TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Tupeni hata habari nzuri za mwenge jamani
 
Mlioko site tupeni updates za mambo kibao hapo town jamani tulioko mbali tunapenda sana kujua yaliyoko huko nyumbani, msitubanie na sie wa mbali
 
Shana iwe nabomwanyu inywenka!
Katika ishu za maendeleo sikuwahi kuona komenti yako hata ya maneno mawili ...tunahitaji komenti zako kuhusu maendeleo ya mkoa wetu na sie tutafurahi sana kwa mchango wako. Usikwazike kwa lolote lile wala kuijiweka kando na mkoa wetu Kagera kwani unatuhitaji sote
 
Mwezi February tuliona mkuu wa mkoa akiamlisha Mkandarasi wa kujenga barabara Mecco akamatwe na kufikishwa ofisini kwake huku tenda ikitangazwa upya. Tunaomba tujue baada ya hapo ni nini kilifuata na sahivi hari ikoje?

Mlioko mkoani tunaomba mmpunguze ubinafsi wa habari, habari ni nguzo kubwa sana kimaendeleo. Wanasema information is power ...tunaomba tuendelee kuhabarishana kwa yale yote yanayojiri mkoani kwetu
 
Unajua sie wanadamu wa Tz kuna kipindi najiuliza sijui tumeumbwaje sie. Yaani ukiona watu walivyobusy kwenye page ya mange alafu ulageukia page hii isivyotakiwa kuonekana kwao unabaki kinywa wazi. Kweli wazungu wameendelea kututawala sana kwa kila aina na mbinu
 
Baada ya mda mrefu wa kusota kujua na kuona habari juu ya masuala mbalimbali ya mkoa wetu yakienda mbele pasi na msaada, nimekata shauri la kurudi nyumbani kwa ajiri ya kuifanya hiyo kazi. Namuomba Mwenyezi Mungu anisaidie ili ndani ya miezi hii michache kabla ya 2019 niwe nimerejea ili kuendelea na harakati za kuukomboa mkoa wetu.

Na kama watakuwepo waliyo tayari katika kuungana nami kurudi kwenda kuwasaidia ndugu zetu basi twende pamoja na tukajitoe kwa ajiri ya watu wetu. Yako mengi ya kupeleka na kushiriki na ndugu zetu walioko huko. Tusisahau kwamba hatuna mjomba wala shangazi nje ya sisi katika kuusaidia mkoa wetu ...thus, it is our time and it is our turn.
 
Watafutiwe pengine hata kama ni viwanja vya maeneo ya bwalo la polisi kuelekea miembeni mbona kuna plots ziko wazi, kulitumia hilo eneo ni kumisuse na kuwakosesha wananchi pa kukutana na kufanya burudani kwenye mwambao wao wa ziwa. Tuchukulie mfano eneo la koko beach na walichotaka kulifanya, leo kila mmoja anapongeza maamuzi ya raisi alafu leo tunajitoa utimamu tena tunataka kurudia kosa lile lile.

Binafsi napeenda sana mkoa wetu uwe wa mfano lakini si kwa maamuzi ya hivi katu
Kweli tupu
 
Tupo sote tupo live ...tupe habari za ujenzi wa miundombinu hapo make tunajua ipo mingi tu kuanzia ihungo, barabara za W. Bank, stand n.k tupeni hata tupicha tulishe macho yetu
Ihungo inapendeza kweli yaani inaupamba mji
tapatalk_1526411544024.jpeg
tapatalk_1526411232261.jpeg
 
Ndugu Jimmy Karugenzi na viongozi wenzako mkoani Kagera, mojawapo ya ufumbuzi wa upanuzi na uboreshaji wa mji wa bukoba ni kulihamisha gereza la bkb mjini. Miji yote mikubwa na ya kisasa magereza hujengwa nje ya miji km. Butimba mwanza na segerea dsm. Gereza la bkb pale lilipo ni prime area sawa na mnazi mmoja dsm. Ni vema serikali ya mkoa ikashauriana na serikali kuu ili kutekeleza hatua hii kuacha lile eneo likajengwa chuo kikuu au complex ya biashara, makazi n.k
Ni mawazo mazuri sana sijui watayaona
 
Kamati ya CCM ya Mkoa Kagera wametoa maagizo ya kusitisha ujenzi wa soko jipya na stendi kwa sababu haijashirikisha wananchi, kampuni ishawahi kunyooshewa kidole kwenye ubadhilifu. Source: kasibante fm
Sasa sijui wamefikia wap
 
March 9, 2018 kimefanyika kikao cha bodi ya barabara {ROAD BOARD} mkoa wa Kagera, ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa uliopo manispaa ya Bukoba, ambapo imeibuka changamoto ambayo halmashauri inakumbana nayo juu ya Kampuni ya ujenzi MECCO.

Meya wa manispaa ya Bukoba Chief Kalumna amesema walipokea fedha za mradi wa barabara kutoka benki ya Dunia takribani Billion 6 na walitangaza zabuni ya ujenzi wa barabara hizo, kampuni ya ujenzi Mecco ilishinda katika mchakato huo lakini wameitwa kusaini mkataba wamekataa bila sababu zozote hali iliyopelekea manispaa kushindwa kutekeleza mradi kwa muda uliopangwa na kuamua kutangaza zabuni upya.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa Kagera Meja Jeneral mstaafu Salum Kijuu amemuagiza Mkuu wa polisi Kagera kumkamata mkandarasi huyo na kumfikisha ofisini kwake akiwa na pingu ili aweze kueleza kwa nini amesababisha usumbufu huo
Ila Bk INA siasa nyingi ndo maana haiendelei
 
Neema kagera ujenzi Wa chuo cha veta kuanza July bukoba wachina hao walikuwa bukoba kusurvey eneo
FB_IMG_15264845045981007.jpeg
FB_IMG_15264845004391835.jpeg
FB_IMG_15264844916547267.jpeg
FB_IMG_15264844869630753.jpeg
FB_IMG_15264844961586584.jpeg
 
Back
Top Bottom