TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

bukoba inakuja kwa kasi.mpaka raha.
Uko sahihi mkuu. Unajua sehemu kubwa ya manispaa/mkoa kwa ujumla ilikuwa bado iko underutilised kama pamelala hivi ndo kila mtu akawa anatukebehi na wakasahau endapo vitu vyake vikianza kutumika ipasavyo itakuwa ni kimbilio la kila mtu sasa wanaanza kukana maneno yao wenyewe. Ni jambo jema sana kwamba wananchi wanao uwezo wa kujimultiply na ukizingatia raisi kasema anataka kuifanya Kager a mkoa wa uwekezaji, tulia uone. Naamini hadi mwaka huu ukaishe tutakuwa tunaongea mambo tofauti kabisa, mambo mengi yako njiani kwa kasi isiyo ya kawaida
 
Hata mi huwa nashangaa watu wanauona Uzi tena ni wa bukoba halafu wanapita tu sijui bukoba nani alituroga yaani watu tunasahau nyumbani kiasi hicho tunahitaji sala nyingi kweli
Nadhani umimi umetutawala sana, ila tukiacha hayo tukashirikiana hata kwa kutoa maoni nadhani bado tuna nafasi ya kurudisha heshima ya mkoa wetu. Kujifanya mambo ya kagera hayakuhusu kisa upo mikoa ya watu haikufanyi mtu usiwe wa kagera Kwa hiyo kama kuna kitu hakiendi vizuri huko lazima watu wanaokujua watakunyooshea kidole kwamba mbona kwenu kuko hivi.
Ni bahati mbaya sana tunao hadi wanakagera wanaponda mkoa wa kagera wakiwa mikoa ya watu, nadhani hili linafanya watu watushangae. I believe kagera is still the best isipokuwa inahitaji mabadiliko ya kifikra kuanzia watu wanaoishi ndani ya mkoa mpaka kwa wanakagera walio nje ya mkoa
 
bukoba inakuja kwa kasi.mpaka raha.
Kumbe umeona eti.hivi sasa mji unabadirika haraka na kukua kwa kasi sana sio kama zamani ila miundombinu ASA katikati ya mji bado ni changamoto kati kati kuna udongo mwekundu ,barabara sio kubwa,mitaro nk .ningeomba manispaa ijenge barabara za mjini kati kama walivyotengeneza ya rwamishenye au ya pale kanoni yaani udongo usiwepo mjini ,kuwepo na taa na traffic light,round about za maana ,nk hapo mji wa bukoba utavutia zaidi ila kimajengo yaani ujenzi wa maghorofa na nyumba speed inaridhisha kuliko miji mingi tz
 
Bukoba isonge mbele.naimani itawezekana
Wakuu mnakaribishwa kuleta mawazo yenu ili kuendeleza mji wa bukoba ambayo ndo sura ya mkoa wa kagera.mmepotea siku hizi
Kwakweli nafurahi sana kuona mkuu Maxence Melo kwanza..ametupatia chombo huru cha habari cha kueleza maoni yetu..Pili sasa kaja hili swala la maendeleo..Kweli mkuu ubarikiwe na MUNGU na timu yako nzima.

Ratiba ya utekelezaji iko wapi ili tukienda rikizo Xmass tupitie kuona maendeleo ya utekelezaji labda tunaweza kutupia kwenye account.

Ila wewe, dah! wahenga wangelikuwepo ungepigwa adhadu, hujui ishami zamani walikuwa wanatengeneza mboga?
teh
 
Ndugu wananchi wa Bukoba,

Katika mradi wa "Tushirikishane" kwa BM tumekubaliana vipaumbele vinne ambavyo ni;

i) Ujenzi wa Soko Kuu, Soko la Kashai na Stand mpya ya Kyakailabwa

ii) Urasimishaji Makazi

iii) Mikopo kwa Wanawake na Vijana

iv) Bima ya Afya

Nitawashirikisha hatua zilizokua zimefikiwa katika vipaumbele vitatu (3) vya awali (kwa kufuata mpangilio hapo juu) kabla ya kutokea janga la tetemeko.

1. UJENZI WA SOKO KUU, KASHAI NA STAND YA KYAKAILABWA

Tayari TIB wamekubali kutoa 70% ya pesa ya kujenga soko kuu sawa na 13 billion tsh. 30% ya pesa inayobaki itatolewa na BMC ama kwa ubia au wao wenyewe.

