TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Maruku Vanilla Tunabisha; Kagera si Masikini!
c2abdd5a3ead4bad943eac7fb0fb66e4.jpg
 
NDIZI BUKOBA; FURSA YA BIASHARA KWA MBEYA NA IRINGA

Leo nimeenda soko la Mabibo na jamaa yangu. Soko Zima hakuna Ndizi za Bukoba Sokoni nilipoulizia ndizi bukoba nikaoneshwa ndizi za Mbeya wao wanauza ndizi za mbeya kwa jina la Ndizi bukoba nilipowabana wakaniambia ukweli kuwa hizi ndizi za Mbeya ila Tunauza kwa kuwaambia wateja wetu kuwa ni Ndizi bukoba...Wanachofanya wafanya biashara Wanauza Ndizi za Mbeya kwa Mgongo wa Jina la Ndizi Bukoba.....Then Unanambia Bukoba ni Maskini kumbe kuna watu wanatumia jina la bukoba kuingiza kipato....Bukoba ndizi zimetoweka karagwe, Muleba, Tanzania iliwategemea ..hivi Zao la Ndizi limekumbwa na Ugonjwa Wa MNYAUKO kama Ukimwi kwa binadamu hautibiki kweli????

-Mastawil Fahamy
 
Mwisho wa siku maneno matupu hayatouvunja mfupa, matendo yatahukumu yenyewe, asante kwa mnaokuja na idea za kipi kifanyike kwa sababu inaonyesha mnajielewa na mnaelewa kuwa maendeleo ni jukumu la kila mtu na sio mchezo wa ngoja tuone kama atatoboa.

Siasa zinaendelea lakini siasa za maji taka zilikoma baada ya uchaguzi kuwaibua washindi na washindwa.

Hatua za miradi mikubwa ya ujenzi zinaendelea vizuri sana japo kwa umakini na wakati mwingine kimya kimya kukwepa masnitch wasitibue, tuendelee kuomba uzima muda sio mrefu moshi utaanza kufuka kwa mbali kuashiria moto kuwaka.

Wenye mioyo safi na nia njema kwa jimbo la Bukoba mjini tuendelee kushirikiana na kuleta hoja za kujenga na si majungu, fitna na vijembe.

Shiriki kwa vitendo kuhamasisha maendeleo ya jimbo lako sio porojo tu za kuufurahisha umma, maneno matupu hayatouvunja mfupa.

Alamsiki
 
NDIZI BUKOBA; FURSA YA BIASHARA KWA MBEYA NA IRINGA

Leo nimeenda soko la Mabibo na jamaa yangu. Soko Zima hakuna Ndizi za Bukoba Sokoni nilipoulizia ndizi bukoba nikaoneshwa ndizi za Mbeya wao wanauza ndizi za mbeya kwa jina la Ndizi bukoba nilipowabana wakaniambia ukweli kuwa hizi ndizi za Mbeya ila Tunauza kwa kuwaambia wateja wetu kuwa ni Ndizi bukoba...Wanachofanya wafanya biashara Wanauza Ndizi za Mbeya kwa Mgongo wa Jina la Ndizi Bukoba.....Then Unanambia Bukoba ni Maskini kumbe kuna watu wanatumia jina la bukoba kuingiza kipato....Bukoba ndizi zimetoweka karagwe, Muleba, Tanzania iliwategemea ..hivi Zao la Ndizi limekumbwa na Ugonjwa Wa MNYAUKO kama Ukimwi kwa binadamu hautibiki kweli????

-Mastawil Fahamy
Ukame umekuwa tishio kubwa sana kwa kipindi hiki kwa wilaya wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula
 
