TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

NDIZI BUKOBA; FURSA YA BIASHARA KWA MBEYA NA IRINGA

Leo nimeenda soko la Mabibo na jamaa yangu. Soko Zima hakuna Ndizi za Bukoba Sokoni nilipoulizia ndizi bukoba nikaoneshwa ndizi za Mbeya wao wanauza ndizi za mbeya kwa jina la Ndizi bukoba nilipowabana wakaniambia ukweli kuwa hizi ndizi za Mbeya ila Tunauza kwa kuwaambia wateja wetu kuwa ni Ndizi bukoba...Wanachofanya wafanya biashara Wanauza Ndizi za Mbeya kwa Mgongo wa Jina la Ndizi Bukoba.....Then Unanambia Bukoba ni Maskini kumbe kuna watu wanatumia jina la bukoba kuingiza kipato....Bukoba ndizi zimetoweka karagwe, Muleba, Tanzania iliwategemea ..hivi Zao la Ndizi limekumbwa na Ugonjwa Wa MNYAUKO kama Ukimwi kwa binadamu hautibiki kweli????

-Mastawil Fahamy
 
Mwisho wa siku maneno matupu hayatouvunja mfupa, matendo yatahukumu yenyewe, asante kwa mnaokuja na idea za kipi kifanyike kwa sababu inaonyesha mnajielewa na mnaelewa kuwa maendeleo ni jukumu la kila mtu na sio mchezo wa ngoja tuone kama atatoboa.

Siasa zinaendelea lakini siasa za maji taka zilikoma baada ya uchaguzi kuwaibua washindi na washindwa.

Hatua za miradi mikubwa ya ujenzi zinaendelea vizuri sana japo kwa umakini na wakati mwingine kimya kimya kukwepa masnitch wasitibue, tuendelee kuomba uzima muda sio mrefu moshi utaanza kufuka kwa mbali kuashiria moto kuwaka.

Wenye mioyo safi na nia njema kwa jimbo la Bukoba mjini tuendelee kushirikiana na kuleta hoja za kujenga na si majungu, fitna na vijembe.

Shiriki kwa vitendo kuhamasisha maendeleo ya jimbo lako sio porojo tu za kuufurahisha umma, maneno matupu hayatouvunja mfupa.

Alamsiki
 
Ukame umekuwa tishio kubwa sana kwa kipindi hiki kwa wilaya wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula
 
Ushauli au maoni?
 
Wajina nielekeze pa kuielewa vizuri hii WCY
 
Pole sana ila things have changed angalau, japo kuna ofisi za umma bado baadhi ya watendaji wanauliza we ni chama gani? Kitu ambacho hakina tofauti na uchawi
 
Asante sana dada, hizi ndizo akili za kuwashauli walioshika mpini wajue wapi waelekeze majembe yao. Good ideas kiukweli
 
Bukoba tujilaumu kwa upofu wetu kuendelea kuchagua watu kwa majina na ushabiki wa kiitikadi bila kujali ni mustakabari maisha ya sasa na vizazi vijavyo. Tunawachagua wachumia tumbo sio wapenda maendeleo.
Utamjuaje!?
 
Ni kweli usemacho mkuu, Nilisema mapema kuwa Lwakatare hawezi kutusaidia na hayupo kutusaidia zaidi ya familia yake. Alikuwa ameshachoka sana kimwili na kiakili, tulihitaji mbunge shupavu na wa kujitoa. Tumuombe Mungu tufike salama.
Tumuandae au tukuandae?
 
Serikali ina nia nzuri ila ukiona wilaya au mkoa umepewa mkuu ambaye ukuu wake umetokana na kazi nzuri katika chama chake na akakutana na halmashauri inayoongozwa na chama pinzani ujue kuna mziki, mkuu wa wilaya au mkoa kuwa kada ni taabu tupu. Wanajeshi wanapenda sana maendeleo bila fitna wala kujali itkadi za vyama.
 
Hawashindwi kwasababu hawana pesa, na suala la kuwa na dala dala za trip za mjini si suala la tajiri, ni suala la wataalamu wa hapo manispaa,hao nao ni majipu tu hamna kitu. Hawana ubunifu japo wengi wao ni magraduates
Kwa idadi ya pikipiki zilizopo mjini na ufinyu wa mji wa bukoba kuweka daladala unajipigisha. Mpaka mji upanuke
 
Nimekuwa Bukoba kwa wiki tatu ila ajabu sijaona mradi mkubwa wa maana unaotekelezwa, mbunge wetu na madiwani sijui wamekwama wapi au ni sarakasi za serikali kuu kwasababu ya Halmashauri kuwa chini ya upinzani!! Inasikitisha sana. Twafaa
Soon mambo yataanza kuonekana bro, tuvute subra
 
Kwa idadi ya pikipiki zilizopo mjini na ufinyu wa mji wa bukoba kuweka daladala unajipigisha. Mpaka mji upanuke
Mji upanuke kivipi sie tunateseka sana hasa Wa kahororo tunalipa 1000 kwenda town hivi kukiwa na daladala za mjini tukalipa 400 au mia tano haiwezakani unakuta kutoka kahororo hadi kyakairabwa 2000 mji utapanukaga lini wakati hakuna mpango wowote Wa kuupanua tutaseka wanaoishi mbali na mji .mbona mji Wa moshi na singida ambazo ni midogo kulinganisha na bk lakini INA daladala
 
Ni kweli, nauli za mizunguko ya mjini bkb ni kubwa sana. Sijui nini kifanyike maana daladala zilikuwepo Rwamishenye, Kibeta na Itahwa lakini zimepotea, hakuna hata moja tena.
 
Ni kweli, nauli za mizunguko ya mjini bkb ni kubwa sana. Sijui nini kifanyike maana daladala zilikuwepo Rwamishenye, Kibeta na Itahwa lakini zimepotea, hakuna hata moja tena.
Watu Wa kyebitembe na nshambya na migera wamefikia hatua ya kuomba hiace ya safari za bk to mtukula iwasafirishe asubuhi wakienda town na wanalipa 500 tu kutoka kyebitembe wakati kwa bodaboda unalipa 1000 SAA nyingine 1500 kwenda town na ile daladala inafanya Mara mbili au tatu asubuhi kabla ya kuanza safari zake na anapiga hela kama mnaona kazi nunua daladala 5 tu zinatosha kama majaribio waone kama watakosa watu wakusafiri maana usafiri Wa bodaboda ni mgumu na unatozo kubwa tunaomba manispaa ifanyie kazi hilo halmashauri itakosaje kuwahimiza watu kuwekeza katika biashara hiyo au watafute milioni 200 kwa ajili ya hilo swala linaonekana do go lakini linaweza ingizia halmashauri kipato na kuongeza ufanisi Wa kuleta maendeleo
 
Msipofanya haraka miradi haraka mwatelwa ccm itachukua jimbo msiiogope vitisho vya ccm hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…