Eneo la muda lililopendekezwa kuhamia wafanyabiashara wa Soko kuu ni eneo la KCU jiran na Rumuli na Police. Mazungumzo baina ya BMC na TIB yanaendelea ili kupata msaada wa kujenga soko la muda

Tathmini ya mazingira imekwisha fanyika kwa Stand, Soko Kuu na soko la Kashai. BMC inasubiri tu vyeti

Waliokua wakidai fidia ya eneo litakalojengwa Stand Mpya ya Kyakailabwa tayari wamekwisha lipwa.

2. URASIMISHAJI MAKAZI

Tiyari zoezi limekwishaanza Kashai na hatua iliyokuwa ikifanyika na imekamilika ni kuunda vikundi vitatu vyenye mitaa 3 kwa kila kikundi hivyo kuleta jumla ya mitaa 9 ya kata nzima ya kashai.

Vikundi hivyo vimesajiliwa na Mkurugenzi wa manispaa ili kupata haki ya kufungua akaunti na kupata stakabadhi za malipo.

Vikundi viko kama ifuatavyo:-
1. Kashenye
Kilimahewa
National Housing

2. Mafumbo
Matopeni
Lwome

3. Kashai Halisi
Kisindi
Katotolwansi

Hatua iliyokua imefikiwa ni uhamasishaji wa nyumba kwa nyumba ili wakazi watambue umuhimu wa kupimiwa wa zoezi na waende kulipia garama ya 200000 kupitia akaunti za vikundi walivyomo ili upimaji uanze baada ya malipo kukamilika.

Zoezi lilikwisha anza na pia kata Bakoba, nyumba zilizozipimwa mpk sasa ni 724 kwa mitaa miwili ya Nyakanyasi na Mtoni. Mitaa ya Forodhani na Buyekela zoezi linaendelea

3. MIKOPO KWA WANAWAKE NA VIJANA

Uhamasaishaji wa wananchi kuunda vikundi, na elimu ya mikopo na namna gani ya kupata mikopo umeanza kata ya Bakoba na Kashai

Aidha, jitihada za kufanikisha vipaumbele vya "Tushirikishane" zimesuasua wakati huu wa janga la "tetemeko" ofisi ya Mbunge na BMC kwa pamoja zimeelekeza nguvu zao katika janga. Pia wananchi wa Bukoba wanahitaji kusikia kuhusu janga na hali ya Bukoba ilivyo kwa sasa kuliko kitu kingine chochote.

Pia kuna ishara ya kuwa baadhi ya vipaumbele havitafikiwa ndani ya miezi 9 ya mradi kama ilivyokua imetarajiwa. Mfano Urasimishaji Makazi, inawezekana kusuasusa kwasababu; Kila nyumba inatakiwa kuchangia 200000/- katika kufanikisha hili ambayo ishaonekana kuwa changamoto kwa sasa; Nyumba zilizoathirika ni nyingi sana, kuna zinazoonekana zimesimama lkn hazifai kuishi ni za kujenga upya; Jitihada za serikali hazishawishi kuwa ndani ya miezi 9 watu watakua wamerejea ktk maisha yao ya kawaida. Hivyo, inawezekana swala la Kurasimisha Makazi lisipate mwitikio mzuri kutoka kwa wananchi

====Edited====

Lakini pia inawezekana kutumia janga la 'tetemeko' kama fursa, kuhamasisha wananchi wengi zaidi kujiunga na Bima ya Afya.

Hatua za mradi wa "Tushirikishane" zilizofikiwa kabla ya "tetemeko" zinatia moyo. Ni maombi yetu kuwa kipindi hiki kigumu kipite haraka.

Bwana Atuwezeshe!
Mkuu upo wapi siku hizi karibu tena
 
View attachment 404994 LEO NIMEWASILISHA RIPOTI YA KIKAO NILICHOKIFANYA NA BAADHI YA WANA KAGERA WAISHIO JIJINI DAR ES SALAAM KWA MKUU WA MKOA KAGERA.
View attachment 405000 View attachment 405001 View attachment 405002 View attachment 405003 View attachment 405003 View attachment 405003 View attachment 405004
MH. MKUU WA MKOA,

KAGERA.