Mji umegubikwa na sintofahamu inayotokana na uoga na kutojiamini kwa viongozi.Huwezi kujua kama Manispaa inaongozwa na UKAWA zaidi ya %90 madiwani wote niwa Chama cha Demokrasia na maendeleo.(Chadema) jambo la ajabu uoga wa Meya Chief Karumuna ndo inapelekea wakosa radhi wanapitia kwenye udhaifu wao na kutukana matusi ya nguoni kama Ukimwi,Katerero,Buterangoma Mwaafaa na maneno mengine ya ovyo kama hayo nimatunda ya kupoteza nafasi kwa Meya uyo madiwani na Chama kwa ujumla wake.Mbunge kaishia kwamaneno ya mipasho ,,Mimi ni Nyani mzee nimeisha kwepa mishale mingi"Sasa nataka niwaambie Bukoba hatuhitaji nyani mzee tunahitaji Simba kijana.Mji wa Bukoba ni mchafu kila kona kunzia kwenye sura ya jimbo kukiwa na kaeneo kadogo ambapo nipachafu huwezi kufika pale pana kinyesi na vitu vingi vya hovyo.Lami mashimo hakuna tofauti kati ya utawala wa ccm na chadema.Tumechoshwa na sanaa za wanasiasa.View attachment 459556View attachment 459557View attachment 459558View attachment 459559View attachment 459560View attachment 459561View attachment 459562
Ushauli au maoni?
 
Bado kuna tatizo katika maendeleo na siasa za Bukoba Happiness huu ndiyo ukweli dada yangu...Ila tukiacha kua na misimamo kama hii
Wa chama gani huyo
Wa kabila gani
Ana nini/mali
Elimu gani anayo etc bila kuangalia mawazo ya mtu yana umuhim gani it will take long...WCY wala haitaki mtaji mkubwa wa pesa au mikopo bali uelewa na support to kutoka kwa wanasiasa maana ndivyo tulivyojijenga watanzania
Wajina nielekeze pa kuielewa vizuri hii WCY
 
Things Fall Apart. ...Kagera/Bukoba kuhamka kwenye usingizi huu ni zaidi ya KARNE..Niliwai kubuni kama kijana program inayoitwa WCY...Yaani WEALTHY CREATION TO YOUTHS ila ilikwama kwasababu ya itikadi ya kisiasa...Sasa nenda Uganda ambayo Mseveni anatumia uone kipi kinaendelea
Pole sana ila things have changed angalau, japo kuna ofisi za umma bado baadhi ya watendaji wanauliza we ni chama gani? Kitu ambacho hakina tofauti na uchawi
 
KAGERA TUNATOKAJE HAPA ...?
Mkoa Wa Kagera Tunahitaji Mikakati Imara ya kutuvusha. safari yetu bado ni Ndefu Sana....Tulipotoka, Tulipo na Tunakoelekea.........
Kabla ya Tetemeko la Ardhi mkoa Wa kagera lilotuachia Majeraha
Miezi 2 kabla ya Tetemeko la Ardhi. ilitoka Ripoti iliyoonesha Mkoa wa kagera kuwa miongoni mwa mikoa 3 Maskini Nchini.......
Ilikuwa ni ishara ya kutuamsha sisi Wananchi na viongozi wetu Wa kisiasa na watendaji kujitathimini wapi tumejikwaa na kuibua Mijadala ya kimaendeleo.......

Bahati mbaya hilo lilipita kama mengine yanavyopita likaja na tetemeko la Ardhi likajadiliwa kama mengine yaliyopita........

Kila aliyeongea maneno 10 kuanzia wananchi Wa kawaida hadi viongozi Wa kisiasa hakuna hata neno moja liloelekeza nini kifanyike (way forward, solution) zaidi ilikuwa ni kuadithia historia ya tatizo na kulalamika basi.....

Je ni kweli mkoa Wa kagera tulipaswa kuwa miongoni mwa mikoa 3 maskini nchini. Huenda ni Umaskini wetu ndio unatufanya kutegemea misaada kujenga choo, nyumba, jiko vilivyobomoka kutokana na tetemeko la Ardhi......

Hapa tatizo la msingi ni Umaskini wetu kagera ndio Tatizo......swali kwa nini sisi ni maskini na Tunatokaje kwenye kadhia hili ya Umaskini???

Mkoa Wa kagera Unaundwa na wilaya 8 kiutawala..

Wananchi wengi 85% Wanajishughulisha na kilimo. Kilimo cha biashara na chakula... Hivyo wananchi wengi ni Wakulima wadogo wenye mashamba ya wastani Wa hekta 1.5

Zao kuu la biashara ni kahawa na Ndizi baadhi ya Maeneo. Zao la kahawa linakabiliwa na changamoto nyingi zikiwezo za msululu Wa kodi karibu kodi 26 kwenye zao la kahawa ambazo mh Rais ameagiza ziondolewe,

Zana duni zinazotumiwa na wakulima Wa kahawa, Udhaifu Wa chama cha Ushirika kinachosimamia zao kahawa......

