mradi ni hii hapa[emoji115]
Kama utapata kilichoongelewa jana kwenye kikao cha maendeleo cha mkoa tunaomba utupenyezee ili tuelewe wenzetu walipokutana waliongea nini make nimemwona Prof. Tibaijuka, Meya, mb.wa karagwe n.k
 
Ahaaaaaaah! do we have any more?
Mwaka unaisha hivi hivi, kama utani vile. Every thing is just centered around bwana yule a.k.a Lwakatare.

Bwana huyu alianza mashindao aso yaweza, habari za mpango wake mwenyewe zinamzidi kilo, kawa mwepesi wa kuubeba mkonga wake mwenyewe na sasa anajificha uvunguni mwa meza kila uchao. Aje tu apulize firimbi ili mchezo uishe.
 
Suala la misaada ya waathirika wa tetemeko limeishia wapi?

Sioni kinachoendelea zaidi, au mshanogewa na senene?
 
Punguza machungu mkuu, muda ndio utakaoamua. Mji wa Bukoba eti tunazidiwa na Kigoma... Inakujia akilini kweli?
 
[emoji441]Taarifa ya Mkutano wa 'TUSHIRIKISHANE'

Napenda kutumia fursa hii kuwajulisha kuwa siku ya kesho Ijumaa Dec 2, 2016 nitakuwa mwenyeji wa Mbunge wa Bukoba Mjini, Mh. W. Lwakatare katika mkutano wa kujadili hatua za maendeleo ya vipaumbele vya Mradi wa TUSHIRIKISHANE.

Mkutano huu utafanyika kwenye ukumbi Halmashauri ya Manispaa kuanzia saa 8 mchana.

Wadau wenye maslahi na Jimbo la Bukoba Mjini mnakaribishwa kuhudhuria au kushiriki kwa njia zingine za Mawasiliano.

Asanteni kwa ushirikiano katika kuijenga Bukoba Mpya.
 
Kwanza miradi wanayohangaika nayo ilibuniwa wakati wa CCM, yeye ni kitu gani kawahi kubuni na kakisimamia kikazaa matunda?

Naomba kibali cha kudandia treni kwa mbele kuhusiana na mada 'quoted' hapo juu.

Mtazamo wangu ni, si vibaya kuendeleza miradi iliyoanzishwa na waliokutangulia ali mradi ilikuwa ya manufaa kwa jamii inayokuzunguka. Haina mantiki kubuni miradi mipya ilhali iliyokuwepo ambayo ilihitaji usimamizi wako tu inakufa kwa kisingizio cha aidha ilianzishwa na wapinzani wangu au natakiwa kubuni mipya.

Pili, ubunifu si kuunda tairi jipya. Ubunifu waweza pia kuongeza ubora kwenye tairi lililoundwa na mwingine ili kulipa maisha marefu ya kutumika, usalama, nk.

Baada ya kusema hayo naomba kusimamisha treni nishuke.

Nawasilisha,
Mentor.
 
Punguza machungu mkuu, muda ndio utakaoamua. Mji wa Bukoba eti tunazidiwa na Kigoma... Inakujia akilini kweli?
Ndugu yangu kuna mda nikiongea unanipinga sana lakini naamini kuna baadhi ya maeneo tunaelewana walau. Nikisema nchi hii wapinzani ni maneno tu na hawana tofauti na CCM unahisi nawachukia, hawa jamaa tujukubali tukatae ni mizigo na hawajitambui. Wanadai waruhusiwe kuandamana wakati mipango tu ya jimbo inawashinda kuisimamia, watu wa hivi wana faida gani? tuwatofautisheje na wale wa kijani?
 
Dada Happy habari ya mchana!
Naelekea moja kwa moja kwenye mada yako.

1. Tumeshaongea na kushauri sana kupitia chombo hiki, tunachoweza kusema ni; wewe pitia kurasa kwenye mada hii tokea nyuma utaona hayo mengi tuliyokuwa tunasisitiza, kushauri na kuchangia kwa ujumla ...ni mengi sana kusema kweli.

2. Tunaomba na tunasisitiza, mbunge na meya watambue rasmi nguvu ya mitandao ya kijamii, wajifunze kuongea, kupokea na kutoa habari pasipo shuruti. Wajifunze kwa wenzao kwasababu sie wengine hatupati nafasi kufika hapo BMC lakini kwenye mitandao tuko active kweli kweli, waache kujifungia maofisini na kujipoteza mbele ya jamii.

3. Naleta wazo la kimaendeleo. Hii ni kuhusu Uwanja wa Kaitaba. Navyojua mie ule uwanja uko chini ya BMC na si wa chama kama vingine mfano ule wa Kirumba, Kambarage n.k. Huu uwanja ni kitega uchumi, huu uwanja ni mradi mzuri sana kimaendeleo. Ukiutumia huu uwanja utawasaidia sana kukuza mapato ya BMC, hawatashindwa kupata mamilioni ya sh. kwa mwaka. Sasa nini kifanyike, watafute watu wajenge majukwaa kwa kuwekeza pale, waweke maduka n.k, waweke hotel/restaurant n.k. Waweke taa na mambo ya namna hiyo, watu wanakosa kuja kwasababu huduma nzuri hazipo. Uwanja uvutie na iwe sehemu ya kivutio cha kitega uchumi, tusikimbilie vikubwa tu wakati hivi vilivyopo vinaachwa hovyo. Tayari TFF wamesaidia vya kutosha sasa baraza la madiwani waangalie wavutie michezo, hili litasaidia ukuaji wa mapato, mji, mahoteli, utalii n.k. Michezo sahivi ni uchumi na ni fursa, wakae kimichezo na wawaze kifursa zaidi.
 
Shukran sana ndugu Rweye kwa kushiriki[emoji120]
 
BAADHI YA MAFANIKIO YA MRADI WA TUSHIRIKISHANE



Msingi wa mradi huu ni Ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za maendeleo ya Bukoba yao kama jina la mradi linavyosadifu. Hivyo pamoja na vipaumbele vyetu vinne (rejea taarifa za nyuma) ambavyo tulikubaliana kutekeleza kwa pamoja, msisitizo hasa wa mradi uko katika UTOAJI na UPATIKANAJI wa taarifa kwa wananchi ili waweze kufahamu kinachoendelea na kushiriki katika hatua zote za maendeleo.

Tumefurahi na tunampongeza Mbunge Wilfred Lwakatare kwa kuanza kulifanyia kazi swala hili mtambuka. Tunasisitiza Halmashauri pia kufuata nyayo zake. Wito huu wa kutoa taarifa pia uwafikie wadau mbali mbali wa maendeleao ya Bukoba.

Wananchi pia wanapaswa kufatilia, kuhoji na kushiriki kikamilifu kwamaana maendeleo hayataletwa na viongozi tu
 
Tangia huu mradi uanze ni mda sasa, kuna kipi ambacho tayari kimefanyika? siulizi kwa mabaya ila tu kwa maendeleo! Tuliona mmetuwekea vipaumbele vya kufanya!

Ndio tunajua kuwa mambo ya tetemeko yalirudisha michakato nyuma ila haizuii kutoa taarifa ya maendeleo ya Mradi.
Asanteni na Nawatakia utekelezaji mwema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…