MAAZIMIO YALIYOPITISHWA KWENYE KIKAO KILICHOITISHWA NA MH. WILFRED LWAKARATE(MB), MBUNGE WA JIMBO LA BUKOBA MJINI, KUJADILI ATHARI ZA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, KUONA JINSI YA KUSAIDIA WALIOPATWA NA MADHARA.TAREHE 18 SEPTEMBA, 2016 KWENYE HOTELI YA KEBBY'S, MWENGE, DAR ES SALAAM.

1. Kwa kauli moja kikao kimetambua na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua zakuridhisha kufuatia janga hili, ikiwa ni pamoja na ;
i. Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, (Mb), Waziri Mkuu, pamoja na kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Aikael Mbowe (Mb) kufika B ukoba mara moja kuona athari za tetemeko na kushiriki mazishi ya watu waliofariki kutokana na janga hili na pia kuwafariji waliojeruiwa na kuathirika kwa namna mbali mbali.

ii. Kuandaa mkutano wa kuishirikisha jumuiya ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara kwa lengo la kukusanya misaada kwa ajili ya kukabiliana na janga hili.

iii. K uandaa matembezi ya hisani kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia nakukabiliana na madhara ya janga hili.

iv. Viongozi waandamizi mbali mbali waserikali, wakiwemo Mawaziri, Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Makatibu wakuu na wakuu wa vitengo muhimu vinavyo husiana na maafa kufika kwenye eneo la tukio kwa haraka.

2. Kwa kauli moja kumuomba Mh. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ndiye baba wa nchi, pamoja na shughuli zake nyingi, kutenga siku mapema itakavyo mpendeza kufika mkoani Kagera kuwapa pole wananchi wake kutokana na janga hili. Tunaamini walioathirika watafarijika sana kumuona Rais wao akiwa nao kwenye eneo la tukio.

4. Kwa kuwa janga hili la kitaifa halina itikadi ya siasa, dini, rangi, kabila wala ubaguzi wa aina yoyote ile, hivyo ushiriki wa watu wote ni muhimu sana.

5. Kwa kutambua ukweli wa walioathirika zaidi ni wananchi wa mkoa wa Kagera, inawapasa wao kuwa msitari wa mbele katika kushiriki katika juhudi zote zinazofanyika, kwa njia na jinsi yoyote inayowezekana, iwe ni kwa hali au mali, mshikamano wao katika janga hili ni muhimu sana. Mpaka sasa, imejidhihirisha kwamba ushiriki wa wana Kagera bado ni hafifu sana. Wana kagera wanahimizwa kutokukata tamaa nakuamsha hari ya kushirikiana katika kuusaidia mkoa wao kwa nidhamu ya hali ya juu . Ili kusisitiza umuhimu huo, mfano wa kwamba ili kuweza kupewa msaada wa usafiri (lift) ni lazima uwe njiani, unahusika.

6. Kwamba kutokana na mkoa wa Kagera kukumbwa na maafa makubwa na mengi mfululizo kuanzia miaka ya 1970 zilipoanza chokochoko za nduli Iddi Amini wa Uganda, vita vya Uganda , Ukimwi, mdudu wa migomba (ekiuka), madhara ya wakimbizi kutoka nchi jirani yaliyo leta ujambazi , kufa kwa Vyama vya Msingi vya Ushirika na Chama Kikuu cha Ushirika (BCU/ KCU) kulikoambatana na kuanguka kwa bei ya zao la kahawa, kuanguka kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kulikosababisha bei za bidhaa za viwandani ambavyo vingi vipo Dar es salaam, kuwa juu kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania, ugonjwa wa mnyauko ambao umeangamiza kabisa migomba na zao lake ndizi, na sasa ni janga la tetemeko. Majanga hayo yote ni sababu kubwa kwa mkoa wa kagera kushuka sana kiuchumi kutoka kati ya mikoa mitatu tajiri miaka ya 70 - 80 hadi kuwa kati ya mikoa mitano masikini sana nchini. Serikali inaombwa ichukue hatua za makusudi kutoa upendeleo wa kisera wa kuusisimua upya uchumi (a stimulus package) kwa mkoa wa Kagera kwa kufanya yafuatayo :

i. Kutoa msamaa wa kodi zote kwenye bidhaa zote za ujenzi zinazouzwa mkoani Kagera kwa kipindi cha miaka kumi.