Zamani zao la kahawa liliwawezesha wakulima hawa wazee wetu kusomesha watoto wao kuendesha maisha yao baada ya mauzo lakini sasa hivi hali ni tofauti.......

Wapo wafugaji wakubwa na wadogo Wa kibiashara na kilimo...

Wapo Wavuvi wadogo na wakati katika ziwa Victoria, ziwa ikimba na mto Ngono......bado nao wanakabiliwa na changamoto ya zana za kizamani za kuvuli kama mitumbwi, nyavu..Uvuvi haramu unaopelekea samaki kupungua haraka..

Wapo Wafanyabiashara wadogo na wakubwa....Wa mazao ya kilimo na vifaa vya madukani...

Wapo wajasiriamali wadogo ( boda boda, machinga, mama ntilie, Fundi Uashi, Ujenzi, Gereji, Seremala, fundi wa ushonaji n.k hawa nao wanazo changamoto zao nyingi....

kwanza kutorasmishwa kazi zao hivyo kwenye Sera na mipango hawajadiliwi kuhusu changamoto ya mitaji, maeneo rafiki ya kufanyia biashara na kazi zao na masuala ya kodi kwao..........

Tunatokaje hapa hilo ndilo la msingi....

1. Halmashauri zetu zote lazima zibuni vyanzo vipya vya Uzalishaji hasa vile vyanzo vyenye chani ya Uzalishaji ili kutoa Ajira kwa vijana na kuongezea Mapato Halmashauri zetu..mfano Halmashauri ya Bukoba Vijijini Kuna Ziwa ikimba na MTO Ngono Tunaweza kuyatumia maeneo haya kuvutia kilimo cha Mpunga kwa kutoa mikopo maalum kwa ajili ya project hiyo au kilimo cha miwa halmashauri ikaingia Uwekezaji Wa Ubia au join venture ili kuwekeza kiwanda cha kati cha kuzalisha sukari angalau Tani 20 kwa siku......tutazalisha ajira na kuongeza mapato ya halmashauri...

2. Halmashauri zote zirasmishe shughuli za hawa wajasiriamali ili waingizwe kwenye mipango ya kibudget na mazingira rafiki ya kufanyia kazi...hawa watu wakichangamka na biashara yao kuchanganya watalipa kodi kwenye halmashauri zetu hivyo tutaongeza mapato......

3. Hivyo mabadiliko yoyote ya kuleta Mapinduzi ya kilimo kagera yanapaswa kuwa ni ya kubadilisha Mashamba Mashamba kuwa ya kisasa hivyo ni muhimu kila Halmashauri kuwa na trekta za kukodisha wakulima kwa gharama nafuuu ili kubadili kilimo cha jembe la mkono kwenda kilimo cha kisasa...

4. Kuwapatia wakulima Elimu ya kilimo bora kupitia kwa Maafisa kilimo, mashirika binafsi kwa njia ya semina au shamba darasa kwa mashamba ya mifano ya kilimo.......

Pia itolewe elimu ya kulima mazao mbadala kama Alzeti, na Mtama ni mazao yanayoweza kustawi maeneo mengi mkoa Wa kagera. Kuhimiza kupanda miti na kutolima kwenye vyanzo vya maji ili kupunguza sababu za kibinadamu zinazochangia mabadiriko ya tabia ya nchi na kupelekea Ukame maeneo mengi.....

5. Kuanzishwe mfumo Maalum Wa kukopesha wananchi maskini Mifugo kama Ng'ombe baada ya kuzaa anarudisha Ndama jike ili kukopa wengine. Utaratibu huu ulikuwepo katika mkoa Wa kagera miaka 90 chini ya shirika moja kutoka nchini Sweden... Mfumo huu uliwasaidia sana wananchi maskini katika mkoa wetu Wa kagera kwa kuwakopa mifugo hasa mbuzi na Ng'ombe....

