TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

bukoba inakuja kwa kasi.mpaka raha.
Uko sahihi mkuu. Unajua sehemu kubwa ya manispaa/mkoa kwa ujumla ilikuwa bado iko underutilised kama pamelala hivi ndo kila mtu akawa anatukebehi na wakasahau endapo vitu vyake vikianza kutumika ipasavyo itakuwa ni kimbilio la kila mtu sasa wanaanza kukana maneno yao wenyewe. Ni jambo jema sana kwamba wananchi wanao uwezo wa kujimultiply na ukizingatia raisi kasema anataka kuifanya Kager a mkoa wa uwekezaji, tulia uone. Naamini hadi mwaka huu ukaishe tutakuwa tunaongea mambo tofauti kabisa, mambo mengi yako njiani kwa kasi isiyo ya kawaida
 
Hata mi huwa nashangaa watu wanauona Uzi tena ni wa bukoba halafu wanapita tu sijui bukoba nani alituroga yaani watu tunasahau nyumbani kiasi hicho tunahitaji sala nyingi kweli
Nadhani umimi umetutawala sana, ila tukiacha hayo tukashirikiana hata kwa kutoa maoni nadhani bado tuna nafasi ya kurudisha heshima ya mkoa wetu. Kujifanya mambo ya kagera hayakuhusu kisa upo mikoa ya watu haikufanyi mtu usiwe wa kagera Kwa hiyo kama kuna kitu hakiendi vizuri huko lazima watu wanaokujua watakunyooshea kidole kwamba mbona kwenu kuko hivi.
Ni bahati mbaya sana tunao hadi wanakagera wanaponda mkoa wa kagera wakiwa mikoa ya watu, nadhani hili linafanya watu watushangae. I believe kagera is still the best isipokuwa inahitaji mabadiliko ya kifikra kuanzia watu wanaoishi ndani ya mkoa mpaka kwa wanakagera walio nje ya mkoa
 
bukoba inakuja kwa kasi.mpaka raha.
Kumbe umeona eti.hivi sasa mji unabadirika haraka na kukua kwa kasi sana sio kama zamani ila miundombinu ASA katikati ya mji bado ni changamoto kati kati kuna udongo mwekundu ,barabara sio kubwa,mitaro nk .ningeomba manispaa ijenge barabara za mjini kati kama walivyotengeneza ya rwamishenye au ya pale kanoni yaani udongo usiwepo mjini ,kuwepo na taa na traffic light,round about za maana ,nk hapo mji wa bukoba utavutia zaidi ila kimajengo yaani ujenzi wa maghorofa na nyumba speed inaridhisha kuliko miji mingi tz
 
Bukoba isonge mbele.naimani itawezekana
Wakuu mnakaribishwa kuleta mawazo yenu ili kuendeleza mji wa bukoba ambayo ndo sura ya mkoa wa kagera.mmepotea siku hizi
Kwakweli nafurahi sana kuona mkuu Maxence Melo kwanza..ametupatia chombo huru cha habari cha kueleza maoni yetu..Pili sasa kaja hili swala la maendeleo..Kweli mkuu ubarikiwe na MUNGU na timu yako nzima.

Ratiba ya utekelezaji iko wapi ili tukienda rikizo Xmass tupitie kuona maendeleo ya utekelezaji labda tunaweza kutupia kwenye account.

Ila wewe, dah! wahenga wangelikuwepo ungepigwa adhadu, hujui ishami zamani walikuwa wanatengeneza mboga?
teh
 
Mkuu upo wapi siku hizi karibu tena
 
Mheshimiwa tunakukaribisha tena kujibu hoja zetu huku
 
Umepotea mkuu
 
kiukweli miundombinu mjini ndo inatuangusha wanaousika sijui ndo manispaa jengeni barabara jitahidini zamu yenu kuonesha uwezo mlionao then udongo mwekundu unaharibu taswira ya mji.na ikiwezekana wanapojenga barabara za lami wahakikishe wanaondoa kabiasa huu udongo mazingira ya barabara.kama ingekuwa mimi nimgetafuta ufumbuzi namna gan wa kuuondoa hata kwa kuleta udongo/au mchanga from one place to another japo zipo njia nyingi za kuuondoa kama wahusika wakiwa wabunifu.ni mawazo yangu kama kijana mwenye uchungu na maendeleo hasa ya bukoba na kagera kwa ujumla.
 