ii. K wa kutambua madhara ya mdororo wa uchumi wa mkoa wa Kagera kwa muda mrefu hivyo kuwepo tatizo kubwa la ajira na umasikini, miradi yote ya ujenzi wa miundombinu ya kijamii kama mashule, zahanati, vituo vya afya na majengo mengine ya serikali yatakayo jengwa upya au kukarabatiwa, ugawaji wa kandarasi ufanywe kwa mtindo wa uwezeshaji kwa makampuni yaliyopo na yanayoendesha shughuli zao mkoani kagera yenye uwezo, wakishirikiana na makampuni ya wana -Kagera walioko nje ya mkoa pale inapobidi . Vigezo vitaandaliwa ili vizingatiwe.

7. Kwa kutambua kuwa serikali imeunda kamati za maafa za Kitaifa na Mkoa ambapo Wabunge wa mkoa wa Kagera wameshirikishwa, ni vyema ushiriki kwenye kamati hizo upanuliwe na kuzijumuisha taasisi za dini ambazo mkoani kagera zimekuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii kwa miaka mingi. Hatua hii itasaidia kuongeza ufanisi katika zoezi zima la uthamini wa madhara, ukusanyaji wa taarifa na usambazaji wake. Aidha kwenye hizo kamati uwepo umuhimuwa ku wahusisha wataalam wa habari kuongeza ufanisi katika upashanaji wa habari .

8. Kwa kuzingatia mamlaka ya Mbunge anayopewa na katiba ya jamhuri ya Muungano wa T anzania, mifuko ya majimbo pia itumike kusaidia kwenye majanga yamaafa kama haya.

9. Kwa kukubali kwamba bado uitikiaji na ushiriki wa wana -Kagera bado ni hafifu sana, juhudi mpya zifanyike kwa kuishirikisha Serikali ya mkoa wa Kagera, Wabunge wote wa mkoa na viongozi wa dini zote kuitisha mkutano/ kusanyiko jingine haraka iwezekanavyo hapa dar es salaam kwa lengo la kuwashirikisha wana-Kagera na wadau wengine wote wenye mapenzi mema, katika kuonyesha kuguswa kwetu kama jamii na tatizo hili, tukusanye rasilimali kusaidia kwenye janga hili. Ndiyo njia pekee ya kuonyesha kuwa tunahitaji kupatiwa msaada wa usafiri (lift), hivyo ni vyema tukawa njiani.

NB : Katika kikao hicho cha wana kagera ahadi za jumla ya Tshs. 6,780,000/= zilitolewa na pesa taslimu Tshs. 1,480,000/= na kuleta jumla ya Tshs. 8,260,000/=

Sekretarieti iliyoundwa inaendelea kuratibu ukusanyaji wa michango hiyo ili itakapokamilika iwasilishwe sehemu husika.

Imewasilishwa leo tarehe 22/09/2016

Ofisi ya mkuu wa mkoa.

Wilfred Muganyizi Lwakatare (Mb)

Jimbo la Bukoba Mjini.

K. N.Y Wana Kagera wanaoishi Dar es Salaam (Waliohudhuria kikao hicho).

NAKALA KWA;

Mh. Waziri Mkuu.

Viongozi wakuu wa madhehebu ya kidini.

Viongozi wa vyama vya siasa.

Waheshimiwa wabunge wote wa mkoa Kagera.

Waandishi wa Habari.
Mheshimiwa tunakukaribisha tena kujibu hoja zetu huku
 
Sisi tuna nyumba pale mtaa wa uswahilini.
Ni ya late bibi.nimejaribu kuwashauli Mama zetu ambao ni warithi watuachie sisi watoto wao. Tuijenge iwe ya kisasa na vizazi vyetu baadae nao kila likizo wawe na sehemu nzuri ya kufikia. Nimegonga mwamba.
Wamepiga hesabu zao nani kabaki bk na kuna ambaye anahitaji kurudi bk kati yao.wameamua kuiuza. Kwa kuwa wao wapo Dar na majumba mazuri they dont care.
Imagine utajili tuliouweka nje ungekuwa pale town Bk ingekuwaje?
Elimu imetuharibu.
Ndio maana mchaga ambae hana elimu ya mzungu akibahatisha town anainvest kwao.
Now Moshi pana heshima sio only ya mashule bali pia uwekezaji ukilinganisha na sisi ambao tunaongoza kuwa na civilized elimu ya mzungu.
Ningeshauli ipite kwanza elimu ya kujua uthamini wa nyumbani kwanza
Umepotea mkuu
 