6. Sekta ya Uvuvi bado hatujaitendea haki tuna fursa ya kujenga mabwawa makubwa ya samaki tukapata samaki Wa kutosha kwa ajili ya biashara kupitia project za halmashauri au mikopo maalum kwa ajili uwekezaji Wa ufugaji Wa samaki Wa mabwawa lakini wavuvi vijana ni muhimu kupatiwa mikopo ya nyavu zile zinazoruhusiwa na serikali na mitumbwi ya kisasa inayotumia mashine badala ya mashine za kizamani za makasia hivyo vijana watapanuka kimtaji na halmashauri zetu zitaongeza mapato pia....

7. Kila mwanasiasa anayeiongelea mkoa Wa kagera kati ya Maneno 10 angalau maneno 4 yawe ya kuonesha njia ya nini kifanyike kila sekta (way forward, solution)......tunguze blaa blaa wananchi wanaumia.....

8. Huduma za kijamii bado sio za kuridhisha jitihada zinahitajika Elimu, Afya. Mfano katika manispaa ya Bukoba mjini Elimu. Wilaya ya Bukoba mjini matokeo ya kidato cha nne 2015 . Bukoba mjini ina shule 26 zilizofanya mtihani kidato cha 4 jumla ya Wanafunzi 2218 division 1 =186=8%
Division 11=301=14% division 111=362=16%
Division iv =919=41%
Division O =450=20%
Lazima mbunge Wa bukoba mjini na halmashauri wawe na mikakati maalum kuhakikisha kiwango cha ufaulu kwa hawa watoto Wa mamantilie, watoto Wa machinga, Fundi selemara na bodaboda watoto wao wanafaulu ili waje kuzisaidia familia zao....

Huduma ya Afya bado sijaona mikakati ya wanasiasa na halmashauri za kuhamasisha wananchi kujiunga kwenye bima za Afya ili kupunguza kiasi kikubwa cha fedha wanachotumia kupata huduma ya Afya.......

9. Ni muhimu kila jimbo kuwa na kombe la mpira na baadae kuwa na kombe la mkoa Wa kagera hii itasaidia kuibua vipaji vya vijana kila jimbo hadi mkoa tutauza wachezaji wetu kwenye timu za kitaifa....tunaweza kumtaka kila mbunge agharamie kombe la jimbo na fainali za mkoa zikasimamiwa na ofisi ya mkuu Wa mkoa.....

10. Ni muhimu kuunganisha rasirimali watu Wa mkoa Wa kagera ambao wengi wao wana ukwasi mkubwa lakini wanaishi nje ya mkoa Wa kagera tunahitaji uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo na vya kati lazima fursa za mkoa Wa kagera zitangazwe kwa kiasi cha kutosha....

Kila kiongozi kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa, Diwani na mbunge lazima wawe na mpango mkakati strategic plan ya eneo lake la uongozi na namna anavyoshirikisha wananchi na fursa ya rasirimali watu wenye uwezo kufanikisha plan hizo za kiuchumi na kijamii.

Credit: Fahami Matsawili
Asante sana dada, hizi ndizo akili za kuwashauli walioshika mpini wajue wapi waelekeze majembe yao. Good ideas kiukweli
 
Bukoba tujilaumu kwa upofu wetu kuendelea kuchagua watu kwa majina na ushabiki wa kiitikadi bila kujali ni mustakabari maisha ya sasa na vizazi vijavyo. Tunawachagua wachumia tumbo sio wapenda maendeleo.
Utamjuaje!?
 
Ni kweli usemacho mkuu, Nilisema mapema kuwa Lwakatare hawezi kutusaidia na hayupo kutusaidia zaidi ya familia yake. Alikuwa ameshachoka sana kimwili na kiakili, tulihitaji mbunge shupavu na wa kujitoa. Tumuombe Mungu tufike salama.
Tumuandae au tukuandae?
 
Shida za hapo manispaa wengi si wenyeji na wana hulka ya kuchukia wenyeji Wa mkoa sijui kama wana nia yoyote ya kuendelaza mji huu.sisi wenyewe ndo wakujiogarnize na kuleta kero zote za mji na kuzitatua wenyewe ukiona imefikia hatua tunaambiwa tubebe misalaba yetu twafaa ujue serikali haina nia yoyote ya kuendeleza mkoa huu
Serikali ina nia nzuri ila ukiona wilaya au mkoa umepewa mkuu ambaye ukuu wake umetokana na kazi nzuri katika chama chake na akakutana na halmashauri inayoongozwa na chama pinzani ujue kuna mziki, mkuu wa wilaya au mkoa kuwa kada ni taabu tupu. Wanajeshi wanapenda sana maendeleo bila fitna wala kujali itkadi za vyama.
 
