Umaskini katika mkoa wetu Kagera na baadhi ya mikoa mingine, ulisababishwa na mambo yafuatayo:-
1.Kuanguka au kudorora kwa vyama vya ushirikika kama vile BCU,BBU,UNGA,KNPA, N.K.
2.Kushushwa bei kwa zao la buni/kahawa.
3.Kudhoofika kwa baadhi ya viwanda kama vile kiwanda cha Pepsi,kiwanda cha kahawa, n.k Sababu zote hizo zilichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mkoa wetu kurudi nyuma maana vijana wengi walikosa ajira sambamba na kukosekana mapato ya kutosha,kodi na ushuru wa kuiendesha Manispaa ya Mji wa Bukoba,hivyo ikabaki kuwa tegemezi ya ruzuku toka serikali kuu ili iweze kujiendesha.