Kumbe umeona eti.hivi sasa mji unabadirika haraka na kukua kwa kasi sana sio kama zamani ila miundombinu ASA katikati ya mji bado ni changamoto kati kati kuna udongo mwekundu ,barabara sio kubwa,mitaro nk .ningeomba manispaa ijenge barabara za mjini kati kama walivyotengeneza ya rwamishenye au ya pale kanoni yaani udongo usiwepo mjini ,kuwepo na taa na traffic light,round about za maana ,nk hapo mji wa bukoba utavutia zaidi ila kimajengo yaani ujenzi wa maghorofa na nyumba speed inaridhisha kuliko miji mingi tz
kiukweli miundombinu mjini ndo inatuangusha wanaousika sijui ndo manispaa jengeni barabara jitahidini zamu yenu kuonesha uwezo mlionao then udongo mwekundu unaharibu taswira ya mji.na ikiwezekana wanapojenga barabara za lami wahakikishe wanaondoa kabiasa huu udongo mazingira ya barabara.kama ingekuwa mimi nimgetafuta ufumbuzi namna gan wa kuuondoa hata kwa kuleta udongo/au mchanga from one place to another japo zipo njia nyingi za kuuondoa kama wahusika wakiwa wabunifu.ni mawazo yangu kama kijana mwenye uchungu na maendeleo hasa ya bukoba na kagera kwa ujumla.
 
nimekaa nimewaza mbali sana.moyoni nikasema neno moja (NAKUJA) nikiwa namaanisha one day maisha yakininyookea nayoyatafuta lazima niwekeze sana bukoba natamani kufungua viwanda vingikiwanda cha chakula,cha ujenzi kutengeneza boat nakutoa mikopo kwa wananchi ili kuimalisha mzunguko wa hela.Ila kwa sasa sina uwezo ila nina neno moja tu kama kijana NAKUJA.Then wenye uwezo ziko oppurtunity nying sana bukoba kwa mfano iwe ziwani ufukweni mtu akijenga hoteli za kitalii kuuangalia upande wa ziwa pembeni mabot ya kuzuga kwa wale wanaotaka kutalii ziwani kabisa.ataingiza faida kubwa coz watalii wa ndani na wa ngambo lazima waje maana huo ni utalii tosha jumlisha utalii wa aina nyingine.hata wale wenye mtaji midogo kama mimi lazima kunakitu cha kufanya kwa7babu ya ubunifu na kitu hiko kiwe kizuri hata kiwe kidogo coz siku zote kuzuri chajiuza.(NAKUJA) Vijana wa kagera tuwe hata na haka kamsemo ili kuondoa maumivu na kujipa moyo ya jambo ambalo ulitamani litokee kwa namna unavyotaka lakini siyvo linavyotokea au makosa yanatokea kizembe kabisa ambapo ww ungepata nafasi hyo hakika ungeweza kubadilisha mtazamo uliopo.
 
Tuna mchanga kando mwa ziwa, mchanga huu ukiletwa kureplace ganda la udongo mwekundu basi barabara zetu zitakuwa nadhifu sana. Mfano mzuri ni nyumba za NHC, ziangalie kabla na sahivi zikiwa na rangi nyeupe.

Pili, mawe/majabari yaliyouzunguka mji mzima toka Kahororo-Kashura ni rasilimali kubwa sana, haya mawe yakisagwa tukapata kokoto za saizi ni nzuri zikatumika kuondoa udongo mwekundu kando mwa barabara zetu. Weupe wa mchanga/kokoto hizi ni mzuri kwani unag'arisha mji na kuleta mvuto zaidi kwasababu kwanza zinaakisi mwanga/mihale tofauti na udongo mwekundu uliofifia na kuleta tope mjini.

Lakini pia naamini kama barabara zikipanuliwa na kuwekewa mitaro ya vibaraza kwa juu sioni tena kama huo udongo utaonekana barabarani. Tunahitaji kutumia akili ndogo sana kuyafanya haya.