Hawashindwi kwasababu hawana pesa, na suala la kuwa na dala dala za trip za mjini si suala la tajiri, ni suala la wataalamu wa hapo manispaa,hao nao ni majipu tu hamna kitu. Hawana ubunifu japo wengi wao ni magraduates
Kwa idadi ya pikipiki zilizopo mjini na ufinyu wa mji wa bukoba kuweka daladala unajipigisha. Mpaka mji upanuke
 
Nimekuwa Bukoba kwa wiki tatu ila ajabu sijaona mradi mkubwa wa maana unaotekelezwa, mbunge wetu na madiwani sijui wamekwama wapi au ni sarakasi za serikali kuu kwasababu ya Halmashauri kuwa chini ya upinzani!! Inasikitisha sana. Twafaa
Soon mambo yataanza kuonekana bro, tuvute subra
 
Kwa idadi ya pikipiki zilizopo mjini na ufinyu wa mji wa bukoba kuweka daladala unajipigisha. Mpaka mji upanuke
Mji upanuke kivipi sie tunateseka sana hasa Wa kahororo tunalipa 1000 kwenda town hivi kukiwa na daladala za mjini tukalipa 400 au mia tano haiwezakani unakuta kutoka kahororo hadi kyakairabwa 2000 mji utapanukaga lini wakati hakuna mpango wowote Wa kuupanua tutaseka wanaoishi mbali na mji .mbona mji Wa moshi na singida ambazo ni midogo kulinganisha na bk lakini INA daladala
 
Mji upanuke kivipi sie tunateseka sana hasa Wa kahororo tunalipa 1000 kwenda town hivi kukiwa na daladala za mjini tukalipa 400 au mia tano haiwezakani unakuta kutoka kahororo hadi kyakairabwa 2000 mji utapanukaga lini wakati hakuna mpango wowote Wa kuupanua tutaseka wanaoishi mbali na mji .mbona mji Wa moshi na singida ambazo ni midogo kulinganisha na bk lakini INA daladala
Ni kweli, nauli za mizunguko ya mjini bkb ni kubwa sana. Sijui nini kifanyike maana daladala zilikuwepo Rwamishenye, Kibeta na Itahwa lakini zimepotea, hakuna hata moja tena.
 
Ni kweli, nauli za mizunguko ya mjini bkb ni kubwa sana. Sijui nini kifanyike maana daladala zilikuwepo Rwamishenye, Kibeta na Itahwa lakini zimepotea, hakuna hata moja tena.
Watu Wa kyebitembe na nshambya na migera wamefikia hatua ya kuomba hiace ya safari za bk to mtukula iwasafirishe asubuhi wakienda town na wanalipa 500 tu kutoka kyebitembe wakati kwa bodaboda unalipa 1000 SAA nyingine 1500 kwenda town na ile daladala inafanya Mara mbili au tatu asubuhi kabla ya kuanza safari zake na anapiga hela kama mnaona kazi nunua daladala 5 tu zinatosha kama majaribio waone kama watakosa watu wakusafiri maana usafiri Wa bodaboda ni mgumu na unatozo kubwa tunaomba manispaa ifanyie kazi hilo halmashauri itakosaje kuwahimiza watu kuwekeza katika biashara hiyo au watafute milioni 200 kwa ajili ya hilo swala linaonekana do go lakini linaweza ingizia halmashauri kipato na kuongeza ufanisi Wa kuleta maendeleo
 
Serikali ina nia nzuri ila ukiona wilaya au mkoa umepewa mkuu ambaye ukuu wake umetokana na kazi nzuri katika chama chake na akakutana na halmashauri inayoongozwa na chama pinzani ujue kuna mziki, mkuu wa wilaya au mkoa kuwa kada ni taabu tupu. Wanajeshi wanapenda sana maendeleo bila fitna wala kujali itkadi za vyama.
Msipofanya haraka miradi haraka mwatelwa ccm itachukua jimbo msiiogope vitisho vya ccm hata kidogo
 
Back
Top Bottom