TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

maeneo ilipo prince hotel karibu na hotel ya walkguard transit Uganda road
Asante mkuu kwa kurahisisha mambo, kama hutojari niliwahi ona majengo fulani kwa chini kidogo ya round about rwamishenye ...limeshafunguliwa?
 
Aisee, umefanya la mbolea sana kwa hizi picha. Hiyo ghorofa ya Bkb shopping mall linajengwa maeneo gani mkuu?
Mkuu karibu na prince IP motel mbele ya transit hotel ,barabara ya custum sasa wameshafikia ghorofa ya nne
 
Asante mkuu kwa kurahisisha mambo, kama hutojari niliwahi ona majengo fulani kwa chini kidogo ya round about rwamishenye ...limeshafunguliwa?
Hilo sijui ni nini ila kama lilishaisha vile
 
Kimsingi bk kimajengo inakua kwa kasi maghorofa yanachipua sana hivi sasa kuna maghorofa 12 yanajengwa bila kuhesabu ihungo kwa upande huo bk inakua kwa kasi ila majengo ya serikali bado kikwazo yale nhc yapo kizamani sana haya ni baadhi tu ya maghorofa
8c43f86b9364de440dda90b1ae12b21e.jpg
30d3cdc81334bd13c69ff52e4bf631c1.jpg
23b4464f5f443e78f3497d21355ab488.jpg
 
Safi sana instanbul, we tupia tu ulivyonavyo. Hii Debora Stationery iko maeneo gani hapo town?
 
naona marekebisho ya ufukiaji wa mashimo katika barabara ya manispaa yanaendelea ila wanarudio kosa lile lile tu kufukia mashimo kwa udongo
Manispaa na viongozi wake wanatumia barabara kuingiza pesa mfukoni .hivi barabara zote wakifanya walivyofanya pale stendi inashindikana? Wakipokea pesa watengeneze barabara moja baada ya nyingine ilimradi ziwe imara.manispaa wezi na wala rushwa sana ndo hicho kinarudisha manispaa nyuma hawana uchungu na mji wao na hawajifunzi kutoka manispaa nyingine
 
Hivi hawa jamaa wataacha upumbavu huu lini maana tumechoka sasa na mji kuwa udongo, haina haja ya kuwa na barabara nyingi zisizo na ubora, ni bora ziwe chache ila imara na zenye ubora
 
Kuna haja ya kuomba rais atume ofisi ya CAG ikaikague miradi na pesa zote zinazotumiwa hapo manispaa, sekta ya ujenzi ni uchochoro wa watu kujitajirisha
 
Hongereni wana Bkb kwa matokeo ya vijana wenu, hakika Mungu anafurahia kazi mnayoifanya na pesa wanazolipa wazazi hakika matunda yake yanapimwa badala ya kuishia kuzitumbua tu kama wanavyofanya kwingineko
 
Manispaa na viongozi wake wanatumia barabara kuingiza pesa mfukoni .hivi barabara zote wakifanya walivyofanya pale stendi inashindikana? Wakipokea pesa watengeneze barabara moja baada ya nyingine ilimradi ziwe imara.manispaa wezi na wala rushwa sana ndo hicho kinarudisha manispaa nyuma hawana uchungu na mji wao na hawajifunzi kutoka manispaa nyingine
Mkuu hebu tuwekee na tupicha kule kyakailabwa tuone kumefikia wapi. Sahivi kila sekta ni kama iko upande wetu vile, ujenzi, elimu na sasa boti mpya ...Mungu ana malengo nasi 2018
 
Hivi sasa Niko mwanza sio bukoba tena kwa hiyo itakuwa vigumu kuleta picha labda ambao wako bk watujulishe mie nitarudi mei huko .tuombe tu isiingiwe na migogoro kama ilivyotokea 2012 na kustopisha ujenzi Mungu awe nasi wanabk
 
Kuna habari nimeisikia ikisema mwalo wa muleba umefungwa wa magarini muleba na watu kulazimishwa kutumia soko la kimataifa la chato .jambo ambalo ni pigo kubwa kwa mkoa wa kagera maana mapato yote ya samaki yataelekezwa chato
 
Very sad aisee make ukiwepo kidogo tunakuwa na updates sana tofauti na wanaosalia huko kwao haya mambo si vipaumbele sana. Kama hauwaoni hata wakichangia hapa basi usitarajie miujiza sana kutoka kwao, all the best!
 
Kuna habari nimeisikia ikisema mwalo wa muleba umefungwa wa magarini muleba na watu kulazimishwa kutumia soko la kimataifa la chato .jambo ambalo ni pigo kubwa kwa mkoa wa kagera maana mapato yote ya samaki yataelekezwa chato
Hizo habari i kweli au source ya taarifa ni reliable? maana kuna uwekezaji ulikuwa uendelee pale ila sasa kwa jambo hilo mwekezaji anaweza akaghairi
 
Back
Top Bottom