Lililo kubwa katika hili waletwa macontractors waliokuwa na sifa za maana na uzoefu wa kujenga barabara na mitalo ya hivi ama kama hao wanaojenga stand kutoka dar make hao wanaelewa jinsi ya kudili na michanga kwenye barabara ama kuzitinda/kusisakafia na si hawa wanaoitwa eti ni wazawa kumbe hamna kitu kabisa

Tunahitaji kuwa wabunifu tu mengine yote Mungu alishatupa Bkb
 
kiukweli miundombinu mjini ndo inatuangusha wanaousika sijui ndo manispaa jengeni barabara jitahidini zamu yenu kuonesha uwezo mlionao then udongo mwekundu unaharibu taswira ya mji.na ikiwezekana wanapojenga barabara za lami wahakikishe wanaondoa kabiasa huu udongo mazingira ya barabara.kama ingekuwa mimi nimgetafuta ufumbuzi namna gan wa kuuondoa hata kwa kuleta udongo/au mchanga from one place to another japo zipo njia nyingi za kuuondoa kama wahusika wakiwa wabunifu.ni mawazo yangu kama kijana mwenye uchungu na maendeleo hasa ya bukoba na kagera kwa ujumla.
Hivi sasa rwamishenye udongo mwekundu hauonekani kwa sababu ya barabara kuwa kubwa na sehemu za waenda kwa miguu zina lami wakifanya hivyo mjini kati patavuta na kupendeza sana
 
Hivi ujenzi umeshaendelea baada ya hizi sikukuu? Tupia kapicha kengine mkuu tuendelee kufurahia Bkb yetu
Sijaenda huko tena ila nitaenda jnne ila watakuwa wanaendelea kwa sababu kwa Maelezo ya meya first phase inabidi ikamilike February kadri ya mkataba itahusishwa pavement ya base ya stendi.choo na police station .na chakufurahisha zaidi wanajenga stendi mbili ya mabasi. Na daladala za mikoani zinaonekana hivyo kabla ya Christmas
1e5997288c61b5d788f3454cb923e279.jpg
25fc9d4b2138c17fc77c2658ff9be068.jpg
2d43b75e2f14adf8e60662a83dea0d7e.jpg
 
Jengo jipya la benki ya finca lililofunguliwa bukoba
2e03b799980343b8a88c02b6cde674f6.jpg
na hili linajengwa barabara ya kashura
eec2b8150c12b8def0b42b8d1b32e305.jpg
014ae2abb8e438bfc425c24f2c8c6aeb.jpg
jengo la wanajeshi chemba rwamishenye
172c0fc64721f23731aa0428b6d2d0d2.jpg
sijui watafikia ghorofa ya ngapi wamefikia ya nne nadhani ndo litakuwa jengo refu zaidi bk bukoba shopping mall inayojengwa na mmiliki wa prince motel
1fb40e504730f21c26c4cad719370326.jpg
4e5b8f70afdc9d37194ab7a91b49f012.jpg
kimsingi kimajengo bukoba inabadirika mno tunazidi kuwahamasisha wazawa warudi zaidi kujenga mji speed hii isipunguwe
 
Jengo jipya la benki ya finca lililofunguliwa bukoba
2e03b799980343b8a88c02b6cde674f6.jpg
na hili linajengwa barabara ya kashura
eec2b8150c12b8def0b42b8d1b32e305.jpg
014ae2abb8e438bfc425c24f2c8c6aeb.jpg
jengo la wanajeshi chemba rwamishenye
172c0fc64721f23731aa0428b6d2d0d2.jpg
sijui watafikia ghorofa ya ngapi wamefikia ya nne nadhani ndo litakuwa jengo refu zaidi bk bukoba shopping mall inayojengwa na mmiliki wa prince motel
1fb40e504730f21c26c4cad719370326.jpg
4e5b8f70afdc9d37194ab7a91b49f012.jpg
kimsingi kimajengo bukoba inabadirika mno tunazidi kuwahamasisha wazawa warudi zaidi kujenga mji speed hii isipunguwe
Aisee, umefanya la mbolea sana kwa hizi picha. Hiyo ghorofa ya Bkb shopping mall linajengwa maeneo gani mkuu?
 
Back
Top Bottom