nimekaa nimewaza mbali sana.moyoni nikasema neno moja (NAKUJA) nikiwa namaanisha one day maisha yakininyookea nayoyatafuta lazima niwekeze sana bukoba natamani kufungua viwanda vingikiwanda cha chakula,cha ujenzi kutengeneza boat nakutoa mikopo kwa wananchi ili kuimalisha mzunguko wa hela.Ila kwa sasa sina uwezo ila nina neno moja tu kama kijana NAKUJA.Then wenye uwezo ziko oppurtunity nying sana bukoba kwa mfano iwe ziwani ufukweni mtu akijenga hoteli za kitalii kuuangalia upande wa ziwa pembeni mabot ya kuzuga kwa wale wanaotaka kutalii ziwani kabisa.ataingiza faida kubwa coz watalii wa ndani na wa ngambo lazima waje maana huo ni utalii tosha jumlisha utalii wa aina nyingine.hata wale wenye mtaji midogo kama mimi lazima kunakitu cha kufanya kwa7babu ya ubunifu na kitu hiko kiwe kizuri hata kiwe kidogo coz siku zote kuzuri chajiuza.(NAKUJA) Vijana wa kagera tuwe hata na haka kamsemo ili kuondoa maumivu na kujipa moyo ya jambo ambalo ulitamani litokee kwa namna unavyotaka lakini siyvo linavyotokea au makosa yanatokea kizembe kabisa ambapo ww ungepata nafasi hyo hakika ungeweza kubadilisha mtazamo uliopo.
 
Tuna mchanga kando mwa ziwa, mchanga huu ukiletwa kureplace ganda la udongo mwekundu basi barabara zetu zitakuwa nadhifu sana. Mfano mzuri ni nyumba za NHC, ziangalie kabla na sahivi zikiwa na rangi nyeupe.

Pili, mawe/majabari yaliyouzunguka mji mzima toka Kahororo-Kashura ni rasilimali kubwa sana, haya mawe yakisagwa tukapata kokoto za saizi ni nzuri zikatumika kuondoa udongo mwekundu kando mwa barabara zetu. Weupe wa mchanga/kokoto hizi ni mzuri kwani unag'arisha mji na kuleta mvuto zaidi kwasababu kwanza zinaakisi mwanga/mihale tofauti na udongo mwekundu uliofifia na kuleta tope mjini.

Lakini pia naamini kama barabara zikipanuliwa na kuwekewa mitaro ya vibaraza kwa juu sioni tena kama huo udongo utaonekana barabarani. Tunahitaji kutumia akili ndogo sana kuyafanya haya.

Lililo kubwa katika hili waletwa macontractors waliokuwa na sifa za maana na uzoefu wa kujenga barabara na mitalo ya hivi ama kama hao wanaojenga stand kutoka dar make hao wanaelewa jinsi ya kudili na michanga kwenye barabara ama kuzitinda/kusisakafia na si hawa wanaoitwa eti ni wazawa kumbe hamna kitu kabisa

Tunahitaji kuwa wabunifu tu mengine yote Mungu alishatupa Bkb
 
Hivi sasa rwamishenye udongo mwekundu hauonekani kwa sababu ya barabara kuwa kubwa na sehemu za waenda kwa miguu zina lami wakifanya hivyo mjini kati patavuta na kupendeza sana
 
Hivi ujenzi umeshaendelea baada ya hizi sikukuu? Tupia kapicha kengine mkuu tuendelee kufurahia Bkb yetu
Sijaenda huko tena ila nitaenda jnne ila watakuwa wanaendelea kwa sababu kwa Maelezo ya meya first phase inabidi ikamilike February kadri ya mkataba itahusishwa pavement ya base ya stendi.choo na police station .na chakufurahisha zaidi wanajenga stendi mbili ya mabasi. Na daladala za mikoani zinaonekana hivyo kabla ya Christmas
 
Jengo jipya la benki ya finca lililofunguliwa bukoba na hili linajengwa barabara ya kashura jengo la wanajeshi chemba rwamishenye sijui watafikia ghorofa ya ngapi wamefikia ya nne nadhani ndo litakuwa jengo refu zaidi bk bukoba shopping mall inayojengwa na mmiliki wa prince motel kimsingi kimajengo bukoba inabadirika mno tunazidi kuwahamasisha wazawa warudi zaidi kujenga mji speed hii isipunguwe
 
Aisee, umefanya la mbolea sana kwa hizi picha. Hiyo ghorofa ya Bkb shopping mall linajengwa maeneo gani mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…